Ndugu Mheshiwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa,

Ngugu Katibu Tawala Mkoa

Ngudu  Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa,

Ndugu  Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya ,

Ndugu  Waheshimiwa Wabunge,

Ndugu Wakurugenzi wa Halmashauri,

Ndugu Waheshimiwa Madiwani,

Ndugu Viongozi wa Dini,

Ndugu  Viongozi wa Vyama vya Siasa,

Ndugu Wahandisi wa Maji wa Wilaya na Mamlaka za Maji,

Ndugu Viongozi wa Chama na Serikali,

 
MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA BIBI ZAINAB TERACK ALIYESOMA HOTUBA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA MWANZA WAKATI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA KILELE CHA SIKU YA MAJI. 

Awali ya yote, ninayo heshima kubwa kuwapongezeni katika kushiriki siku hii ya kilele cha wiki ya maji Mkoa wa Mwanza, siku ambayo huadhimishwa siku kama ya leo ya tarehe 22/03 kila mwaka Duniani kote.  Ninayofuraha kunialika hapa kuwa Mgeni rasmi siku ya leo.

Ndugu wananchi,  

Wiki ya Maji huadhimishwa kila mwaka Duniani, kauli mbiu ya mwaka huu kama mlivyokwisha elezwa ni MAJI KWA MWENDELEO ENDELEVU ( WATER FOR SUSTAINABLE DEVELOPMENT).  Natumaini wiki hii imewajengea elimu na uzoefu wa kutosha kutoka kwa wageni mbalimbali walioshiriki  wiki ya Maji.

Ndugu wananchi,

Nimeambiwa kwamba wastani wa utaoji wa huduma ya Maji safi Mkoa wa Mwanza ni asilimia 61, ikiwa maelengo tuliyojiwekea katika MKUKUTA I ni asilimia 65 kufikia June 2015.  Hivyo bado tuna changamoto ya asilimia 4 ili tuweze kukamilisha kiasi kilichobaki kwa muda uliobaki. Aidha, nimeambiwa  kuwa kuna jitihada kubwa za Serikali zinazoendelea katika kuboresha huduma ya maji mijini na vijijini ikiwa ni pamoja na; kujenga miradi mipya katika Mkoa  ikiwemo  Mradi wa maji uliokamilika wa Ngudu Mjini, Ujenzi wa Mradi wa Maji unaoendelea Mjini Nansio na Sengerema, ujenzi wa miradi ya maji maeneo ya milimani Mjini Mwanza( Igogo, Ibanda, Bugarika, Mjimwema nk) na  ujenzi wa miradi ya maji vijiji vipatayo 217.

Aidha, Nimeambiwa pia kuhusu mipango mizuri iliyopo ya kuboresha miundombinu ya Maji katika Mji wa Misungwi na Magu, mradi ambao unatarajiwa kuanza mwenzi Septemba mwaka huu.

Hivyo, niwatake wahandisi wa maji wanaohusika na shughuli za miradi hii ikiwemo MWAUWASA( wanaosimamia ujenzi wa miradi ya Maji mijini), Secretariati ya Mkoa na Wahandisi wa Wilaya na Mameneja wa Mamlaka za miji midogo,  wafuatilie kwa karibu Wakandarasi wa miradi hii na kuhakikisha inakamilika kwa wakati, ubora na thamani ya fedha ionekane katika kazi hizi. Fedha nyingi Serikali imewekeza katika kuboresha huduma ya maji Mkoani Mwanza, hivyo nataka nione matokeo yanayofanana na uwekezaji huo.

Ndugu wanachi,

Niwakumbushe tu kwamba wataalamu wanasema asilimia 80 ya magonjwa yanayotupata yanahusiana na maji (yawezekana kwa kunywa au kuoga maji machafu au kukosekana kwa maji safi). Pia, maji hutumika katika uzalishaji wa vitu viwandani na shughuli zetu za kila siku za kiuchumi hususani uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo.

Hivyo, nami nakubaliana kabisa na kauli mbiu hii kuwa Maji ni muhimu katika maendeleo endelevu. Kwa pamoja tunaweza.

Ndugu wananchi,

Jukumu la kutunza na kulinda vyanzo vya maji visichafuliwe ni la kwetu sote,  Sera yetu ya maji inatutaka tusimamie miradi yetu ya maji inayokamilika kujengwa  kwa kutumia vyombo vya watumia maji kama vile bodi za maji na jumuiya za watumia maji. Kwa sasa katika Mkoa nimeambiwa tunazo jumuiya zipatazo 157 na bodi za maji 5. Vyombo hivi bado havitoshi kusimamia miundombinu yetu ya maji tuliyonayo. Sehemu nyingi bado tunatumia kamati za maji zilizochini ya serikali ya kijiji, miradi mingi iliyojengwa miaka ya 1970 ilikufa kwa sababu ya kukosekana usimamizi bora wa wananchi.  Hivyo, niwaombe Halmashauri za wilaya kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha kwamba katika kila mradi wa maji ya bomba unaojengwa, jumuiya hizi zinaundwa na kusajiliwa  kwa mujibu wa sera na sharia ya maji mapema iwezekanavyo ili ziendeshe na kusimamia miradi hii.

Ndugu wananchi.

Mtakumbuka kuwa utunzaji wa mazingira, Upimaji wa viwanja na ujenzi wa makazi bora ni vitu muhimu katika upatikanaji wa maji na uzuiaji wa majanga yanayotokana na mvua nyingi au vimbunga. Mfano mzuri ni janga la uezuaji wa paa za nyumba uliokumba wilaya yetu ya Kwimba mwezi ulioisha, nachukua fursa hii kuwapa pole wanachi wenzetu wa Wilaya ya Kwimba kwa Mkasa huo.

Niwape moyo tu kwamba Serikali ya Mkoa iko pamoja nanyi katika wakati huu mgumu.

Ndugu wanachi,

Ni matumaini yangu kuwa tutakuwa makini kushiriki shughuli za maji na usafi wa mazingira ili kuboresha afya ya jamii yetu kwa ujumla.  Pia, natumaini nyote mumefurahi na kutendea haki kilele hiki cha wiki ya Maji Mkoa. Nawatakieni safari njema mara mrudipo maeneo yenu ya kazi.

 

AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA.

BAADHI YA WAGENI  WALIOHUDHURIA KATIKA MAADHIMISHO HAYO. 

KIKUNDI CHA AKINA MAMA NGUVU KAZI KIKITUMBUIZA KATIKA SHREHE HIZO.

KATIBU TAWALA SEKSHENI YA MAJI WARIOBA SANYA AKITOA TAARIFA YA HALI YA MAJI KATIKA MKOA WA MWANZA

MTAALAM MSHURI KUTOKA MAMLAKA YA MAJI MWANZA, MWAUWASA AKITOA MAELEZO KUHUSU HALI YA MIRADI YA MAJI WANAYO ISIMAMIA KATIKA MKOA WA MWANZA.
Axact

Post A Comment: