Kufanya
makubwa zaidi 2015.
Na : Afisa Habari RS
Mwanza.
MAAFISA WA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA WAKIWA KATIKA MOJA YA ZIARA WILAYANI KUKAGUA MAENDELEO YA SHUGHULI MBALI MBALI ZA SERIKALI. |
Mkoa wa
Mwanza umeshika nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne yaliyo
tangazwa hivi karibuni kwa kupata ufaulu wa GPA 2.67, huku ukitanguliwa na Mkoa
wa Pwani (GPA 2.79) na Shinyanga (GPA 2.69) haya yamebainishwa na Afisa Elimu Taaluma katika
Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza Mwl. Gervas Sezulu wakati wa mahojiano baina
yake na Mtandao huu wa Mkoa.
Sezulu
amesema, ufaulu huo unaifanya Mwanza kuwa moja ya Mikoa inayofikia malengo ya
Mpango wa matokeo makubwa sasa yaani Big
Results Now (BRN). “Mwishoni mwa mwaka jana (2014), mitihani ya kidato cha
nne ilifanyika nchini kote na Mkoa huu wa Mwanza ukiwa ni mmoja wapo shule zetu
zote ” alisema Sezulu na kuongeza kuwa, kwa Mkoa wa Mwanza jumla ya wanafunzi
19,783 waliandikishwa kufanya mtihani huo, walifanya mtihani huo.
Amesema,
kwa matokeo ya mwaka 2013 ya mtihani huo wa kidato cha nne, Mkoa wa Mwanza
ulishika nafasi ya 12 kwa kupata ufaulu wa asilimia 39.29 hali hiyo ulifanya
Mkoa kujipanga vizuri zaidi na huku ukijiwekea mikakati kabambe itakayo wawezesha
kufanya vizuri zaidi kwa mwaka 2015.
Akibainisha
mikakati hiyo, Sezulu alisema ni pamoja na kuendelea kuwathamini walimu,
kuendesha na kutoa semina kwa walimu wote Mkoani hapo, kufanya mikutano na
viongozi wa Elimu wilaya, kuwa na mpango kazi wa ufatiliaji wa karibu katika
ngazi zote, kutoa majaribio yakutosha kwa watahiniwa wote, pamoja na kuwashirikisha
wadau wa elimu kuhusu mafanikio yanayo patikana katika Mkoa wa Mwanza.
Mkoa wa
Mwanza ambao unatekeleza mpango wa BRN uliowekewa wastani wa ufaulu wa kufikia silimia
70 ya kitaifa hali ambayo imeufanya Mkoa huo kubuni mbinu mbali mbali za
kuuwezesha kushika nafasi za juu kitaifa miongoni mwa mikoa 27 ya Tanzania,
ambapo 25 kwa Tanzania bara na miwili Tanzania visiwani.
Mbali na
matokeo ya kidato cha nne, Sezulu alisema mafanikio hayo yamefikiwa kutokana na
ushirikiano mzuri ulipo baina ya Walimu, wazazi pamoja na wanafunzi wenyewe
ambao kwa namna moja wameonekana kujituma zaidi katika masomo yao.
Mbali ya
matokeo ya kidato cha nne, Mkoa wa Mwanza umeonekana kufanya vizuri katika
elimu ya msingi kwa mwaka wa 2014,
kwakuwa katika mtihani wa kumaliza darasa la saba Mkoa ulishika nafasi ya tatu
kitaifa kwa kupata ufaulu wa asilimia 69.07 huku ukitanguliwa na Mkoa wa Dar es
Salaam ambao katika matokeo ya darasa la saba ulipata ufaulu wa asilimia 77.94
na Kilimanjaro asilimia 69.08.
Hata hivyo
Sezulu amesema wamejizatiti kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi katika mitihani
ya mwaka huu wa 2015 kwa ya Shule ya msingi lakini pia Sekondari
Post A Comment: