Imeelezwa kuwa, Sekta ya Uvuvi ni miongoni mwa sekta zinazo ajiri watu wengi nchini kwani kwa mwaka huajiri watu Laki mbili, hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati akifungua Semina ya wataalamu wa Uvuvi kutoka nchi sita za Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda, Senegali na Tanzania ambayo ni Mwenyeji.
Ndikilo amesema, kwa wastani samaki wapatao tani 360,00 huvuliwa kila mwaka kwa kutumia zana mbali mbali za uvuvi ikiwapo, Nyavu pamoja na utumiaji wa boti.
Amesema katika dunia ya sasa ni yenye changamoto nyingi ni vema kila mara wataalam wakakutana ilikubuni mbinu mpya za uvuvi, kwani katika hata soko la Dunia ushindani ni mkubwa sana kutokana na kukuwa kwa Teknolojia hivyo ni wajibu wa kila nchi kuona inafanya bidii ilikuondoka na adha ya kutegemea mataifa makubwa.
Katika hatua nyingine Ndikilo amesema, suala la uvuvi wa dagaa nalo limekuwa na shida hasa kipindi cha mvua na kipindi cha kiangazi kikali hasa kwenye Mbaramwezi hivyo ni lazima zipatikane mbinu mbadala katika kukabiliana na hali hiyo " kwenye ziwa Viktoria pekee hupoteza asilimia 10% hadi 20% kutokana na sababu hizo.
Nchi ya Senegali ni nchi mojawapo barani Afrika iliyofanikwa kwa masuala ya uvuvi, kwani Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 1990's ilikopa teknolojia kutoka Taifa hilo la Magharibi mwa bara la Afrika
Post A Comment: