ASKARI JESHI KWENYE SIKU YA MASHUJAA JIJI MWANZA, HAPA WAKILIPUA RISASI HEWANI KUWAKUMBUKA MASHUJAA WALIOJITOLEA KWA NCHI YAO KATIKA VITA YA PILI YA DUNIA 1939-1945. |
Serikali
Mkoani Mwanza Imekeme tabia ya watu wanaohubiri mambo ya ukabila katika karne
ya sasa wakati mkoa huo ukiwa kwenye maadhimisho ya siku ya mashujaa
yaliyofanyika kwenye mviringo wa makutano ya barabara ya Nyerere, Kenyatta na
makongoro jijini Mwanza.
Akihutubia
Mamia ya wananchi hao, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magessa Mulongo, amesema
ameshangazwa na tabia ya baadhi ya wanasiasa kuhubiri habari ya ukabila kwenye
karne ya sasa hasa kipindi hiki tunacho elekea kwenye uchaguzi mkuu.
MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKITOA HOTUBA FUPI. |
”Nimeshangazwa
na ndugu zetu wa Chadema, juzi wamekuja hapa eti wamekuja kuwaambia wanamwanza,
kuwa Magufuli sio msukuma” alisema Muolongo na kuhoji yaani kweli hiyo ndio
meseji mtu aliyo kuja nayo? Amakweli duniani hapa kuna watu wana akili isiyo
nzuri alisisitiza Mulongo, na kuuliza hiyo kwa watu wa Mwanza inamaana gani? “
Unapokuja na gari la udini unataka kuwaambia nini, na kusema, Ezekiel Wenje,
alichaguliwa na wanamwanza lakini sio msukuma yeye ni Mshashi wa Mara lakini
pia Highness alichaguliwa na kuongoza Ilemela lakini yeye ni Mchaga wa
Kilimanjaro. Nilazima wakati mwingine na nyie wananchi muwe mnapima watu kwa
hoja zao, sio mtu anakuja hapa mkutano mzima yeye ni kutukana tuu na kusema
mambo ya hovyo mwanzo hadi mwisho.
BASE KAMANDA CANAL KIVAMBA AKIPOKEA SIME TAYARI KWA KUWEKA KWENYA MNARA WA MASHUJAA. |
Katika
hatua nyingine, amekemea tabia ya baadhi ya vijana wanaopita mitaani mara baada yakumaliza mikutano ya siasa na
kuanza kubugudhi watu wenye biashara zao, ”Umemaliza kusikiliza mkutano wa
siasa nenda nyumbani kwako kimya kimya” tabia
yakupita mitaani na kuanza kuwakera watu wengine wenye biashara zao sio kitendo
kinacho vumilika hata kidogo na niwaombe tu vijana wenzagu, kwamba kwa atakaye
thubutu kufanya hivyo tena sinto mvumilia” kwa mara ya kwanza niliwazuia askari
kuwachukulia hatua lakini niseme, kwa atakaye kiuka utaratibu huo sinto muonea
haya wala aibu eti kwakuwa tu kuchukua hatua utalalamikiwa, haiwezekani mtu
yeye avunje sheria halafu aangaliwe na hakuna mtu aliye juu ya sheria aliongeza
Mulongo.
Hata
hivyo ameviagiza vyombo vya ulizi na usalama kuhakikisha vinasimamia kikamilifu
ulinzi na usalama na kuhakikisha kila mchakato unapita salama katika kipindi
hiki na maisha mengine yanaendelea kama kawaida.
Awali
kabla ya kutoa maonyo hayo, Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza juu ya uzalendo wa
mtu mmoja mmoja na umuhimu wa kutunza amani” Ndugu zangu yamkini kama tungempa
nafasi mzee wetu Sadalla aeleze kile walichokutana nacho miaka hiyo hangetamani
kirudie tena, lakini hata wenyewe mmeshuhudia hiki walichokuwa wakifanya askari
wetu hapa na hii ilikuwa ni maonesho tu ,sitaki kusema mengi tuitunze amani
kwakuwa hakuna mbadala wa amani, badala ya Amani ni Vita.
MZEE IBRAHIMU SADALA ASKARI MSTAAFU WA KAR AKIFANYA MAHOJIANO NA AFISA HABARI WA MWANZA. |
Naye
kwa upande wake Mzee Ibrahimu Saddala aliyepigana vita vya pili vya Dunia(KAR)
mwenye umri wa miaka 90 kwa hivi sasa, alisema kila anapokumbuka hali
ilivyokuwa hatamani kusikia habari ya vita huku akiwataka watanzania kuilinda
amani kama mboni ya jicho. ”Mimi niliingia jeshi wakati ule nikiwa na miaka
kumi na tisa na ndio kwanza nilikuwa nimemaliza shule, tukaja
tukachukuliwa na kwenda kujiunga jeshi
tukaenda hadi Bama wakati huo tukiongozwa na wazungu” anasema Mzee Saddala na
kuongeza kuwa “pamoja na kwamba vita ile iliniwezesha kupata pesa yakununua
nyumba kwa shilingi miasaba (700) hapa Mwanza lakini kitu ambacho sitaki
kukumbuka ni hali ilivyo kuwa pamoja na umri wangu huu”.
Mzee
Saddala mwenye umri wa miaka tisini kwa sasa, ni miongoni mwa watu
wachache waliosalia kati ya walipigana vita kuu ya pili ya Dunia kati ya
Mwaka 1939-1945 na kwa sasa anaishi jijini Mwanza lakini pia ni mwenye nguvu na
kuweza kutembea yeye mwenyewe kwa kutumia fimbo ndogo aina ya mkongojo inayo
msaidia.
Imeandaliwa na Afisa
habari Mwanza zaidi na picha isome kupitia
ASKARI JESHI WAKITOA HESHMA ZAO WAKATI WA MAADHIMISHO HAYO YALIYOFANYIKA LEO. |
HAPA ASKARI WA GWARIDE WAKIPOKEA MAELEKEZO KUTOKA KWA MMOJA YA VIONGOZI WAO NAMNA YAKUKABIDHI ZANA HIZO KWA VIONGOZI WATAKAO WEKA KUMBU KUMBU. |
HAPA VIONGOZI WA DINI WAKIA WANASIKILIZA KWA MAKINI MAZOEZI YA GWARIDE LA MASHUJAA. |
MPIGANAJI WA KAR KITENGO CHA SIGNO, IBRAHIMU SADALLA, AKIWA AMEMALIZA KUWEKA SHOKA KATIKA MNARA WA KUWAENZI MASHUJAA WA VITA YA PILI YA DUNIA. |
Post A Comment: