PICHANI MBIO ZA MWENGE ZILIPO WASILI KATIKA WILAYA YA MAGU NA HAPO NI KATIKA ENEO LA NYANGUGE. |
MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKIUPOKEA MWENGE WA UHURU WAKATI UKITOKEA KATIKA MKOA WA SIMIYU SIKU YA TAREHE 28.08.2015. |
KATIBU TAWALA WA MKOA WA MWANZA DKT. FAISAL ISSA WAKATI WA MAPOKEZI YA MWENGE MKOANI MWANZA NA HAPA ALIKUWA AKIMPOKEA KIONGOZI WA MBIO HIZO BW. JUMA KHATIB CHUM |
MKUU WA MKOA WA MWANZA ALIPOKUWA AKIWAHUTUBIA WANANCHI WALIOKUSANYIKA KATIKA ENEO LA KIJIJI CHA NSOLA WAKATI WA MAPOKEZI YA MWENGE. |
VIJANA WA SHULE WAKIWA KATIKA MOJA YA MIKUSANYIKO YA MWENGE MWAKA 2015. |
KIONGOZI MKUU WA MBIO ZA MWENGE 2015 JUMA KHATIB CHUM AKIMTWIKA MAJI MMOJA YA WAKINA MAMA KATIKA WILAYA YA MAGU. |
Kama inavyo fahamika kila mwaka Mwenge wa uhuru hukimbizwa kote nchini na mkoa wa Mwanza kama iliyo kwa mikoa mingine mkoa wa Mwanza hupitiwa na mbio hizo na hapa pata kufahamu jinsi mwenge ulivyo pita na miradi iliyopitiwa na Mwenge huo.
Mwaka 2015,
Jumla ya miradi 64 yenye thamani ya Tshs. Billioni 18,497,953,314 itaweza
kufikiwa Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Mwanza. Katika miradi hiyo, Miradi 15 yenye
thamani Tsh. Bilioni 10,167,443,654 itawekewa mawe ya msingi, miradi 21 yenye
thamani ya Tsh. Bilioni 1,353,151,574 itazinduliwa,
na miradi 28 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 6,977,358,086 itafunguliwa.
Miradi yote
imegharamiwa na serikali kuu Tsh. Bilioni 5,296,616,637. Halmashauri Tsh. Bilioni
2,109,308,123. Nguvu za wananchi Tsh. Bilioni 2,680,133,700 pamoja na wahisani mbalimbali
ambao wamechangia Ths. Bilioni 8,411,854,854. Miradi hii ipo katika sekta za
elimu, afya, barabara, maji, utawala bora, vijana, wajasiriamali, biashara,
kilimo na ufugaji.
Je nini Ujumbe wa Mwaka huu.?.. Mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Kama mnavyofahamu ujumbe wa mwaka huu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
unasema “Tumia haki yako ya
kidemokrasia: jiandikishe na kupiga kura katika uchaguzi wa 2015”. Ujumbe huu ni muafaka
kabisa kwa wakati huu na hasa ikifahamika kuwa tarehe 25 Oktoba, 2015
kutakuwepo na upigaji wa kura ili kuchagua viongozi ambao ni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani. Niwapongeze wale wote waliotumia haki yao ya
kikatiba na kisheria ya kujiandikisha na kupewa kitambulisho cha mpiga kura.
Kujitokeza kwenu kwa wingi mumewezesha mkoa wa Mwanza kuvuka lengo la
uandikishaji kwa asilimia 103 ambapo
jumla ya watu 1,442,391 waliweza
kuandikishwa. Ombi langu kwenu, ni kuvitunza vitambulisho mlivyopewa na siku
ikifika, nendeni kwenye vituo mlivyojiandikisha
ili kupiga kura. Mkoa umejipanga
kuhakikisha amani na utulivu vinatawala kipindi chote cha uchaguzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa mkoa hasiti kutia msisitizo wa ujumbe wa kudumu.....
Pamoja na ujumbe mkuu wa Mbio za Mwenge wa uhuru 2015, upo ujumbe wa kudumu ambao unahimiza wananchi kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa
UKIMWI, Malaria, Rushwa na Dawa za kulevya. Takwimu za mkoa zinaonesha kuwa
maambukizi ya UKIMWI yanazidi kupungua kutoka wagonjwa 979,035 mwaka
2009 hadi kufikia wagonjwa
367,545 mwaka 2014 ambapo kiwango cha maambukizi katika Mkoa ni asilimia 4.2 kwa mwaka 2014.
Mkuu wa Mkoa wa mkoa analiona janga la dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI.
Ombi langu kwa watanzania mnaonisikiliza na hasa wanaotumia dawa
za kufubaza virusi vya UKIMWI wasiache kuzitumia. Wakiacha kwa sababu yo
yote ile wanavipa vijidudu nafasi kujiimarisha na hivyo kuhatarisha maisha
yao. Tuendelee kuwasaidia
wenzetu walioathirika na kuwahudumia badala ya kuwanyanyapaa na
kuwatenga. Na, muhimu zaidi tuwasaidie watoto yatima na wazee ambao
wameachwa bila msaada wowote.
Vipi suala la Rushwa?
Mwaka huu, katika Mbio za Mwenge wa Uhuru naomba nikumbushe
wajibu wa kila mmoja kupambana na
rushwa, kwa kauli mbiu isemayo “kata mnyonyoro wa rushwa: chagua
kiongozi Mzalendo’. Ujumbe huu unakwenda
sambamba na juhudi za serikali za kupambana na rushwa nchini. Tunafahamu
kuwa rushwa ni adui wa haki na kikwazo kikubwa cha maendeleo ya jamii na
taifa. Nchi ikiwa imegubikwa na vitendo vya rushwa itakosa maendeleo
stahiki na watu watadhulumiwa haki zao. Kwa mfano, kwa kipindi cha
miaka mitatu, yaani kati ya 2010 hadi 2013, zaidi ya shilingi bilioni 28 zimeokolewa ambazo zingeweza kunufaisha
watu wachache wanaoendeleza vitendo vya rushwa. Naomba wananchi waendelee kutoa taarifa zitakazosaidia
kuwatambua na kuwakamata watoaji na wapokeaji rushwa.
Mkuu wa mkoa analiona suala la dawa za kulenya kama kikwazo cha maendelea je! anasema nini?
Tatizo la biashara na matumzi ya dawa za kulevya limeendelea kuwa
moja ya changamoto kubwa zinazolikabili taifa letu. Serikali imeendelea kufanya
jitihada kubwa kupambana na changamoto hiyo. Ugumu wa kazi hiyo unaletwa
na ukweli kwamba watu wanaohusika ni wengi na wanazidi kuongezeka kila kukicha
kwa tamaa ya kupata utajiri wa haraka.
Serikali haitachoka kufanya kila tuwezalo kupambana na uhalifu huu
mpaka ushindi upatikane, ikiwa ni pamoja na kutumia vikundi na taasisi
mbalimbali za uelimishaji wa mabadiliko ya tabia. Wakibadili mbinu nasi
tutabadili maarifa ya uchunguzi na utambuzi mpaka tuwapate. Kwa mfano, kuanzia
Januari hadi Septemba, mwaka huu (2015) watu
2000 (wafanya biashara na watumiaji wa dawa za kulevya) wamekamatwa.
Mashamba kadhaa ya bangi yameteketezwa, na aina mbalimbali ya dawa za kulevya
ikiwa ni pamoja na kilo 681 za
dawa hatari ya heroine, zimekamatwa na watuhumiwa wamefikishwa kwe Mkondo wa sheria. Nawaomba sana ndugu zangu na wananchi
wenzangu mshirikiane na vyombo vya dola katika kupambana na usafirishaji,
uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya.
Baada
ya kutoa salamu hizi nachukua nafasi hii kuwaribisheni Mkoani Mwanza na
najisikie mko nyumbani,
NAWATAKIA KILA LA HERI! ASANTENI KWA
KUNISIKILIZA.
Post A Comment: