JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
OFISI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA
TAARIFA KWA UMMA.
YAH: MLIPUKO WA
UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE
Kumetokea mlipuko wa ugonjwa wa Homa
ya Nguruwe (African Swine Fever) Wilaya ya Nyamagana, Kata za Mabatini, Mirongo
kishiri na Buhongwa na Igoma. Mlipuko huu umedhibitishwa kwa uchunguzi
uliofanyawa na Maabara ya Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)
Ugonjwa wa Homa ya Nguruwe
unasababishwa na Virusi (African Swine fever virus). Madhara yake ni makubwa
kwa wafugaji na kiuchumi kwani husababisha vifo asilimia 100 (100%) kwa Nguruwe
wote walioambukizwa.
Ugonjwa wa Homa ya Nguruwe hauna chanjo wala tiba na hauambukizi
Binadamu. Njia pekee ya kudhibiti ugonjwa huu ni kuzuia kueneoa kwa
maambuzi toka eneo lenye maambukizi kwenda eneo lisiloambukizwa.
HATUA ZA TAHADHARI KUZUIA KUENEA KWA UGONJWA WA
HOMA YA NGURUWE
·
Wafugaji waepuke kununua Nguruwe
kutoka kwenye Maeneo/Mashamba yenye ugonjwa
·
Nguruwe wafugwe kwenye Mabanda imara
na waepuke kutembea ovyo
·
Nguruwe wasilishwe mizoga au masalio
ya chakula kutoka vyanzo visivyojulikana
·
Teketeza Mizoga iliyokufa kwa ugonjwa
na ufanye usafi kwa kuzingatia maelekezo ya watalaam na kwa kutumia dawa za kuua
vimelea vya magonjwa (disinfectants)
·
Wakulima watoe taarifa ya uwepo wa
ugojwa haraka kwa mtalaa wa Mifugo aliye karibu
·
Wananchi wazingatie maelekzo yote
yanaotolewa pindi watalaam wa Mifugo wanapoweka Tangazo la Karantini
(QUARANTINE) la kuzuka kwa ugonjwa wa Homa ya Nguruwe
·
IMETOLEWA
LEO 11. DESEMBA, 2015.
Dkt Yohana D. Sagenge
Kny: KATIBU TAWALA (M)
MWANZA
Post A Comment: