MWAKILISHI WA KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA, MWALIMU HAMISI MAULIDI AKIFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO, WAANDAAJI WA FILAMU NCHINI. |
PICHANI NI BIBI JOYCE FISOO, KATIBU MTENDAJI WA BODI YA FILAMU NCHINI, AKIWASILISHA MADA WAKATI WA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZOWANATSNIA YA FILAMU MKOANI MWANZA. |
RAIS WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA BW. SAIMON MWAKIFWAMBA(KULIA), AKIFAFANUA JAMBO KWA MAAFISA WA WA HIFADHI YA JAMII WA PPF KANDA YA ZIWA. |
Na Lorietha Laurence-Mwanza
Mkoa wa Mwanza waweka
mkakati wa kukuza na kuendeleza sekta ya
filamu kwa kuhakikisha inazalisha bidhaa bora zenye kufuata taaluma na weledi
wa tasnia hiyo ili kufikia soko la kimataifa.
Hayo yameelezwa leo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Hamis Maulidi ,wakati wa ufunguzi wa warsha ya
wadau wa tasnia ya filamu yenye lengo la kuwajengea uwezo wanatsnia hao.
Akizungumza katika Ufunguzi
huo Maulidi ameeleza kuwa filamu ni
kielelezo muhimu cha utamaduni wa watu na jamii husika hivyo ni budi kuulinda ,
kuenzi pamoja na kuendeleza suala zima la filamu, huku akiahidi Mkoa wake kusimamia ipasavyo ili kuleta mabadiliko
lakini pia kuwawezesha wana tasnia hao kujiajiri.
“Ni wajibu wa jamii husika
kuhakikisha kuwa tasnia ya filamu inalindwa na kuenziwa ili kuleta kuendelea
kulinda na kuhifadhi utamaduni,silka na
mila zetu”
Maulidi amesema, tasnia ya
filamu imeleta ajira rasmi kwa wananchi wetu ambao wamekuwa wakijihusisha na
utengezaji, uaandaaji pamoja na uigizaji
wa filamu na kuziuza kwa wadau mbalimbali jambo ambalo limekuwa likiwaingizia
kipato cha kujikimu kimaisha.
Awali akimkaribisa
kufungua semina hiyo ya siku tatu Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bibi. Joyce Fissoo, amewataka wanatasnia hao
kuwa watulivu na kujifunza zaidi kupitia warsha hiyo ili kuzalisha filamu zenye
kuzingatia taaluma na weledi wakati wote wa maandalizi hadi uzalishaji wa
Filamu hapa nchini .
Warsha ya kuwajengea uwezo
wanatsnia wa filamu Mkoani Mwanza imejikita katika kuhakikisha kuwa, tasnia ya
filamu nchini inakuwa na kufikia viwango vya kimataifa ili kuwezesha ushindani
katika masoko ya kimataifa.
Post A Comment: