Mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw John Mongella (kulia) akipokea cheti cha kutambua jitihada zake katika kufanikisha Rock City Marathon kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi. Mbio hizo zilizofanyika Septemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
 
Na Mwandishi wetu,
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw John Mongella amesema mkoa wake umejipanga kutumia michezo kama nyenzo muhimu katika kutangaza fursa na vivutio vya utalii vilivyopo mkoani humo.
Bw Mongella alitoa kauli hiyo jijini Mwanza jana wakati akipokea cheti cha kutambua jitihada zake katika kufanikisha Rock City Marathon zilizofanyika kwa mafanikio makubwa Septemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi.
“Mafanikio yaliyoonekana kupitia Rock City Maratahon mwaka huu ndio yameongeza chachu ya kuhakikisha kwamba timu yetu ya mpira wa miguu ya Pamba nayo inapanda na kuingia ligi kuu ili kuungana na timu za Mbao na Toto Afrika zilizopo ligi kuu,’’ alisema Mongella ambae alishiriki mbio za km 5 kwenye Rock City Marathon.
Alitoa wito kwa waandaaji wa mbio hizo Kampuni ya Capital Plus International (CPI) kuhakikisha Rock City Marathon mwakani zinahusisha mbio za km 42 (Full marathon) kutoka km 21 za sasa kutokana na mwitikio mkubwa kutoka kwa wadau wa mchezo huo ndani na nje ya nchi.
“Niseme tuu, tukiitumia hii michezo vizuri ndio njia pekee yakujitangaza na kutangaza fursa mbali mbali zilizopo mkoani kwetu…hivyo naomba sana wadau mbalimbali mkoani Mwanza na mikoa mingine kuunga mkono jitihada za waandaaji wa michezo mbalimbali hapa nchini,’’ aliongeza.
Kwa upande wake Bw Ngowi aliwashukuru viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakiwemo viongozi wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) ,huku akiongeza kuwa  wao kama waandaaji wa mbio hizo wamefurahishwa sana na ushirikiano mkubwa waliopata kutoka wa viongozi hao.
“Kubwa zaidi pia ni kuwashukuru sana wadhamini wa mbio hizi kwa kuendelea kutuunga mkono kwenye maandalizi haya yaani kampuni za Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust, Benki ya NMB,  New Mwanza Hotel, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR Solutions, kampuni ya Fabec, Tiper, Puma Energies, Clouds Fm, Jembe Fm, Barmedas Tv na EF Out Door,’’ alitaja.


Axact

Post A Comment: