Hakika ilikuwa simanzi pale mwili wa marehemu Dkt. William Shija ulipokuwa ukiagwa katika safari yake ya mwisho. Makamu wa Rais akimuelezea Dkt. Shija alisema alikuwa ni mtu wa vitendo na aliyaamini yale aliyo yasimamia huku akitolea mfano suala la uwanzishaji wa TCU taasisi ambayo inahusika na wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya Vyuo vikuu.
Naye Spika wa Bunge la Tanzania mama Anne Makinda, alisema marehemu Dkt. Shija, aliamini kuwa siasa sio ugomvi bali siasa inatakiwa itumike kufanya wengine kuwajibika kwa tija na manufaa kwa umma.
Akihubiri katika Ibada ya mwisho Paroko wa Parokia hiyo alisema, Dkt. William Shija alitumia nafasi yake kwa jamii yake na sio kujinufaisha kama ilivyo kwa viongozi wa leo, kwani viongozi wengi wa leo imekuwa kinyume kwa kujijali zaidi wao kuliko jamii wanazo zitumikia, huku akitolea mfano wa uwekaji Umeme katika mji wa Nyampande ambapo Mhe Shija alianza kupeleka Umeme kwenye nyumba za Ibada kabla hata ya kuunganisha Nyumbani kwake.
Hapa chini fuatilia kwa karibu kwa njia ya picha matukio yalivyo kuwa.
MWILI WA MAREHEMU DKT. WILLIAM SHIJA UKIWA UMEHIFADHIWA NA IBADA IKIENDELEA. |
VIONGOZI WA SERIKALI WAKIWA KATIKA VYUSO ZA HUZUNI WAKATI WA MSIBA WA WILLIAM SHIJA. |
MJANE WA MAREHEMU PAMOJA NA WATOTO WAKIWA KATIKA SIMANZI NZITO WAKATI WA IBADA YA MWISHO KWA MAREHEMU DKT WILLIAM SHIJA. |
HILI NDILO KANISA LA KWANZA KUWEKEWA UMEME KATIKA KIJIJI CHA NYAMPANDE IKIWA NI SEHEMU YA UTUME ALIO UFANYA DKT. WILLIAM SHIJA AKIWA MBUNGE WA SENGEREMA MIAKA YA 90'S. |
MAKAMU WA RAIS AKITOA HESHMA ZA MWISHO KWENYE MWILI WA MAREHEMU. |
SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ANNE MAKINDA AKITOA HESHMA ZA MWISHO. |
HAPA NI WAZIRI WA NCHI OFISI RAIS BUNGE SERA NA URATIBU. |
MKUU WA MKOA WA MWANZA EVARIST NDIKILO AKITOA HESHMA ZA MWISHO. |
DKT. TIZEBA NAIBU WAZIRI UCHUKUZI AKITOA HESHMA ZA MWISHO. |
ZITTO KABWE MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI AKITOA HESHMA ZA MWISHO MBELE YA MWILI WA MAREHEMU. |
MHE. ZITTO KABWE ALIPOKUWA AKISOMA WASIFU WA MAREHEMU DKT. SHIJA. |
WAOMBOLEZAJI WAKIWA WANASIKILIZA MAHUBIRI. |
WATOTO WA MAREHEMU WAKITOA YALE AMBAYO WALIHUSIWA NA MAREHEMU BABA YAO DKT. WILLIAM SHIJA, WAKISEMA ALIPENDA DINI NA ELIMU. |
BWANA WETENGULA MWAKILISHI KUTOKA NCHINI KENYA NAYE ALIFIKA KWA AJILI YAKUWAKILISHA NCHI YAKE NA BUNGE WALILOKUWA WAKILITUMIKIA NA DKT. SHIJA.. |
SAFARI YA MWISHO ILIVYO ANZA KWENDA KWENYE NYUMBA YA MILELE. |
MHE. DKT. BILALI AKIWEKA SHADA LA MAUWA KWENYE KABURI LA DKT. WILLIAM SHIJA, ALIPO IWAKILISHA SERIKALI KATIKA MSIBA HUO. |
Post A Comment: