Waathirika wa kesi inayomkabili rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
wameutaka Umoja wa Mataifa kukataa wito wa kutaka kucheleweshwa kwa kesi dhidi
ya Rais Kenyatta katika mahakama ya kimataifa ya ICC mjini The Hague,
Uholanzi.
Baadhi ya viongozi wa Afrika wameandaa rasimu ya azimio la kuomba kesi
inayomkabili Rais Kenyatta iahirishwe kwa mwaka mmoja kwa masilahi ya usalama wa
taifa, kufuatia shambulio la kigaidi katika kituo cha kibiashara cha Westgate
mjini Nairobi.Lakini mwanasheria wa waathirika, Fergal Gaynor, amesema kucheleweshwa kwa kesi kutapunguza nafasi ya kupatikana haki kwa waathirika. Bwana Kenyatta anakanusha mashitaka yanayomkabili dhidi ya uhalifu wa kibinadamu, kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007.
Post A Comment: