WAKALA WA VIPIMO (WMA) 
SIKU YA VIPIMO DUNIANI
VIPIMO VINAVYOTUMIKA KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI

(MEASUREMENT FOR TRANSPORT)

Mei, 20 kila mwaka nchi nyingi duniani husherehekea siku ya  vipimo duniani. Mwaka huu kauli  mbiu ( theme) ya maadhimisho ni vipimo katika sekta ya usafirishaji (measurement for transport).


Hamis Abdul, wakituo cha mafuta cha Puma cha Jijini Mwanza kama alivyokutwa akipima Mafuta hii leo siku ya Vipimo Duniani.
Shirika la Vipimo Duniani (OIML) hutoa mapendekezo  na miongozo ya kimataifa katika nchi mbalimbali mojawapo ikiwa ni Tanzania kupitia Wakala wa Vipimo kuhusiana na matumizi ya vipimo sahihi katika  biashara, na sasa tuko kwenye mpango wa kuingia katika  sekta za afya, usalama na mazingira, nia na lengo likiwa ni kuleta usahihi katika dhana nzima ya  vipimo  kwa dunia nzima.

Hivyo, katika Sekta ya Usafirishaji kwa mfano ambayo ndio theme ya Siku ya Vipimo Duniani; Mizani itumikayo  barabarani, au kwenye viwanja vya ndege au katika vituo vya mabasi  ni lazima ihakikiwe na kuthibitishwa  na Wakala wa Vipimo  ili kupata  usahihi wakati wa kupima uzito wa magari au mizigo mbalimbali. Kama Mizani hiyo haitathibitiwa basi usalama wa wasafiri pamoja na mizigo yao utakuwa mashakani. Vile vile, Vyombo vingi vya usafiri ili viweze kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine huhitaji nguvu yaani mafuta au gesi. Mafuta au gesi hutolewa kwa vipimo sahihi ili kuhakikisha chombo kinafika sehemu sahihi kulingana na kiasi cha mafuta/gesi iliyochukuliwa kituoni. Vipimo ambavyo vyombo vya usafiri (Ndege, Mabasi, Magari) huchukuwa mafuta/gesi ni Vituo vya mafuta (Dispensing pumps) na Flow meters.
Gari ilikipita katika Mizani, ili kuhakikiwa usahihi wa vipimo vyake.

 
Kupitia Maadhimisho haya tutaeleza majukumu ya Wakala wa Vipimo kwa ujumla na kubainisha umuhimu wa usahihi wa Vipimo nchini. Vile vile tutajikita zaidi katika sekta ya usafirishaji ambayo ndio kauli mbiu ya maadhimisho.

JUKUMU LA WAKALA WA VIPIMO TANZANIA

·        Wakala wa Vipimo inalo jukumu la kumlinda mlaji na umma kwa ujumla kupitia uhakiki na uthibiti wa vipimo vinavyotumika katika biashara na huduma nyingine, kuhakikisha kuwa vipimo hivyo ni sahihi na vinatumika kwa usahihi kulingana na Sheria ya Vipimo Sura 340 mapitio ya mwaka 2002 na maboresho yake ya mwaka 2016 pamoja na kanuni zake.

·        Hivyo, Jukumu kuu la Wakala wa Vipimo ni kumlinda mlaji kupitia matumizi ya vipimo sahihi.

       KAZI ZA WAKALA

·        Kuilinda jamii kutokana  na madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya vipimo katika Sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira.


·        Kudhibiti ufungashaji wa bidhaa (Net quantity & lebelling)

·        Kuwa kiungo cha Taifa letu na taasisi za Kikanda na Kimataifa katika masuala ya vipimo (legal Metrology)

·        Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya vipimo kwa wadau

·        Kuhakikisha vifaa vyote vitumikavyo nchini  vinakuwa  na ulinganisho sahihi na ule wa Kimataifa.

  
Mmoja ya Meneja  wa wakala wa Vipimo, Bibi Fotunatha Makoye akifanya uhakiki
wa vipimo katika kituo cha mafuta
 
KAZI ZA WAKALA WA VIPIMO KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI

 Kuhakiki mizani mikubwa inayotumika barabarani (Weighbridges/Axle Weighers). Weighbridges ni mizani zinazofungwa barabarani kwa ajili ya kupima uzito wa magari makubwa. Mizani hizi hutumika kupimia magari ya kubebea mizigo/mabasi. Hufungwa barabarani kwa lengo la kupima uzito wa magari ili yasiharibu miundombinu ya barabara yasisababishe ajali.
 
Kuhakiki mizani  aina ya Platform, Counter Scales & Spring   Balances Mizani hii mara nyingi hutumika Airport, bandarini, Posta na katika vituo vya mabasi  kwa ajili ya kupimia uzito wa mizigo inayosafirishwa katika sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Vile vile Mizani hii hutumika Posta kwa ajili ya kupimia vifurushi mbalimbali vinavyosafirishwa toka eneo moja kwenda eneo   jingine. Vifurushi hivyo hutozwa gharama za kusafirishia kulingana na uzito wake. Mizani  zote hizi  yote upima uzito wa mizigo mbalimbali.

 
Kwa kutumia vipimo hivi, wamiliki wa mizigo au wa vyombo vya usafiri hutozwa nauli za mizigo hiyo kulingana na uzito wa mizigo husika. Pia, kutumia mizani katika vituo vya usafirishaji hupunguza uwezekano wa kuzidisha uzito na kuepusha ajali za barabarani zinazotokana na kuzidisha uzito.

Katika vituo vya mafuta na bandarini kuna Dispensing pumps na Flow meters, hivi ni Vipimo ambavyo vyombo vya usafiri kama Ndege, Mabasi, Magari huchukuwa mafuta/gesi. Mafuta au gesi hutolewa kwa vipimo sahihi ili kuhakikisha chombo kinafika sehemu sahihi kulingana na kiasi cha mafuta/gesi iliyochukuliwa kituoni.

FAIDA ZA KUTUMIA VIPIMO KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI

A: Kuna faida mbalimbali zinazopatikana kwa kutumia vipimo vya uzito   katika sekta ya usafirishaji, baadhi ya faida hizo ni pamoja na:-

i)     Kulinda miundombinu ya barabara kupitia mizani (Weighbridges) zinazofungwa barabarani.

ii)   Husaidia kupunguza ajali barabarani kwa magari yanayobeba mizigo.

iii)  Husaidia wateja kutozwa ada ya mizigo/vifurushi vinavyosafirishwa kulingana na uzito wa mzigo.

B: Vipimo vya kupimia mafuta na gesi (Volume Measurements)

 Vyombo vingi vya usafiri ili viweze kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine huhitaji nguvu yaani mafuta au gesi. Mafuta au gesi hutolewa kwa vipimo sahihi ili kuhakikisha chombo kinafika sehemu sahihi kulingana na kiasi cha mafuta/gesi iliyochukuliwa kituoni. Vipimo ambavyo vyombo vya usafiri (Ndege, Mabasi, Magari) huchukuwa mafuta/gesi ni Vituo vya mafuta (Dispensing pumps) na Flow meters.

Jaribu kufikiri kwa mfano ndege inaondoka ikiwa imepakia abiria pamoja na mizigo na imejaza mafuta yakiwa pungufu yaani haijazingatia matumizi sahihi ya vipimo ni dhahiri itakapokuwa angani itaishiwa mafuta, hivyo usalama wake na wa abiria utakuwa mashakani. Hivyo, Vipimo vina umuhimu mkubwa sana katika sekta ya usafiri.

C. Kipimo cha kupima mwendokasi (Speed Measuring Device)

Speed measuring device ni kifaa kinachotumika na Traffic kupima speed (Mwendo kasi) wa magari yanayo tembea barabarani. Kifaa hicho hupima na kurekodi mwendokasi wa gari linalokimbia barabarani. Faida ya kutumia vifaa hivi vya kudhibiti mwendokasi ni dhahiri, mojawapo ikiwa ni kudhibiti ajali barabarani.

D. Vipimo vingine katika sekta ya usafiri ambavyo Wakala wa Vipimo ipo kwenye mchakato wa kuvihakiki ni taximeter pamoja na tyre pressure gauge.

CHANGAMOTO



     i.        Upungufu wa watumishi na vitendea kazi katika kufanya shughuli za vipimo.

    ii.        Uelewa mdogo wa sheria za vipimo kwa jamii ya wafanyabiashara na wananchi.

  iii.        Kuwepo kwa mizani mingi batili na isiyokuwa na ubora sahihi inayoingizwa nchini kinyemela na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu. Changamoto hii inasababishwa na uhaba wa mizani nchini na hata ile michache inayopatikana/ kuagizwa toka nje ni ghali  kwa wananchi wa kawaida kumudu.

  iv.        Uhaba wa Vipimo  (hasa mizani) halali nchini.
  
Maafisa Vipimo katika Picha ya pamoja, hii leo siku ya Vipimo Duniani.
Hivyo tukiwa tunaadhimisha Siku ya Vipimo Duniani ambayo mwaka huu imejikita katika Sekta ya Usafirishaji, ni vyema tukatambua kuwa umuhimu wa  Vipimo sahihi uko katika kila sekta ya maisha yetu hapa nchini. Baadhi ya sekta hizo ni kama Biashara, Afya, Usalama, Mazingira na nyingine nyingi. Ni wajibu wetu pia kutambua kuwa Wakala wa Vipimo ndio iliyopewa majukumu haya muhimu ya kumlinda mwananchi katika harakati zake za kujenga uchumi.

 

 

 
Axact

Post A Comment: