Wakulima wa mkoa wa kanda ya ziwa kwa ujumla wameshukiwa na neema ya pekee kufuatia jitihada za serikali ya awamu tano kuwaanzishia Benki yao katika kanda hii, ambayo itakuwa na makao yake makuu katika Mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John
Mongella, akizungumza wakati wa makabidhiano wa jengo litakalo tumika kwa ajili
yashughuli za kibenki kwa kanda ya ziwa lakini pia kama tawi kwa mkoani wa
Mwanza, amesema Sekta ya kilimo ambayo hubeba zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa
Tanzania kwa sasa imepatiwa mkombozi.
Jengo hapa likifunguliwa tayari kukaguliwa na kukabidhiwa kwa wahusika. |
“Kama mnavyo fahamu, sekta hii ina
mnyororo mrefu, wapo wanao lima, wengine wanachakata mazao lakini wapo pia
wanao safirisha mazao kwendanje ya nchi na wengine wanao leta mzao ndani ya
nchi, alisema Mongella na kuongeza, “tunavyozungumzia asilimia 80% ni hawa
wote, tunataka mwisho wa siku kilimo kimlipe mtu na kuendesha maisha yake”
alisema Mkuu wa Mkoa.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi
mtendaji wa Benki ya Kilimo Nchini, Francis Assenga, yeye amesema shabaha yakufunguliwa
kwa benki hiyo nikutaka kumkomboa mkulima kutoka katika kilimo cha kujikimu na kuingia
katika kilimo cha kibiashara, “Tukasema tuangalie sehemu ambayo inamatokeo ya
haraka lakini eneo ambalo linachangia kwa kiwango kikubwa katika pato la taifa,
tukasema Mwanza ni mahali sahihi”. Alisema Assenga.
Amesema kanda ya ziwa inayo miradi
mingi ya kilimo hasa wingi wa viwanda
ambavyo vitatumika, katika kusindika , kuchakata na kufanya kilimo cha biashara
ambapo mnyororo wa thamani ulivyo kwa kanda ya Mwanza.
Mkurugenzi huyo, amesifu pia
utayari wa Viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa kwa utayari
walio uonesha lakini pia kutafuta eneo ambalo Benki hiyo itakuwepo, “Kimsingi
tumefurahishwa sana na utayari wa Mkuu wetu wa Mkoa John Mongella, akisema
anatenda, sasa miongoni mwa kanda sita tunazo kwenda kuzianzisha Mwanza inakuwa
kanda ya kwanza kwani fedha tayari zimetolewa na serikali kwa ajili ya
uanzishwaji wa Benki hii” alisema Assenga.
Katikati ya Makabidhiano hayo,
Mhandisi wa Majengo katika Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Yohana Mashausi, akasema wao
wapo tayari kwaajili yakuwakabidhi Benki ya wakulima Jengo ambalo lilikuwa
likitumiwa na Mamlaka ya mapato (TRA) hapo kabla.
Mwandishi wa habari kutoka Magazeti ya serikali Nashonny Kennedy, akitaka uafanuzi wa jambo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Wakulima nchini, wakati wa hafla ya Makabidhiano ya Benki hiyo. |
Post A Comment: