Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akiongea na waandishi wa habari juu ya kulaani vitendo vya mauwaji kwa kujichukulia sharia mikononi kwa baadhi ya watu. |
Mkuu wa mkoa wa Mwanza akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari. |
Hapa Mkuu wa Mkoa alikuwa akikemea juu ya tabia ya waandishi wa habari kununuliwa na nakuanza kuandika watu vibaya. |
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, pichani ni Mwandishi wa Mtanzania Benjamini Masese wakwaza kushoto. |
Na: Afisa habari- Mwanza.
Serikali
mkoani Mwanza imelaani mauwaji yaliyofanywa na mfanyabiashara maarufu jijini
humo Jumanne Mahende(J4) hivi karibuni katika eneo la Nyakato Sokoni katika
Wilaya ya Ilemela mkoani humo.
Tamko
hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo wakati akiongea na
waandishi wa habari ofisini kwake mapema hivi leo, akitoa tamko hilo mbele ya
waandishi wa habari, Mkuu wa mkoa wa Mwanza amesema sio kitendo kinacho kubalika wala
kuhalalishwa na mtu yeyote mwenye roho ya binadamu.
Mulongo
amesema, hata wavumilia wala kuwachekea watu wanao thubutu kutoa uhai wa mtu
kwa kisingizio cha madeni, “nataka wananchi wafahamu hakuna mbadala wa uhai wa
mtu, kama Serikali ya mkoa, wataiomba mahakama iweze kutenda haki pale ambapo
ushahidi utakapojitosheleza ili haki ipatikane.
Aidha,
amesema hakuna mtu aliye juu ya sheria na kuamua kutoa uhai wa mtu mwingine. ”Ndugu
zangu nataka kila mmoja wetu afahamu hakuna mbadala wa maisha au uhai wa mtu,
haiwezekani mtu afanye mauwaji halafu aachwe aendelee kutamba kwa kusema yupo
karibu na vyombo vya usalama, mimi kama mkuu wa mkoa nataka umma ufahamu kuwa
tunataka kuongoza watu kwa amani na utulivu na ikitokea mmoja hataki kufuata
utaratibu lazima sheria ifuate mkondo wake.
Waandishi wa wakimsikiliza Mulongo. |
Alisema
“ kuondoa haki ya mtu kuishi na kufanya
wategemezi wa familia kuwa wategemezi kwa watu wengine kitu ambacho kina dumaza
uchumi wa mtu mmoja mmoja, jamii lakini uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla.
Wakati
huohuo ameiomba jamii ya wanamwanza kutoa ushirikiano wa dhati kwa kutoa
taarifa kwa vyombo vya dola pindi wanapo ona kuna viashiria vya uvunjifu wa
amani huku akiahidi kusimama kidete na kuona haki inatendeka kikamilifu.
Mbali
ya kutoa karipio hilo, mkuu huyo wa mkoa ametumia wasaa huo kutoa taarifa ya
uandikishaji wapigakura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa
BVR katika mkoa huo na kusema mkoa umevuka lengo kwa kufikisha asilimia 103,
ambayo ni mafanikio makubwa kutokana na malengo waliyo jiwekea hapo awali.
Alisema
hapo awali mkoa ulijiwekea malengo ya
kuandikisha watu 1,403,743 lakini kutokana na maandalizi na mipango mizuri ya mkoa
wamefanikiwa kuandikisha watu 1,442,391 sawa na asilimia 103.
Akitoa
mchanganuo huo kwa kila jimbo alisema Jimbo la Nyamagana wameandikisha watu (273,636).
Ilemela (234,879), na Sengerema (153,054), majimbo mengine ni Buchosa (158,510),
Misungwi (149,535), Magu (147,155),Kwimba (86,273), Sumve (76,466) na Ukerewe (162,883).
Mkoa
wa Mwanza kwa mujibu wa Sensa ya watu wa makaazi ya Mwaka 2012 ulikuwa na watu
wapatao Mil.2.7.
Mwisho.
Post A Comment: