Na. Atley Kuni - RS Mwanza.
 
Mkoa wa Mwanza umepania kufanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne kwa mwaka wa 2015 na kuzidi matokeo ya mwaka 2014, ambapo mkoa huo ulishika nafasi ya tatu kwa shule za Sekondari pamoja na msingi.
 
Akisoma hali ya ufaulu katika mkoa huo, Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Hamis Maulidi ,alisema kwa mwaka wa 2014 walifanya vizuri katika shule za msingi na sekondari  lakini shauku yetu na adhima yao ni kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi kwa mwaka  wa 2015.
 
Maulidi aliyasema hayo wakati wa kukabidhi zawadi kwa shule, Wilaya,  na wanafunzi waliofanya vizuri kwa mwaka wa 2014.
 
Kwa upande wake kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza , Ndaro Kwilijira amewapongeza wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine na kuhakikisha mkoa unafanya vizuri "Nyie ndugu zangu mimi sina mengi lakini nawapongeza kuanzia wazazi, walimu, viongozi wa Wilaya na Mkoa kwa jitihada zenu mlizo zionesha hata kuuletea mkoa wetu sifa hii" alisem na Kulwijila na kuongeza kuwa ushindi huo isiwe ni sehemu ya kubweteka bali wwaongeze bidii na kuhakikisha tunashika nafasi za juu Zaidi.
 
 
AFISA ELIMU MKOA WA MWANZA MWALIMU HAMIS MAULIDI AKITOA TAARIFA MBELE YA WATAALAM WA HALMASHAURI NA MKOA WAKATI WAKUKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MWAKA 2014.
 

BAADHI YA WATAALAM WASHAURI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI AFISA ELIMU MKOA WA MWANZA HAMIS MAULIDI WAKATI WA UTOAJI ZAWADI ZA WASHINDI WA ELIMU MKOA WA MWANZA.
 


AFISA ELIMU WILAYA YA UKEREWE AKIPOKEA CHETI CHA USHINDI WA KWANZA KWA SHULE ZA MSINGI KATIKA MKOA HUO KWA MWAKA WA 2014.
 
KAIMU AFISA ELIMU JIJI OMARY KWESIGA AKIPOKEA CHETI CHA USHINDI WA PILI KWA SHULE ZA ZA MSINGI KATIKA MKOA WA MWANZA KUTOKA KWA KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA NDARO KWILIJIRA.
 
MZAZI WA JOVIET KAIJAGE WA  UKEREWE AKIPOKEA CHETI KWA NIABA YA  BINTI YAKE ALIYESHIKA  NAFASI YA KWANZA KIMKOA.
 
MWALIMU KUTOKA ALINCE AKIONESHA FURAHA YAKE MARA BAADA YA SHULE YAO KUZAWADIWA VYETI VINGI VYA USHINDI SHULE HIYO IMEKUWA YA PILI KIMKOA.
 

Axact

Post A Comment: