Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Articles by "Uzalendo."
Showing posts with label Uzalendo.. Show all posts
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
![]() |
| RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGULI ALIPOKUWA AKITANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI KUSHOTO NI MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU NA KULIA NIA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA. |
Magufuli:
Kumekuwa na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua
baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa
angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza.
Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na mawaziri na manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi kukaa bila baraza, katika baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri.
Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani.
WIZARA
Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora: Mawaziri ni George Boniface Taguluvala Simbachawene na Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, Naibu waziri Selemani Saidi Jafo.
Ofisi ya makamu wa Rais, muungano na mazingira: Waziri ni January Yusuf Makamba, naibu Luhaga Mpina
Ajira, walemavu: Jenista Joakim Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Abdallah Possi. M ambae ni mhadhiri Dodoma
Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu: Waziri ni Jenista Muhagama, manaibu Anthony Mavunde, Possy Abdallah.
Kilimo, mifugo na uvuvi: Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba, naibu William Ole Nasha
Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri mhandisi Edwin Ngonyani.
Fedha na mipango: Waziri bado tunamtafuta, naibu waziri ni Ashantu Kizachi
Nishati na madini: Waziri ni Professa Sospeter M. Muhongo, Naibu waziri ni Medalled Karemaligo
Katiba na sheria: Waziri Harrison George Mwakyembe
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa: Waziri ni Augustine Philip Mahiga ambae nimemteua kuwa mbunge na kisha waziri, Naibu ni Dr Suzan Kolimba.
Ulinzi na kujenga taifa: Waziri ni Dr. Hussein Ali Mwinyi
Mambo ya ndani: Charles Muhangwa Kitwanga
Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi: Waziri ni William Vangimembe Lukuvi, Naibu Angelina Mabula
Maliasili na Utalii: Waziri bado, naibu ni Ramo Makala
Viwanda, biashara na uwekezaji: Waziri Charles John Poul Mwijage
Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi: Waziri bado hajapatikana, Naibu ni Stella Manyanya
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto: Waziri Ummy Ally Mwalimu, Naibu ni Hamisi Andrea Kigwangalla
Habari, utamaduni, wasanii na michezo: Waziri Nape Nnauye, naibu Anastazia Wambura
Wizara ya maji na umwagiliaji: Waziri Makame Mnyaa Mbarawa ambae nilimteua kuwa mbunge, Naibu ni Isack Kamwela
=====================
Swali: Kuna baadhi hukutaja, tatizo ni nini hasa kwa wizara ambazo hujateua? Wabunge wa chama chako hawana sifa? Usimamizi wa baraza unatarajia zitafanya kazi zake Dodoma ukiondoa TAMISEMI?
Magufuli: Nilitegemea ungeniuliza kwanini sikuteua siko niliyoteuliwa, subira yavuta heri, hawa wameanza na wengine watafata. Usiwe na haraka. Kuhusu Dodoma tutatekeleza yaliyoko kwenye ilani ya chama cha mapinduzi.
Swali: Umesema hakutakuwa na semina elekezi, utafanya nini waweze kwenda na kasi ya hapa kazi?
Magufuli: Niliyowachagua wote wana CCM na wengi wao ni wabunge, walinadi ya sera hapa kazi na ndio maana haja ya semina elekezi, spidi ni hiyo hiyo ndio maana hatutatumia semina elekezi ya bilioni mbili.
Manyerere Jackton: Kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na kwa kulinganisha na tulipotoka, serikali itakuwa imepunguza kiasi gani?
Magufuli: Wewe ndie utapiga hesabu, kwa vile ni mmiliki wa gazeti huwa unapiga hesabu huwa unapata kiasi gani. Utanisaidia katika kupunguza baraza tutakuwa tumesevu kiasi gani na zile tulizosevu za gharama elekezi, kuchelewa kutangaza baraza na wale ambao sijawataja na bahati nzuri nyie waandishi mnaweza kupiga hesabu vizuri. Zipo nchi zina mawaziri wengi mpaka kufikia hata 70, wizara 44, manaibu na mawaziri. Tutakapomaliza tutakuwa na baraza la watu 34 tu.
Wakienda kule mawaziri wakafanye kazi kweli ndio maana sisi tulipochaguliwa tulifanya kazie kweli na hatukwenda kwenye semina elekezi na tulijielekeza, wakajieleze kwenye maeneo yao.
Wasihangaike kufanya sherehe kwa sababu ni kazi ngumu na kama wapo wanaopenda kufanya sherehe wajiandae kufanya sherehe siku wakifukuzwa, contract ni miaka mitano. Wakawafanyie kazi watanzania bila kuwabagua, Baraza hili la wizara 15 tumejiridhisha linaweza kufanya kazi tunayowatarajia kuifanya effectivly. Ngoja tukimaliza uteuzi wote tutajua tumesave kiasi gani ili ziweze kwenda kwa wananchi.
Raymond(Uhai Production): Siku saba zimetimia, wafanyabiashara wamesharesha zile hela?
Magufuli: Swali hilo kamuulize kamshna wa kodi TRA.
SWALI: Kuna wizara ina mawaziri wawili, huko kazi ngumu?
Magufuli: Kafanye utafiti hio wizara imeunganisha wizara ngapi, utapata majibu.
Swali: Katika baraza, kuna mawaziri wa baraza lililopita, ulizangatia nini wakati wa uteuzi?
Magufuli: Umekosea hata kupiga hesabu, Kafanye hesabu vizuri, waliorudi ni saba na sio kumi? Ukipiga utaelewa ni vigezo gani nilivyotumia.
Asanteni sana na ninawashukuru

| PICHANI MBIO ZA MWENGE ZILIPO WASILI KATIKA WILAYA YA MAGU NA HAPO NI KATIKA ENEO LA NYANGUGE. |
![]() |
| MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKIUPOKEA MWENGE WA UHURU WAKATI UKITOKEA KATIKA MKOA WA SIMIYU SIKU YA TAREHE 28.08.2015. |
![]() |
| KATIBU TAWALA WA MKOA WA MWANZA DKT. FAISAL ISSA WAKATI WA MAPOKEZI YA MWENGE MKOANI MWANZA NA HAPA ALIKUWA AKIMPOKEA KIONGOZI WA MBIO HIZO BW. JUMA KHATIB CHUM |
![]() |
| MKUU WA MKOA WA MWANZA ALIPOKUWA AKIWAHUTUBIA WANANCHI WALIOKUSANYIKA KATIKA ENEO LA KIJIJI CHA NSOLA WAKATI WA MAPOKEZI YA MWENGE. |
![]() |
| VIJANA WA SHULE WAKIWA KATIKA MOJA YA MIKUSANYIKO YA MWENGE MWAKA 2015. |
![]() |
| KIONGOZI MKUU WA MBIO ZA MWENGE 2015 JUMA KHATIB CHUM AKIMTWIKA MAJI MMOJA YA WAKINA MAMA KATIKA WILAYA YA MAGU. |
Kama inavyo fahamika kila mwaka Mwenge wa uhuru hukimbizwa kote nchini na mkoa wa Mwanza kama iliyo kwa mikoa mingine mkoa wa Mwanza hupitiwa na mbio hizo na hapa pata kufahamu jinsi mwenge ulivyo pita na miradi iliyopitiwa na Mwenge huo.
Mwaka 2015,
Jumla ya miradi 64 yenye thamani ya Tshs. Billioni 18,497,953,314 itaweza
kufikiwa Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Mwanza. Katika miradi hiyo, Miradi 15 yenye
thamani Tsh. Bilioni 10,167,443,654 itawekewa mawe ya msingi, miradi 21 yenye
thamani ya Tsh. Bilioni 1,353,151,574 itazinduliwa,
na miradi 28 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 6,977,358,086 itafunguliwa.
Miradi yote
imegharamiwa na serikali kuu Tsh. Bilioni 5,296,616,637. Halmashauri Tsh. Bilioni
2,109,308,123. Nguvu za wananchi Tsh. Bilioni 2,680,133,700 pamoja na wahisani mbalimbali
ambao wamechangia Ths. Bilioni 8,411,854,854. Miradi hii ipo katika sekta za
elimu, afya, barabara, maji, utawala bora, vijana, wajasiriamali, biashara,
kilimo na ufugaji.
Je nini Ujumbe wa Mwaka huu.?.. Mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Kama mnavyofahamu ujumbe wa mwaka huu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
unasema “Tumia haki yako ya
kidemokrasia: jiandikishe na kupiga kura katika uchaguzi wa 2015”. Ujumbe huu ni muafaka
kabisa kwa wakati huu na hasa ikifahamika kuwa tarehe 25 Oktoba, 2015
kutakuwepo na upigaji wa kura ili kuchagua viongozi ambao ni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani. Niwapongeze wale wote waliotumia haki yao ya
kikatiba na kisheria ya kujiandikisha na kupewa kitambulisho cha mpiga kura.
Kujitokeza kwenu kwa wingi mumewezesha mkoa wa Mwanza kuvuka lengo la
uandikishaji kwa asilimia 103 ambapo
jumla ya watu 1,442,391 waliweza
kuandikishwa. Ombi langu kwenu, ni kuvitunza vitambulisho mlivyopewa na siku
ikifika, nendeni kwenye vituo mlivyojiandikisha
ili kupiga kura. Mkoa umejipanga
kuhakikisha amani na utulivu vinatawala kipindi chote cha uchaguzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa mkoa hasiti kutia msisitizo wa ujumbe wa kudumu.....
Pamoja na ujumbe mkuu wa Mbio za Mwenge wa uhuru 2015, upo ujumbe wa kudumu ambao unahimiza wananchi kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa
UKIMWI, Malaria, Rushwa na Dawa za kulevya. Takwimu za mkoa zinaonesha kuwa
maambukizi ya UKIMWI yanazidi kupungua kutoka wagonjwa 979,035 mwaka
2009 hadi kufikia wagonjwa
367,545 mwaka 2014 ambapo kiwango cha maambukizi katika Mkoa ni asilimia 4.2 kwa mwaka 2014.
Mkuu wa Mkoa wa mkoa analiona janga la dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI.
Ombi langu kwa watanzania mnaonisikiliza na hasa wanaotumia dawa
za kufubaza virusi vya UKIMWI wasiache kuzitumia. Wakiacha kwa sababu yo
yote ile wanavipa vijidudu nafasi kujiimarisha na hivyo kuhatarisha maisha
yao. Tuendelee kuwasaidia
wenzetu walioathirika na kuwahudumia badala ya kuwanyanyapaa na
kuwatenga. Na, muhimu zaidi tuwasaidie watoto yatima na wazee ambao
wameachwa bila msaada wowote.
Vipi suala la Rushwa?
Mwaka huu, katika Mbio za Mwenge wa Uhuru naomba nikumbushe
wajibu wa kila mmoja kupambana na
rushwa, kwa kauli mbiu isemayo “kata mnyonyoro wa rushwa: chagua
kiongozi Mzalendo’. Ujumbe huu unakwenda
sambamba na juhudi za serikali za kupambana na rushwa nchini. Tunafahamu
kuwa rushwa ni adui wa haki na kikwazo kikubwa cha maendeleo ya jamii na
taifa. Nchi ikiwa imegubikwa na vitendo vya rushwa itakosa maendeleo
stahiki na watu watadhulumiwa haki zao. Kwa mfano, kwa kipindi cha
miaka mitatu, yaani kati ya 2010 hadi 2013, zaidi ya shilingi bilioni 28 zimeokolewa ambazo zingeweza kunufaisha
watu wachache wanaoendeleza vitendo vya rushwa. Naomba wananchi waendelee kutoa taarifa zitakazosaidia
kuwatambua na kuwakamata watoaji na wapokeaji rushwa.
Mkuu wa mkoa analiona suala la dawa za kulenya kama kikwazo cha maendelea je! anasema nini?
Tatizo la biashara na matumzi ya dawa za kulevya limeendelea kuwa
moja ya changamoto kubwa zinazolikabili taifa letu. Serikali imeendelea kufanya
jitihada kubwa kupambana na changamoto hiyo. Ugumu wa kazi hiyo unaletwa
na ukweli kwamba watu wanaohusika ni wengi na wanazidi kuongezeka kila kukicha
kwa tamaa ya kupata utajiri wa haraka.
Serikali haitachoka kufanya kila tuwezalo kupambana na uhalifu huu
mpaka ushindi upatikane, ikiwa ni pamoja na kutumia vikundi na taasisi
mbalimbali za uelimishaji wa mabadiliko ya tabia. Wakibadili mbinu nasi
tutabadili maarifa ya uchunguzi na utambuzi mpaka tuwapate. Kwa mfano, kuanzia
Januari hadi Septemba, mwaka huu (2015) watu
2000 (wafanya biashara na watumiaji wa dawa za kulevya) wamekamatwa.
Mashamba kadhaa ya bangi yameteketezwa, na aina mbalimbali ya dawa za kulevya
ikiwa ni pamoja na kilo 681 za
dawa hatari ya heroine, zimekamatwa na watuhumiwa wamefikishwa kwe Mkondo wa sheria. Nawaomba sana ndugu zangu na wananchi
wenzangu mshirikiane na vyombo vya dola katika kupambana na usafirishaji,
uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya.
Baada
ya kutoa salamu hizi nachukua nafasi hii kuwaribisheni Mkoani Mwanza na
najisikie mko nyumbani,
NAWATAKIA KILA LA HERI! ASANTENI KWA
KUNISIKILIZA.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
![]() |
| ASKARI JESHI KWENYE SIKU YA MASHUJAA JIJI MWANZA, HAPA WAKILIPUA RISASI HEWANI KUWAKUMBUKA MASHUJAA WALIOJITOLEA KWA NCHI YAO KATIKA VITA YA PILI YA DUNIA 1939-1945. |
Serikali
Mkoani Mwanza Imekeme tabia ya watu wanaohubiri mambo ya ukabila katika karne
ya sasa wakati mkoa huo ukiwa kwenye maadhimisho ya siku ya mashujaa
yaliyofanyika kwenye mviringo wa makutano ya barabara ya Nyerere, Kenyatta na
makongoro jijini Mwanza.
Akihutubia
Mamia ya wananchi hao, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magessa Mulongo, amesema
ameshangazwa na tabia ya baadhi ya wanasiasa kuhubiri habari ya ukabila kwenye
karne ya sasa hasa kipindi hiki tunacho elekea kwenye uchaguzi mkuu.
![]() |
| MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKITOA HOTUBA FUPI. |
”Nimeshangazwa
na ndugu zetu wa Chadema, juzi wamekuja hapa eti wamekuja kuwaambia wanamwanza,
kuwa Magufuli sio msukuma” alisema Muolongo na kuhoji yaani kweli hiyo ndio
meseji mtu aliyo kuja nayo? Amakweli duniani hapa kuna watu wana akili isiyo
nzuri alisisitiza Mulongo, na kuuliza hiyo kwa watu wa Mwanza inamaana gani? “
Unapokuja na gari la udini unataka kuwaambia nini, na kusema, Ezekiel Wenje,
alichaguliwa na wanamwanza lakini sio msukuma yeye ni Mshashi wa Mara lakini
pia Highness alichaguliwa na kuongoza Ilemela lakini yeye ni Mchaga wa
Kilimanjaro. Nilazima wakati mwingine na nyie wananchi muwe mnapima watu kwa
hoja zao, sio mtu anakuja hapa mkutano mzima yeye ni kutukana tuu na kusema
mambo ya hovyo mwanzo hadi mwisho.
![]() |
| BASE KAMANDA CANAL KIVAMBA AKIPOKEA SIME TAYARI KWA KUWEKA KWENYA MNARA WA MASHUJAA. |
Katika
hatua nyingine, amekemea tabia ya baadhi ya vijana wanaopita mitaani mara baada yakumaliza mikutano ya siasa na
kuanza kubugudhi watu wenye biashara zao, ”Umemaliza kusikiliza mkutano wa
siasa nenda nyumbani kwako kimya kimya” tabia
yakupita mitaani na kuanza kuwakera watu wengine wenye biashara zao sio kitendo
kinacho vumilika hata kidogo na niwaombe tu vijana wenzagu, kwamba kwa atakaye
thubutu kufanya hivyo tena sinto mvumilia” kwa mara ya kwanza niliwazuia askari
kuwachukulia hatua lakini niseme, kwa atakaye kiuka utaratibu huo sinto muonea
haya wala aibu eti kwakuwa tu kuchukua hatua utalalamikiwa, haiwezekani mtu
yeye avunje sheria halafu aangaliwe na hakuna mtu aliye juu ya sheria aliongeza
Mulongo.
Hata
hivyo ameviagiza vyombo vya ulizi na usalama kuhakikisha vinasimamia kikamilifu
ulinzi na usalama na kuhakikisha kila mchakato unapita salama katika kipindi
hiki na maisha mengine yanaendelea kama kawaida.
Awali
kabla ya kutoa maonyo hayo, Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza juu ya uzalendo wa
mtu mmoja mmoja na umuhimu wa kutunza amani” Ndugu zangu yamkini kama tungempa
nafasi mzee wetu Sadalla aeleze kile walichokutana nacho miaka hiyo hangetamani
kirudie tena, lakini hata wenyewe mmeshuhudia hiki walichokuwa wakifanya askari
wetu hapa na hii ilikuwa ni maonesho tu ,sitaki kusema mengi tuitunze amani
kwakuwa hakuna mbadala wa amani, badala ya Amani ni Vita.
![]() |
| MZEE IBRAHIMU SADALA ASKARI MSTAAFU WA KAR AKIFANYA MAHOJIANO NA AFISA HABARI WA MWANZA. |
Naye
kwa upande wake Mzee Ibrahimu Saddala aliyepigana vita vya pili vya Dunia(KAR)
mwenye umri wa miaka 90 kwa hivi sasa, alisema kila anapokumbuka hali
ilivyokuwa hatamani kusikia habari ya vita huku akiwataka watanzania kuilinda
amani kama mboni ya jicho. ”Mimi niliingia jeshi wakati ule nikiwa na miaka
kumi na tisa na ndio kwanza nilikuwa nimemaliza shule, tukaja
tukachukuliwa na kwenda kujiunga jeshi
tukaenda hadi Bama wakati huo tukiongozwa na wazungu” anasema Mzee Saddala na
kuongeza kuwa “pamoja na kwamba vita ile iliniwezesha kupata pesa yakununua
nyumba kwa shilingi miasaba (700) hapa Mwanza lakini kitu ambacho sitaki
kukumbuka ni hali ilivyo kuwa pamoja na umri wangu huu”.
Mzee
Saddala mwenye umri wa miaka tisini kwa sasa, ni miongoni mwa watu
wachache waliosalia kati ya walipigana vita kuu ya pili ya Dunia kati ya
Mwaka 1939-1945 na kwa sasa anaishi jijini Mwanza lakini pia ni mwenye nguvu na
kuweza kutembea yeye mwenyewe kwa kutumia fimbo ndogo aina ya mkongojo inayo
msaidia.
Imeandaliwa na Afisa
habari Mwanza zaidi na picha isome kupitia
![]() |
| ASKARI JESHI WAKITOA HESHMA ZAO WAKATI WA MAADHIMISHO HAYO YALIYOFANYIKA LEO. |
![]() |
| HAPA ASKARI WA GWARIDE WAKIPOKEA MAELEKEZO KUTOKA KWA MMOJA YA VIONGOZI WAO NAMNA YAKUKABIDHI ZANA HIZO KWA VIONGOZI WATAKAO WEKA KUMBU KUMBU. |
![]() |
| HAPA VIONGOZI WA DINI WAKIA WANASIKILIZA KWA MAKINI MAZOEZI YA GWARIDE LA MASHUJAA. |
![]() |
| MPIGANAJI WA KAR KITENGO CHA SIGNO, IBRAHIMU SADALLA, AKIWA AMEMALIZA KUWEKA SHOKA KATIKA MNARA WA KUWAENZI MASHUJAA WA VITA YA PILI YA DUNIA. |
![]() |
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
![]() |
| MKUU WA MKOA WA MWANZA MWENYE SHATI JEUSI, MAGESA MULONGO, AKIONESHWA KITU NA MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA WAKATI WA MOJA YA ZIARA YAKE MKOANI HUMO. |
Wazee
katika Mkoa wa Mwanza, wamemshauri Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kuanza kulima zao la
alizeti ili kuuwezesha mkoa huo kuinuka kuichumi kutokana na hali mbaya ya
mazao kama pamba kupoteza umaarufu kwenye sekta ya uchumi wa mkoa huo.
Wakizungumza
katika kikao kilicho wakutanisha wazee hao na mkuu wa mkoa hivi karibuni katika
hoteli ya Mwanza, wazee hao walisema kutokana na hali isiyoridhisha kwa zao
kama pamba ambalo ndilo lilikuwa zao kuu la uchumi wa mkoa huu kupoteza
umaarufu ni vema sasa jamii ikabadilika na kuhamishia nguvu zake kwenye zao la
alizeti.
Akizungumza
kwa niaba ya wazee wenzake, aliyekuwa Mkuu wa kwanza wa wilaya ya Ilemela, Jared John Gachocha,
alisema, haoni sababu ya mkoa wa Mwanza kushindwa kutilia mkazo zao la alizeti
ambalo gharama zake za uzalishaji ni nafuu zaidi ukilinganisha na pamba.” Mh.
Mkuu wa mkoa mimi nadhani kipindi hiki tushughulike kufa na kupona kwenye
alizeti, sioni kwa nini wenzetu wa Singida watupite katika hili, zao la alizeti
ni rahisi mno kulilima halina usumbufu halihitaji mbolea nyingi, haliitaji maji
mengi na maandalizi yake kwakweli ni rahisi lakini pia faida yake ni kubwa”
alisema na kuongeza kuwa “hali hiyo itasaidia mkoa kujitosheleza kwa mafuta
lakini pia kuweza kuuza kwa watu wengine.
Mbali
ya zao la alizeti wazee hao pia walimuasa mkuu huyo wa mkoa, kuelekeza nguvu
zaidi kwenye masuala ya ufugaji, wakisema kuwa tupo nyuma sana katika masuala
ya mifugo huku wakitolea mfano nchi ya Kenya kwamba Ng’ombe anauwezo wakutoa
maziwa lita hadi 20 tofauti na Tanzania, hali inayo walazimu wazee hao kumuasa
mkuu wa mkoa kuwataka wafugaji kuachana na ufugaji wa kizamani na badala yake
watafute mitamba itakayoweza kuleta tija kwa wafugaji. “Ni ukweli usiopingika
kwamba hapa kwetu kumpata ng’ombe anayeweza kukupatia lita 10 za maziwa ni
nadra sana hivyo tuwashawishi wakulima waweze kutafuta mitamba ambayo itakuwa
niya kisasa ili waweze kukuza uchumi wao lakini uchumi wa mkoa kwa ujumla.
Awali
akizungumza mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kabla yakuanza kupokea maoni ya wazee hao,
alisema mkoa wa Mwanza wenye watu Milioni mbili na laki saba na mia saba sabini
na mbili mia tano na tisa, huku mkoa ukiwa unachangia Trioni 4.9 katika pato la
taifa, Watu wake milioni moja uchumi wao
unategemea zaidi katika Sekta ya Uvuvi, “Wazee wangu nimewaiteni tusaidiane
kuongoza mkoa huu, mkoa huu ni mkubwa na changamoto tulizo nazo ni nyingi”
alisema Mulongo na kuongeza kuwa, “kati ya watu mil. 2.7, watu Milioni moja wanategemea
ziwa kuanzia mvuvi ziwani hadi mparuaji na mchuuzi mdogo mdogo wa mtaani sasa
hali ya ziwa letu kwa upande wa uzalishaji sio salama sana, tuna kwendaje
lazima tujipange kisawasawa alisema Mulongo.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza toka amewasili mkoa wa Mwanza, ameweka utaratibu wakukutana
na watu wa makundi mbali mbali mkoani hapa ili kufahamu changamoto ambazo zipo
ili waweze kuzitatua kwa kushirikiana kwa pamoja, makundi ambayo tayari
yamekutana na mkuu huyo wa mkoa hadi sasa ni pamoja na, Wananchi wa kawaida kwa
kuzungumza nao kwenye mikutano ya hadhara na kusikiliza kero zao na kuzipatia
ufumbuzi, Wafanya biashara wadogo ambao alifanikisha kufanyika kwa uchaguzi
wao, wakuu wa taasisi za umma zilizoko mkoani hapa, viongozi wa dini, viongozi
wa kisiasa na asasi zisizo za kiraiya.
Mkoa
wa Mwanza ni mkoa wa pili kwa uchangiaji wa pato la taifa kwa asilimia 9.15% ukitanguliwa na Mkoa wa Dar Es Salaam, huku
wastani wa pato la mwananchi wa kawaida ikiwa ni
Tshs. 910,824 kwa mwaka.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
![]() |
| Picha ya pamoja ya kumbukumbu na viongozi wa ngazi za juu. |
![]() |
| Picha ya pamoja ya kumbukumbu na wakuu wa Ulinzi na usalama. |
![]() |
| Picha ya pamoja ya kumbukumbu na wanafamilia wa Bw. George. |
![]() |
| Picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wenzake. |
![]() |
| Picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi Tume ya Sheria. |
![]() |
| Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyekuwa akisubiri kuapishwa, George Mcheche, akizungumza jambo na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, wakati wa hafl hiyo. |
![]() |
| Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo. |
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kiongozi wa Albino asema hukumu ikishindikana Duniani, itatolewa Mbinguni.
Watu 15 Wanashikiliwa na Polisi, nayo pikipiki iliyotekeleza mpango yabambwa na polisi, uchunguzi unaendelea.
![]() |
| WANANCHI WA NDAMI TARAFA YA MWAMASHIMBA WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA MWANZA. |
![]() |
| WAANDISHI WA HABARI SHEILA SEZI NA GRACE CHILONGOLA WAKIWA NA MAMA PENDO EMMANUEL, AMBAYE HIVI SASA ANA MAJONZI BAADA YA MTOTO WAKE KUTWALIWA NA WATU HAO. |
![]() |
| ALFREDY KAPOLE MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WA MWANZA AKIONGEA KATIKA KIKAO HICHO |
![]() |
| SUNGU SUNGU KWENYE KIKAO. |
![]() |
| MWENYEKITI WA CHAWATA MKOA WA MWANZA NA MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WA MWANZA WALIPOKUWA WAKIONGEA NA MAMA YAKE NA PENDO EMMENUEL. |
MKUU WA MKOA.
![]() |
| MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO. |
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa
Mulongo, alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kijijini hapo na kuwahusisha wananchi wakijiji hicho pamoja
na uongozi wa Wilaya na Mkoa huku akitaka kujua hatua iliyofikiwa na wana nchi
hao katika kuwabaini walifanya unyama huo.
Mtoto Pendo alitekwa na watu wasiojulikana mnamo usiku
wa tarehe 27.12.2014 majira ya saa nne usiku akiwa amelala na wazazi wake huko
Nyumbani kwao na kisha watekaji kutoweka naye na kwenda kusiko julikana hadi
sasa, huku taarifa za Polisi zikionesha jumla ya watu kumi na watano (15),
wakiendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Akihutubia wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza, alisema ni tukio la kusikitisha kwani toka mwaka 2007 hakuna tukio
la namna hiyo lililo wahi kutokea katika Wilaya hiyo na tukio la mwisho lililotokea
lilimkumba mwananchi wa Wilaya hiyo aliyekuwa amesafiri kwenda Mkoani Shinyanga
kwa shughuli zake.
Amesema kiburi walicho nacho watekaji hakiwezi
kuwa nje ya mipaka ya kijiji hicho cha Ndami bali mpango mzima unajulikana kwa
wenyeji na ndio maana ilikuwa rahisi kufanya unyama huo “Kiburi cha watekaji
kimo humu humu haiwezekani mtu kutoka mbali aje atekeleze tukio hapa kijijini
bila yakuwa na wenyeji lazima kuna mtu au watu walioshirikiana na wahalifu hao”,
alisema Mulongo na kuongeza “ kwa mazingira ya Nyumba ya kina Pendo ilipo kule
hakuna sehemu yakutokea na kama mliona pikipiki inaranda randa mchana,.. iweje
mshindwe kuitilia shaka? Hapana, hii haikubaliki!
mimi nimekuja kuwaambia nataka Pendo apatikane na sio vinginevyo, nawapa siku
tano ijumaa nitarudi hapa mniambie Pendo yuko wapi! Alisema mkuu huyo wa Mkoa
akionesha kusononeshwa na tukio hilo.
“Mbona mifugo inapo ibwa inapatikana”? Aliwahoji viongozi
wa sungu sungu na kusema haiingii akilini kusema wakati wa tukio la utekaji
sungu sungu wote walikuwa wamekwenda kula chakula na ndipo kadhia hiyo
ilipotokea, mkuu wa mkoa, alihoji kufatia kauli iliyotolewa na kiongozi wa
sungu sungu kuwa wakati wa tukio askari wote wa sungu sungu walikuwa wamekwenda
kula majira ya saa tatu na tukio kutokea saa nne.
MWENYEKITI
WA ALBINO MWANZA.
Awali akielezea kusikitishwa kwake na tukio hilo,
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa Ngozi mkoani hapa Alfred Kapole,
alisema inasikitisha kuona wanadamu wakiwauwa binadamu wenzao kama vile wanyama
bila hata woga na vyombo vya maamuzi vikishindwa kutoa hukumu kwa wakati huku
akielekeza lawama zake kwa mahakama na Mkemia Mkuu. “Mh. Mkuu wa mkoa
inasikitisha kuona miongoni mwa kesi 72 zilizokuwa mahakamani, ni kesi 3 tu
ndizo zilizokwisha kutolewa hukumu” alisema Kapole, na kuongeza ingekuwa ni
kesi ya Wabunge wameshindana kwenye masuala ya uchaguzi ingekuwa imekwisha
hukumiwa lakini kwakuwa ni mlemavu wa ngozi,
basi kupuuzia kumekuwa kwingi
mno. Alisema kapole.
Akinukuu maneno kutoka katika kitabu cha Biblia,
Kapole alisema hata kama hukumu zitashindwa kutolewa na wanadamu hapa Duniani, naamini
Mungu wa Mbinguni kuna siku haki itatendeka kwa kuwa “Kitabu cha Mika 3.3-7 kinaeleza
juu ya hukumu watakayo ipata watu walao nyama za watu bila woga. Kesi
zinaendeshwa Polisi wanajitaihidi sana lakini mkemia watendaji wa ofisi ya
mkemia mkuu wanatuhujumu kwa kuita nywele zetu albino ni za Midoli, aling’aka Kapole wakati
akielezea kusikitishwa na ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali pindi inapo pelekewa
Nywele.
Mwenyekiti Kapole pia aliomba kwa yeyote aliye na Mtoto
huyo kumrejesha na kama wamemdhuru basi warejeshe hata mwili wake ili matanga
yaweze kufanyika, akatumia fursa hiyo kumomba Rais wale wote waliohukumiwa
kunyongwa wanyongwe ili kuepusha kuendelea kula chakula cha serikali bure.
RC ITIKADI
KATIKA KAZI.
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa aliwataka wanachi
kuweka mbali itikadi zao za namna yoyote na kufanya kila linalowezekana ili kufanikisha zoezi zima la kuwasaka walio
husika na utekaji wa mtoto Pendo Emmanuel, ambao unasimuliwa kuleta siamanzi
kubwa ndani ya jamii ya wana Kwimba na watanzania lakini pia kuchafua taswira ya nchi mbele ya
mataifa mengine ya Dunia . Huku akiwaonya watu wa haki za binadamu kuacha kupaza
sauti za kuwatetea wahalifu. Tanzania inatajwa kuwa kinara cha ukatili huo
tangu mauwaji hayo yalipo zuka mwanzoni mwa miaka ya 2006/2007.
TAKWIMU ZA
KIMATAIFA.
Kwa Mujibu wa takwimu za kimataifa zinaonesha ni
asilimia 2% tu ya watu ambao huzaliwa na ulemavu wa ngozi ndio hufikia na
kusherekea miaka 40 ya kuzaliwa kwao, huku pia takwimu zikionesha katika nchi
za Afrika mtu mmoja (1) kati ya elfu mbili (2000) huzaliwa wakiwa na ulemavu wa
ngozi wakati katika marekani ni mtu mmoja kati ya elfu kumi na saba ndio huishi
na ulemavu wa ngozi.
Mauaji ya Albino katika Tanzania yanaonekana
kushamiri katika Mikoa ya kanda ya ziwa, ambapo imani za kishirikina zikitajwa
kuwa chanzo kikubwa cha mauwaji ya hayo lakini pia yale yalio wahusu vikongwe yanayo
husishwa na masuala ya kujipatia utajiri
wa haraka suala ambalo sio la kweli, ambapo takwimu zinaonesha kuwa mauwaji
yalianza siku nyingi japo kuripotiwa
katika mamlaka za serikali na vyombo vya habari ilianza mwaka 2006/2007.
Hivi sasa zipo asasi za kiraia zinazo jihusisha na
harakati za kupinga mauwaji hayo ikiwapo asasi ya Under The Same Sun ya Nchini Canada
na kwa Tanzania imeshakuwa na tawi toka mwaka 2008.
KAMANDA WA
POLISI.
Awali akitoa taarifa ya uchunguzi wa tukio hilo
kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mulowola alisema tayari watu 15
wanashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani humo kwa mahojiano zaidi akiwapo baba
mzazi wa Pendo, lakini pia jeshi hilo limefanikiwa kuipata piki piki
iliyotumika kufanya unyama huo. “Hivi sasa tunawashikilia watu wapatao kumi na
watano na wanaendelea kuhojiwa na Polisi” alisema Mlowola na kuongeza kuwa huo
sio mwisho kwa kuwa jinai haina mwisho hata miaka ishirini tukio hili
litaendelea kuchunguzwa”, na kusema hata kama yeye atahamishwa au kustaafu
kijana atakayekuja ataendelea na kesi hiyo, hivyo wananchi waendelee kutoa
ushirikiano kwa kile wanacho kifahamu, alisema Mlowola na kusema tayari Jeshi
hilo mkoani hapa limetangaza kuto Milioni tatu 3 kwa atakayefanikisha
kupatikana kwa mtoto Pendo.
Mtoto Pendo alikuwa ni miongoni mwa alibino 74
waliopo katika wilaya ya Kwimba na alikuwa namba 9 katika suala la kupatiwa
ulizi.
Imeandaliwa
na Afisa habari Mwanza- Atley Kuni.
Subscribe to:
Posts (Atom)