Articles by "Usalama"
Showing posts with label Usalama. Show all posts
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
MKUU WA MKOA WA MWANZA MWENYE SHATI JEUSI, MAGESA MULONGO, AKIONESHWA KITU NA MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA WAKATI WA MOJA YA ZIARA YAKE MKOANI HUMO.
Wazee katika Mkoa wa Mwanza, wamemshauri Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kuanza kulima zao la alizeti ili kuuwezesha mkoa huo kuinuka kuichumi kutokana na hali mbaya ya mazao kama pamba kupoteza umaarufu kwenye sekta ya uchumi wa mkoa huo.
Wakizungumza katika kikao kilicho wakutanisha wazee hao na mkuu wa mkoa hivi karibuni katika hoteli ya Mwanza, wazee hao walisema kutokana na hali isiyoridhisha kwa zao kama pamba ambalo ndilo lilikuwa zao kuu la uchumi wa mkoa huu kupoteza umaarufu ni vema sasa jamii ikabadilika na kuhamishia nguvu zake kwenye zao la alizeti.
Akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake, aliyekuwa Mkuu wa kwanza  wa wilaya ya Ilemela, Jared John Gachocha, alisema, haoni sababu ya mkoa wa Mwanza kushindwa kutilia mkazo zao la alizeti ambalo gharama zake za uzalishaji ni nafuu zaidi ukilinganisha na pamba.” Mh. Mkuu wa mkoa mimi nadhani kipindi hiki tushughulike kufa na kupona kwenye alizeti, sioni kwa nini wenzetu wa Singida watupite katika hili, zao la alizeti ni rahisi mno kulilima halina usumbufu halihitaji mbolea nyingi, haliitaji maji mengi na maandalizi yake kwakweli ni rahisi lakini pia faida yake ni kubwa” alisema na kuongeza kuwa “hali hiyo itasaidia mkoa kujitosheleza kwa mafuta lakini pia kuweza kuuza kwa watu wengine.
Mbali ya zao la alizeti wazee hao pia walimuasa mkuu huyo wa mkoa, kuelekeza nguvu zaidi kwenye masuala ya ufugaji, wakisema kuwa tupo nyuma sana katika masuala ya mifugo huku wakitolea mfano nchi ya Kenya kwamba Ng’ombe anauwezo wakutoa maziwa lita hadi 20 tofauti na Tanzania, hali inayo walazimu wazee hao kumuasa mkuu wa mkoa kuwataka wafugaji kuachana na ufugaji wa kizamani na badala yake watafute mitamba itakayoweza kuleta tija kwa wafugaji. “Ni ukweli usiopingika kwamba hapa kwetu kumpata ng’ombe anayeweza kukupatia lita 10 za maziwa ni nadra sana hivyo tuwashawishi wakulima waweze kutafuta mitamba ambayo itakuwa niya kisasa ili waweze kukuza uchumi wao lakini uchumi wa mkoa kwa ujumla.
Awali akizungumza mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kabla yakuanza kupokea maoni ya wazee hao, alisema mkoa wa Mwanza wenye watu Milioni mbili na laki saba na mia saba sabini na mbili mia tano na tisa, huku mkoa ukiwa unachangia Trioni 4.9 katika pato la taifa, Watu wake  milioni moja uchumi wao unategemea zaidi katika Sekta ya Uvuvi, “Wazee wangu nimewaiteni tusaidiane kuongoza mkoa huu, mkoa huu ni mkubwa na changamoto tulizo nazo ni nyingi” alisema Mulongo na kuongeza kuwa, “kati ya watu mil. 2.7, watu Milioni moja wanategemea ziwa kuanzia mvuvi ziwani hadi mparuaji na mchuuzi mdogo mdogo wa mtaani sasa hali ya ziwa letu kwa upande wa uzalishaji sio salama sana, tuna kwendaje lazima tujipange kisawasawa alisema Mulongo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza toka amewasili mkoa wa Mwanza, ameweka utaratibu wakukutana na watu wa makundi mbali mbali mkoani hapa ili kufahamu changamoto ambazo zipo ili waweze kuzitatua kwa kushirikiana kwa pamoja, makundi ambayo tayari yamekutana na mkuu huyo wa mkoa hadi sasa ni pamoja na, Wananchi wa kawaida kwa kuzungumza nao kwenye mikutano ya hadhara na kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi, Wafanya biashara wadogo ambao alifanikisha kufanyika kwa uchaguzi wao, wakuu wa taasisi za umma zilizoko mkoani hapa, viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa na asasi zisizo za kiraiya.
Mkoa wa Mwanza ni mkoa wa pili kwa uchangiaji wa pato la taifa kwa asilimia 9.15%  ukitanguliwa na Mkoa wa Dar Es Salaam, huku wastani wa pato la mwananchi wa kawaida ikiwa ni Tshs. 910,824  kwa mwaka.
 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kiongozi wa Albino asema hukumu ikishindikana Duniani, itatolewa Mbinguni.
Watu 15 Wanashikiliwa na Polisi, nayo pikipiki iliyotekeleza mpango yabambwa na polisi, uchunguzi unaendelea.

WANANCHI WA NDAMI TARAFA YA MWAMASHIMBA WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA MWANZA.
WAANDISHI WA HABARI SHEILA SEZI NA GRACE CHILONGOLA WAKIWA NA MAMA PENDO EMMANUEL, AMBAYE HIVI SASA ANA MAJONZI BAADA YA MTOTO WAKE KUTWALIWA NA WATU HAO.
Serikali mkoani Mwanza imesema hakuna kulala hadi mtoto Pendo Emmanuel  miaka 4(Albino) apatikane, kufatia tukio la kutekwa na watu wasio julikana toka tarehe 27, Desemba, 2014 katika kijiji cha Ndami, Tarafa ya Mwamashimba Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza na kisha kutoweka naye kwenda kusiko julikana hadi sasa.  
ALFREDY KAPOLE MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WA MWANZA AKIONGEA KATIKA KIKAO HICHO



SUNGU SUNGU KWENYE KIKAO.
  
MWENYEKITI WA CHAWATA MKOA WA MWANZA NA MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WA MWANZA WALIPOKUWA WAKIONGEA NA MAMA YAKE NA PENDO EMMENUEL.

 MKUU WA MKOA.

MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo na kuwahusisha wananchi wakijiji hicho pamoja na uongozi wa Wilaya na Mkoa huku akitaka kujua hatua iliyofikiwa na wana nchi hao katika kuwabaini walifanya unyama huo.
Mtoto Pendo alitekwa na watu wasiojulikana mnamo usiku wa tarehe 27.12.2014 majira ya saa nne usiku akiwa amelala na wazazi wake huko Nyumbani kwao na kisha watekaji kutoweka naye na kwenda kusiko julikana hadi sasa, huku taarifa za Polisi zikionesha jumla ya watu kumi na watano (15), wakiendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Akihutubia wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, alisema ni tukio la kusikitisha kwani toka mwaka 2007 hakuna tukio la namna hiyo lililo wahi kutokea katika Wilaya hiyo na tukio la mwisho lililotokea lilimkumba mwananchi wa Wilaya hiyo aliyekuwa amesafiri kwenda Mkoani Shinyanga kwa shughuli zake.
Amesema kiburi walicho nacho watekaji hakiwezi kuwa nje ya mipaka ya kijiji hicho cha Ndami bali mpango mzima unajulikana kwa wenyeji na ndio maana ilikuwa rahisi kufanya unyama huo “Kiburi cha watekaji kimo humu humu haiwezekani mtu kutoka mbali aje atekeleze tukio hapa kijijini bila yakuwa na wenyeji lazima kuna mtu au watu walioshirikiana na wahalifu hao”, alisema Mulongo na kuongeza “ kwa mazingira ya Nyumba ya kina Pendo ilipo kule hakuna sehemu yakutokea na kama mliona pikipiki inaranda randa mchana,.. iweje mshindwe kuitilia shaka? Hapana,  hii haikubaliki! mimi nimekuja kuwaambia nataka Pendo apatikane na sio vinginevyo, nawapa siku tano ijumaa nitarudi hapa mniambie Pendo yuko wapi! Alisema mkuu huyo wa Mkoa akionesha kusononeshwa na tukio hilo.
“Mbona mifugo inapo ibwa inapatikana”? Aliwahoji viongozi wa sungu sungu na kusema haiingii akilini kusema wakati wa tukio la utekaji sungu sungu wote walikuwa wamekwenda kula chakula na ndipo kadhia hiyo ilipotokea, mkuu wa mkoa, alihoji kufatia kauli iliyotolewa na kiongozi wa sungu sungu kuwa wakati wa tukio askari wote wa sungu sungu walikuwa wamekwenda kula majira ya saa tatu na tukio kutokea saa nne.
MWENYEKITI WA ALBINO MWANZA.
Awali akielezea kusikitishwa kwake na tukio hilo, Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa Ngozi mkoani hapa Alfred Kapole, alisema inasikitisha kuona wanadamu wakiwauwa binadamu wenzao kama vile wanyama bila hata woga na vyombo vya maamuzi vikishindwa kutoa hukumu kwa wakati huku akielekeza lawama zake kwa mahakama na Mkemia Mkuu. “Mh. Mkuu wa mkoa inasikitisha kuona miongoni mwa kesi 72 zilizokuwa mahakamani, ni kesi 3 tu ndizo zilizokwisha kutolewa hukumu” alisema Kapole, na kuongeza ingekuwa ni kesi ya Wabunge wameshindana kwenye masuala ya uchaguzi ingekuwa imekwisha hukumiwa lakini kwakuwa ni mlemavu wa ngozi,   basi kupuuzia kumekuwa kwingi mno. Alisema kapole.
Akinukuu maneno kutoka katika kitabu cha Biblia, Kapole alisema hata kama hukumu zitashindwa kutolewa na wanadamu hapa Duniani, naamini Mungu wa Mbinguni kuna siku haki itatendeka kwa kuwa “Kitabu cha Mika 3.3-7 kinaeleza juu ya hukumu watakayo ipata watu walao nyama za watu bila woga. Kesi zinaendeshwa Polisi wanajitaihidi sana lakini mkemia watendaji wa ofisi ya mkemia mkuu wanatuhujumu kwa kuita nywele zetu albino ni za Midoli, aling’aka Kapole wakati akielezea kusikitishwa na ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali pindi inapo pelekewa Nywele.
Mwenyekiti Kapole pia aliomba kwa yeyote aliye na Mtoto huyo kumrejesha na kama wamemdhuru basi warejeshe hata mwili wake ili matanga yaweze kufanyika, akatumia fursa hiyo kumomba Rais wale wote waliohukumiwa kunyongwa wanyongwe ili kuepusha kuendelea kula chakula cha serikali bure.
RC ITIKADI KATIKA KAZI.
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa aliwataka wanachi kuweka mbali itikadi zao za namna yoyote na kufanya kila linalowezekana  ili kufanikisha zoezi zima la kuwasaka walio husika na utekaji wa mtoto Pendo Emmanuel, ambao unasimuliwa kuleta siamanzi kubwa ndani ya jamii ya wana Kwimba na watanzania  lakini pia kuchafua taswira ya nchi mbele ya mataifa mengine ya Dunia . Huku akiwaonya watu wa haki za binadamu kuacha kupaza sauti za kuwatetea wahalifu. Tanzania inatajwa kuwa kinara cha ukatili huo tangu mauwaji hayo yalipo zuka mwanzoni mwa miaka ya 2006/2007.
TAKWIMU ZA KIMATAIFA.
Kwa Mujibu wa takwimu za kimataifa zinaonesha ni asilimia 2% tu ya watu ambao huzaliwa na ulemavu wa ngozi ndio hufikia na kusherekea miaka 40 ya kuzaliwa kwao, huku pia takwimu zikionesha katika nchi za Afrika mtu mmoja (1) kati ya elfu mbili (2000) huzaliwa wakiwa na ulemavu wa ngozi wakati katika marekani ni mtu mmoja kati ya elfu kumi na saba ndio huishi na ulemavu wa ngozi.
Mauaji ya Albino katika Tanzania yanaonekana kushamiri katika Mikoa ya kanda ya ziwa, ambapo imani za kishirikina zikitajwa kuwa chanzo kikubwa cha mauwaji ya hayo lakini pia yale yalio wahusu vikongwe yanayo husishwa na  masuala ya kujipatia utajiri wa haraka suala ambalo sio la kweli, ambapo takwimu zinaonesha kuwa mauwaji yalianza  siku nyingi japo kuripotiwa katika mamlaka za serikali na vyombo vya habari ilianza  mwaka 2006/2007.
Hivi sasa zipo asasi za kiraia zinazo jihusisha na harakati za kupinga mauwaji hayo ikiwapo asasi ya Under The Same Sun ya Nchini Canada na kwa Tanzania imeshakuwa na tawi toka mwaka 2008.
KAMANDA WA POLISI.
Awali akitoa taarifa ya uchunguzi wa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mulowola alisema tayari watu 15 wanashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani humo kwa mahojiano zaidi akiwapo baba mzazi wa Pendo, lakini pia jeshi hilo limefanikiwa kuipata piki piki iliyotumika kufanya unyama huo. “Hivi sasa tunawashikilia watu wapatao kumi na watano na wanaendelea kuhojiwa na Polisi” alisema Mlowola na kuongeza kuwa huo sio mwisho kwa kuwa jinai haina mwisho hata miaka ishirini tukio hili litaendelea kuchunguzwa”, na kusema hata kama yeye atahamishwa au kustaafu kijana atakayekuja ataendelea na kesi hiyo, hivyo wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa kile wanacho kifahamu, alisema Mlowola na kusema tayari Jeshi hilo mkoani hapa limetangaza kuto Milioni tatu 3 kwa atakayefanikisha kupatikana kwa mtoto  Pendo.
Mtoto Pendo alikuwa ni miongoni mwa alibino 74 waliopo katika wilaya ya Kwimba na alikuwa namba 9 katika suala la kupatiwa ulizi.
Imeandaliwa na Afisa habari Mwanza- Atley Kuni.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Wakutana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Fatilia matukio katika Picha zote Na, Afisa habari RS Mwanza.
MKUU WA MKOA WA MWANZA AKIPOKEA ZAWADI YA NGAO KUTOKA KWA KIONGOZI WA MSAFARA HUO BREGEDIA GENERAL KAPINGA WAKATI WA ZIARA HIYO.
MAKAMANDA WA CHUO CHA UKAMANDA WAKIWA WANAFATILIA KWA KARIBU MAELEZO YA MKUU WA MKOA WA MWANZA HAYUPO PICHANI  WAKATI WA ZIARA HIYO.

MAKAMANDA KUTOKA NCHI ZA RWANDA NA ZAMBIA WAKIWA MAKINI NA MAELEZO YA MHE. MKUU WA MKOA WA MWANZA.

MAKAMANDA KUTOKA TANZANIA WAKINUKUU BAADHI YA MAELEZO YA MHE. MKUU WA MKOA.


HAPA MAKAMANDA WAKIFATILIA JAMBO.


HIVI NDIVYO UKUMBI ULIVYOKUWA UNAFANANA.

KIONGOZI WA MSAFARA HUO BREGEDIA KAPINGA AKITOA MAELEZO MAFUPI KWA MKUU WA MKOA KABLA YA KUANZA MAONGEZI YAO NA MAKAMANDA HAO.


MOJA YA MAKAMANDA ALIYETAKA KUJUA KUHUSU JITIHADA ZA MKOA KATIKA KUMKOMBOA MKULIMA KWA KUWA KILIMO NI UTI WA MGONGO WA TAIFA LA TANZANIA.



HAPA MAKAMANDA WALILAZIMIKA KUPIGA PICHA YA PAMOJA KAMA SEHEMU YA KUMBU KUMBU YA UGENI HUO KUTOKA (CSC- ARUSHA)

NI PICHA YA PAMOJA.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 


RAIS WA KENYA UHURU MWIGAE KINYATTA
Mauaji ya Mpeketoni yemesababisha vifo vya watu zaidi ya hamsini
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa mauaji yaliyofanywa katika mji wa Mpeketoni, Pwani ya Kenya hayakufanywa na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab.
Kauli ya Rais Kenyatta inakuja kupitia kwa televisheni siku moja baada ya kundi hilo kukiri kufanya mauaji yaliyotokea Mpeketoni Jumapili usiku.
Kenyatta emesema kuwa kuna ushahidi kuonyesha kuwa shambulizi hilo lilipangwa vyema na kwamba wanasiasa walihusika nao.
Al Shabaab lilikiri katika taarifa kwa vyombo vya habari kuwa ndilo lilifanya mauaji hayo Jumatatu jioni.
Alisema kuwa ujasusi ulitolewa kuwa mashambulizi hayo yangefanyika lakini hawakuchukua hatua zozote kuzuia mashambulizi hayo.
Rais amesema kuwa maafisa waliohusika tayari wameachishwa kazi na kwamba watashitakiwa. Amesema kuwa kwa sasa wanachunguza wanasiasa waliohusika na mauaji hayo ili sharia iweze kuchukua mkondo wake.
Mauaji zaidi yalifanyika usiku wa kuamkia leo licha ya taarifa ya Al Shabaab kusema kuwa washambuliaji walioshambulia Mpeketo walikuwa wamerejea salama nchini Somalia.
Uharibifu mkubwa ulishuhudiwa katika mji huo huku washambuliaji wakichoma hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari waliyoyatumia kwa usafiri wao.
Kenyatta amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanaochochea uhasama miongoni mwa jamii.
 
Hata hivyo Kenya katika siku za hivi karibuni imekuwa katika hali tete ya mashambulio ya kigaidi likiwepo shambulio kubwa lililowahi kutokea katika Jengo kubwa la Westgate la Jiji Nairobi na kusababisha vifo vya watu kadhaa na mamia wengi kujeruhiwa.
 
Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema kipigo wanachokipata nchi hiyo ni kutokana na kupeleka wanajeshi wake Nchini Somalia kwa ajili ya kukabiliana na makundi ya kigaidi
 
 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
MWANDISHI NGULI NA MWENYE KUFANYA VIPINDI VYA UCHUNGUZI NA  KISIASA NCHINI TANZANIA , KATIKA UKURASA WAKE WA FACE BOOK LEO, NIMEKUTANA NA HABARI HII,  SWALI AMBALO HATA MIMI MWENYEWE NIMEKUWA NAJIULIZA SIKU ZOTE SIPATI JIBU HEBU TUSAIDIANE MAJIBU WAUNGWANA MTAKAOPATA FURSA YAKUISOMA STORI HII KATIKA   www.kuninews.blogspot.com




HAWA NDIO BOKO HARAM WANAODAIWA KUWA NA VIFAA VYA KISASA VYA KIVITA.
 
 
HUYU NI RAIS BARAK OBAMA, RAIS WA NCHI KUBWA KIUCHUMI DUNIANI:  AMERIKA.

 
Na Dotto Bulendu.
 
Binafsi napata utata sana na haya makundi yanayotekeleza mauaji katika nchi mbalimbali hususani barani Afrika,kumekuwa na makundi ya waasi na haya tumepata kuyashuhudia katika nchi za Uganda, DRC Congo, Afrika ya kati, Mali, Misri, Kenya pia makundi yanayotajwa kuwa ni ya kigaidi kama AlQaeda,AlShabaab na Boko Haram Ntarahamwe nk.!..Makundi haya yamekuwa yanafanya mashambulizi ya kushtukiza na kusababisha mauaji ya watu wasio na hatia Duniani ,na hata dunia sasa inahangaika na kundi la Boko Haram,ambalo wakati dunia ikih...angaika kuwanasua mabinti waliotekwa, jana kundi hili limetajwa kutekeleza mauaji kwa kulipua bomu tena huko kaskazini mwa Nigeria na kusababisha vifo vya watu takribani zaidi ya 120, vikundi vya waasi na kigaidi barani Afrika vimekuwa vinatumia silaha za kisasa kupambana na majeshi ya serikali barani Afrika pamoja na kufanya mashambulizi....utata wangu upo katika maeneo haya.
1.Makundi haya ya silaha nzito,nani anawauzia?silaha hizo zinawafikiaje? tunajua silaha zote nzito zinatengenezwa na nchi zilizoendelea na siyo barani Afrika, je makundi haya yanazinunuaje hizi silaha? tunajua biashara za silaha ni biashara yenye faida sana, nahisi nchi za ulaya,marekani na asia zinazotegeneza silaha zinajua fika undani wa makundi haya.
2.Makundi haya yanaajiri vijana wengi, yanakaa mafichoni, yanapata wapi pesa za kununua silaha na malipo pamoja na posho kwa wapiganaji wake? yamehifadhi wapi fedha zao? nani anakwenda benki kuweka na kutoa pesa za makundi haya? naamini zipo taasisi za fedha ambazo zinaujua kwa undani uasili wa makundi haya!!tunajua pesa chafu zinaendesha baadhi ya mataifa.
3.Nani anafadhiri makundi haya? kwa nini makundi haya yanachomoza kwenye nchi zenye utajiri wa mafuta? na wakati makundi haya yakiendelea na uharibifu huu utajiri uliopo katika nchi hizo unaendea kuporwa na wanaopora hawaguswi wala kushambuliwa na makundi haya!
Nani yupo nyuma ya makundi haya? natafakari na karibuni wanajamvi tufanye tafakuri tunduizi(critical thinking),juu ya makundi ya uasi na ugaidi barani Afrika,nani anayafadhiri?ufadhiri wao unapitia wapi? wanatuza wapi fedha zao? wanapitishia wapi silaha zao?..natafakari sana!.
 
Toa maoni yako hata bila kutaja jina nasi tutayachapisha
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
RAIS WA NIGERIA GOODLUCK JONATHAN .

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amezungumza wazi kwa mara ya kwanza kuhusu kutekwa kwa waschana takriban 200 wa shule kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Katika taarifa yake ya kwanza hadharani tangu wasichana 200 kutekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Waislamu wenye itikadi kali wa Boko Haram, Rais Goodluck Jonathan, amesema kuwa kila juhudi zinapaswa kufanywa kuwakomboa wasichana hao.
Tangazo la Rais lilitolewa kufuatia shinikizo zilizotolewa na familia, makundi ya wanawake na watu wengine ambao wameitaka Serikali kufanya bidii zaidi kuhakikisha kuwa wasichana hao wanakombolewa.
Rais alisema kuwa maafisa wa usalama wamekuwa wakitafuta kila mahali wakitumia ndege na helikopta lakini akakiri kuwa hawajafaulu kutambua walikofichwa wasichana hao.
Alisema kuwa Serikali yake imelazimika kuomba msaada katika kuwatafuta wasichana hao kutoka Serikali za Marekani, Uingereza na Uchina.
Jeshi la Nigeria limekuwa likipambana na kundi hilo la wapiganaji tangu mwaka 2009, lakini mashambulizi na milipuko ya mabomu yameendelea kusikika kila mahali bila kukoma.
Hivi majuzi kumekuwa na milipuko katika mji mkuu wa Abuja katika muda wa majuma matatu ambapo karibu watu 90 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Mnamo Jumatano Kongamo la Dunia juu ya Uchumi wa Afrika utafanyika mjini Abuja na swala la usalama limewatia maafisa wa usalama tumbo joto, ambapo imetangazwa kuwa siku hiyo shule zote na afisi za Serikali zitafungwa ili kuimarisha usalama eneo hilo la mkutano
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

SIKU IGP MANGU ALIPOKUWA AKILA KIAPO MBELE YA
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
 
Hatua ya kuhitaji usalama kwa kila binadamu ni kutokana na kuzungukwa na makundi mbalimbali ya waasi ambao kwa tafsri ya haraka tafiti zinawabainisha kama wasaliti wakuu katika maisha.

Madhara makubwa yanayosababishwa na waasi hao ama wahalifu kwa jina lingine ni kufanya mashambulizi ambayo huchangia hata idadi kubwa ya watu kupoteza maisha achilia mbali upotevu wa mali.

Kutokana na familia nyingi kukabiliwa na vikwazo vya kushambuliwa na matatizo mbalimbali na hata kupoteza ndugu na jamaa.

Ndani ya miaka 50 ya Uhuru kutokana mashambulizi hayo ya wahalifu sote tufarijiane kwa pamoja na tuendelee kudumisha usalama na amani katika maeneo yanayotuzunguka.

Hata hivyo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambayo iliundwa Desemba 15  mwaka 1961 baada ya Tanganyika kupata Uhuru ilikuwa na dhamira njema ya kuwahakikishia Watanzania usalama .

Kuanzishwa kwa wizara hiyo tafiti zinaoensha kuwa ililenga kuunda chombo ambacho kingesimamia masuala ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao katika mazingira ya nchi huru.

Ili kuiwezesha nchi yetu kuondokana na sera za kikoloni ambazo zilianzishwa kwa ajili ya kulinda maslahi ya wakoloni.

Majukumu ya wizara yalitekelezwa kwa kupitia jeshi la polisi na idara ya magereza wakati ambao utawala wa Kijerumani haukuanzisha jeshi rasmi la polisi badala yake walikuwa wakiwatumia watawala wa vijiji  wakiwemo Maakida na Majumbe katika kutekeleza majukumu ya kipolisi.

Kwa upande mwingine askari wa jeshi na vikundi vingine vya ulinzi ambao walijulikana kitaalam kama para–military groups vilitumika kudhibiti upinzani wa ndani pamoja na kulinda mipaka.

Mwaka 1916 Wajerumani walianzisha Jeshi la Polisi la kiraia kitaalam Civilian Police Force baada ya kuelekea kushindwa na majeshi ya Kiingereza katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia tangu mwaka 1910 kwa lengo la kulinda vitega uchumi, makazi yao na mipaka ya koloni la Tanganyika.

Kikosi hicho cha Polisi kilichokuwa na askari 31 chini ya Meja Davies kutoka Afrika ya Kusini, kilitekeleza majukumu ya kipolisi hadi mwaka
1919 Wajerumani waliposhindwa na Waingereza.

Wakati wa utawala wa Waingereza tafiti zinaeleza kwamba walianzisha taasisi mbalimbali ikiwemo Jeshi la Polisi lilojulikana kama Tanganyika Police Force and Prisons Service chini ya Sheria ya Jeshi la Polisi na Magereza ya mwaka 1919 yaani The Police Force and Prisons Ordinance Cap.40.

Agosti 25,1919 Serikali ya Kiingereza ilianzisha rasmi Jeshi la Polisi kupitia tangazo la gazeti la Serikali namba .1.Vol.I No. 21-2583 hatua ambayo ilisababisha makao makuu ya jeshi la polisi kuwa Lushoto eneo la Wilemstal mjini Tanga.

Hata hivyo Meja Davies aliteuliwa kuwa Kamishna wa kwanza wa Jeshi hilo na baadaye nafasi yake ilichukuliwa na Meja Brownie Esq aliyehamishwa kutoka
Kenya.

Tofauti na utawala wa Kijerumani, jeshi hilo lilipewa majukumu ya kipolisi, magereza, usalama wa taifa, kimahakama na ya kiutawala pale ambapo hapakuwa na maofisa tawala au wakuu wa wilaya.

Ingawa Jeshi la Polisi lilijitenga na shughuli za kijeshi bado lilikuwa na
jukumu la kulinda maslahi ya wakoloni wa Kiingereza.

Hali hii ilijionesha kwenye muundo wa Jeshi la Polisi ambapo nafasi za juu zilishikwa na wazungu,nafasi za kati zilishikwa na Waasia na vyeo vya chini vilibaki kwa wazawa.

Mwaka 1922 kulikuwa na wazungu 68 wenye vyeo kuanzia wakaguzi hadi makamishna ambapo wakaguzi 25 wenye asili ya Asia na Waafrika 748 wa vyeo vya chini.

Pamoja na kuongezeka kwa idadi ya Waafrika ndani ya jeshi la polisi,
hali ya kubaguliwa iliendelea huku tafiti zikitolea mfano mwaka 1930  jeshi hili lilikuwa na Wazungu 78 kwenye nafasi za juu, Waasia 67 kwenye vyeo vya kati na Waafrika 1719 kwenye nafasi za chini.

Mbali na kushika nafasi za chini katika jeshi hilo, Waafrika pia walibaguliwa kwa taratibu za kiutawala, makazi na stahili.

Wakati wa Utawala wa Kiingereza shughuli za kipolisi zilifanywa kwenye
maeneo ya miji na vijiji vilivyokuwa na idadi kubwa ya walowezi wa kizungu.

Katika maeneo haya vituo vya polisi vya muda yaani Detached Police Stations
vilianzishwa kwa ajili ya kulinda mashamba ya walowezi.

Katika kipindi cha Vita Kuu ya Pili ya Dunia  ambayo ilichukua hatamu tangu mwaka 1939 hadi 1945 utawala wa Kiingereza ulipanua wigo wa ajira ndani ya jeshi la polisi na kuongeza idadi ya Maofisa wa Kiafrika katika nafasi za kati na za juu.

Tafiti zinabainisha kuwa kufikia mwaka 1960, kulikuwa na Waafrika 28 kwenye ngazi za juu za Jeshi la Polisi.

Kwa upande wa Zanzibar jeshi la polisi lilianzishwa mwaka 1873 kwa ajili
ya kusimamia sheria za kupinga biashara ya utumwa.

Jeshi hili lilijumuisha askari wa Kiingereza na wa Sultani wa Zanzibar.

Mwaka 1877 Serikali ya Kiingereza ilimteua Kamanda wa Kikosi cha Maji, Lloyd Mathews, kuongoza askari 1300 wakiwemo Waafrika 300.

Mwaka 1907 wakati Zanzibar ikiwa chini ya uangalizi wa Waingereza kitaalam Protectorate, Sultani alilivunja jeshi la polisi baada ya askari wake kugoma kutokana na mishahara midogo na mazingira duni ya kazi na kuunda lingine ambalo lilijumuisha askari wa akiba kutoka Tanganyika.

Baada ya Tanganyika kupata uhuru wake Desemba 9, 1961 jukumu la Jeshi
la Polisi lilibadilika kutoka kusimamia maslahi ya kikoloni na kuwa jeshi la
kusimamia utekelezaji wa sheria ndani ya Tanganyika huru.

Kimsingi muundo na majukumu ya Jeshi la polisi yalibaki kama yalivyo igawa mabadiliko makubwa yaliyojitokeza wakati huo ni kuongezeka kwa Maofisa wa Kiafrika wenye vyeo vya juu ili kuchukua nafasi zilizokuwa zikishikiliwa na Wazungu.

MAKALA HII NIKWA MSAADA WA GAZETI LA MAJIRA. 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 
MHE. BERNAD MEMBE WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA TANZANIA.
Serikali ya Tanzania itafanya mazungumzo na Rwanda ili "kutatua tofauti za kisiasa kuhusu mgogoro katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti Alhamisi (tarehe 27 Machi).
 
Mazungumzo rasmi yanakusudiwa kuondoa kile Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Bernard Membe alichokiita "vita ya kimaandishi" kilichosukumwa na propaganda ya vyombo vya habari.
 
"Mazungumzo hayo rasmi yatakuwa ndiyo mwanzo," alisema Membe, akiongeza kwamba watarejesha imani kati ya nchi hizo mbili.Membe alikariri kwamba kwa wajibu wa Tanzania katika mgogoro huo uliopo nchini  DRC ni kwa ajili ya jitihada za kuleta amani tu chini ya umoja wa mataifa.  wajibu wa Tanzania katika mgogoro uliopo nchini DRC ni kwa ajili tu ya jitihada za kuleta amani tu chini ya Umoja wa Mataifa.
 
"Kwa mujibu wa ujumbe wetu ulioko huko Goma [mashariki mwa DRC], amani hatimaye inarejea katika eneo hilo na vijana wetu wataendelea kuwa kule kwa mwaka mmoja hadi amani itakaporejea kikamilifu," alisema Membe.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.


KITANZI TAYARI KWA KUNYONGA.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Tanzania imesema hadi kufikia Februari mwaka huu watanzania 177 wamefungwa katika magereza nchini China, huku miongoni mwao 15 wakiwa wamehukumiwa kunyongwa kutokana na makosa ya dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo, John Haule alisema watanzania hao bado hawajanyongwa kutokana na serikali ya China kuthamini ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na China na huenda wakabadilishiwa kifungo na kufungwa kifungo cha maisha jela badala ya Kunyongwa.

Haule amesema serikali ya Tanzania itahakikisha inadumisha ushirikiano na China kwa lengo la kupatikana kwa fursa za kiuchumi na kwamba tayari serikali ya China imetoa vifaa kwa Tanzania kwa ajili ya kugundua watu wanaosafirisha dawa za kulevya katika viwanja vya ndege.