Serikali Mkoani
Mwanza imeamuru shule 11 za msingi na
moja ya Sekondari, zilizokuwa zimefungwa Wilayani Ukerewe kutokana na ukosefu
wa vyoo zifunguliwe na wanafunzi warejee kwenye masomo wakati wa hatua za dharura zinachukuliwa.
Hatua hiyo imefikiwa
mapema hivi leo wakati wa kikao cha pamoja baina ya uongozi wa Mkoa na Wilaya kukaa na kuangalia hatua zipi
zifuate mara baada ya hapo jana Mkurugenzi wa Wilaya ya Ukerewe Bw. Frank
Bahati, kukieleza kikao cha Ushauri cha mkoa wa Mwanza kuwa, wamezifunga shule
hizo kutokana na kukosa vyoo.
Aidha pia halmashauri ya Wilaya imeelekezwa kuwatumia
watendaji wa kata na Vijiji, kusimamia
zoezi hilo na kuwahamasisha wananchi waweze kushiriki katika kufikia adhma hiyo
ya ujenzi wa vyoo ili wanafunzi hao waondokane na adha inayo wakabili.
Kwa upande wa
Uongozi wa halmashauri ya Wilaya ya
Ukerewe, umeahidi kutenga kiasi cha Mil.80 kutoka katika makusanyo ya ndani kwaajili yakufanikisha zoezi hilo la
dharura, huku Wananchi wakitakiwa kushiriki katika uchimbaji wa mashimo.
Shule za msingi zilizokuwa
zimefungwa kutokana na kukosa vyoo ni pamoja na Muhuzya na Murutanga za kata ya
Bukindo, Busangu na Mugu za kata ya Namilembe, Buzegwe na Kilongo za kata ya
Kagunguli, zingine ni Mukasika na Muhandi za kata ya Murutunguru, Mubule
iliyopo kata ya Nyamanga na Chankamba iliyopo kata ya Igalla.
Wakati kwa upande wa
Sekondari ni shule moja tu ya Lugongo iliyopo kata ya Murutunguru.
Imetolewa
Atley J. Kuni
AFISA HABARI RS MWANA
Mwanza
Post A Comment: