Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amezindua Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekouture inayoundwa na wajumbe wapatao 15, huku akiibebesha jukumu lakuhakikisha hospitali hiyo inachana na mfumo wa ukusanyaji mapato wa kawaida na badala yake watumie mfumo wa kieletroniki
Mkuu
huyo wa mkoa amesema pamoja na Hospitali hiyo kuongeza mapato yake lakini bado kiasi
hicho kinacho kusanywa hakingani na hadhi ya hospitali hiyo, kwani kwa mujibu
wa takwimu za makadirio ya watu huo unakadiriwa kuwa na watu wapatao Mil.3.5
kwa sasa.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, akimkabidhi mmoja ya wajumbe wa Bodi Ndungu Christopher Mwita Gachuma Miongozo ya namna yakuendesha Hospitali za Rufaa |
“Ni
kweli kuwa tumeongeza makusanyo yetu kutoka Mil. 500 hadi kufikia Bil. 1 kwa
mwaka, lakini kwa idadi yetu ya watu tulipaswa kufikia Bil.2.5 hadi Bil. 3 kwa
mwaka”, alisema Mongella na kuendelea kuitaka bodi hiyo isimame imara kuhakikisha
malengo hayo ya makusanyo yanafikiwa.
Mongella
pia katika hotuba yake, amesema mpango uliopo kwa sasa nikujenga jengo la
Ghorofa ili kuimarisha na kuongeza shughuli zautoaji huduma za afya katika
hosptali hiyo inayotegemewa hata na baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa, huku
akiahidi kuomba kubadilishiwa matumizi kiasi cha fedha Mil. 460 zilizokuwa zimetolewa
na hazina kuelekezwa katika ujenzi wa jengo la Ghorofa tatu linalo tarajia
kujengwa katika Hospitali hiyo.
Awali
Mganga mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Leonard Subi, akimkaribisha mkuu wa mkoa kuzindua bodi hiyo, alisema
mahitaji halisi ya watumishi wa Idara afya katika mkoa huo ni watumishi 7,582
lakini watumishi waliokuwepo kabla ya zoezi la uhakiki ilikuwa ni watumishi 3,552
sawa na asilimia 48 ya mahitaji yote ya watumishi, aidha Subi amesema kuwa mkoa
wa Mwanza kwa hivi sasa hauna tishio lolote lile la Magonjwa ya Mlipuko.
Akitoa
taarifa ya Hospitali hiyo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Onesmo
Rwakyendera, amesema hospitali hiyo kwa sasa imeendelea kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano
ambayo imelenga kuwahudumia watanzania wote katika kuboresha maisha yao ikiwa
ni pamoja na huduma za afya.
Wajumbe wa Bodi na baadhi ya Waalikwa wakimsikiliza kwa Makini Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe, John Mongella, wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekouture |
“Kupitia
juhudi hizo hospitali imeweza kuwa na mafanikio mbalimbali kama vile uwepo wa
dawa muhimu kwa asilimia 80” amesema Rwakyendera, aidha amesema
katika kufikia mafanikio chanya kwa kipindi cha miaka mitatu Hospitali iliwahudumia
Jumla ya wagonjwa wa nje wapatao 512,548.
Picha ya Pamoja kati ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella na Wajumbe wapya wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekouture. |
Wajumbe watakao simamia
hospitali hiyo iliyo anza mwaka 1994 ni pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa Mwanza
Dkt. Leonard Subi, Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dkt. Onesmo Rwakyendera, Bwana
Christopher Mwita Gachuma, Bibi. Asia Kapande na Shekh Hassan Kabeke, wengine
ni Bwana Joseph Kahungwa, Bibi Elicia Yinza, Bwana Kaviti Mushi, Dr. Richard Mbwambo,
Bibi, Victoria Ndalahwa, Mhe. Serapian
Matiku, Dr. Agnes Mwita, Bwana Charles Misango, Bwana . H.V Shah, Mganga Mkuu
Halmashauri Ya, Manispaa Ilemela
Post A Comment: