.
Jumla
ya Waendesha Pikipiki 1167 wamepatiwa mafunzo ya kuendesha Pikipiki na kupatiwa
Leseni daraja “A” katika kipindi cha Januari – Agosti, 2013.
Boda boda hii kama ilivyonaswa ikiwa imekiuka sharia usalama barabarani. |
“Ni
kweli tuna mpango wa kuwafanya Vijana waweze kujiajiri wenyewe ili kuweza
kujiongezea kipato lakini pia mpango huu unasaidia kupunguza ajali za
barabarani” aliniambia Sajini Kitia wa jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kitengo
cha usalama barabarani tuliyezungumza naye kwa njia ya simu.
Imeelezwa
pia katika mpango huo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Chuo
cha Ufundi VETA, huwapatia mafunzo na badaye jeshi la polisi kwa ushirikiano na
mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), huwakatia Leseni za daraja “A” na kuwasajili
kwenye maeneo wanayofanyia kazi pamoja na kufatilia mwenendo wao wa kazi za
kila siku.
Ni
kwamba kiwango cha ajali kimepungua kwa asilimia 17.8% ikilinganishwa na
kipindi kama hicho cha Januari – Augusti, 2012, ambapo kulitokea ajali 118,
ikilinganishwa na ajali 97 kwa kipindi hicho hicho cha Januari hadi Agost 2013.
Mpango
huo unafuatia agizo lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuwaelekeza Viongozi wa Polisi Mkoani hapa kubaini mbinu
zitakazosaidia kupunguza ajali za barabarani kwa asilimia ikilinganishwa na
mwaka uliopita 50%.
Hivi
sasa Mkoani humo hali imekuwa tofauti ilinganishwa na siku za nyuma wakati
biashara hiyo yakundesha pikipiki ikonekana kama biashara haramu na iliyokuwa
ikipoteza nguvu kazi ya taifa kutokana na ajali zilizokuwa zikitokea.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na Blog hii ya kuninews.blogspot, umeonsha kwa bado kuna baaadhi ya waendesha boda boda wasiotii sheria kwa kupakiza abiria zaidi ya mmoja huku wakiwa hawana kofia ngumu za kujikinga na ajali.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na Blog hii ya kuninews.blogspot, umeonsha kwa bado kuna baaadhi ya waendesha boda boda wasiotii sheria kwa kupakiza abiria zaidi ya mmoja huku wakiwa hawana kofia ngumu za kujikinga na ajali.
Post A Comment: