Tumeshuhudia jamii ikikumbwa na
ukatili wa kijinsia hasa
kwenye vipigo, lakini kwa
msichana Juliana mambo yalikuwa ni tofauti yeye ni mtu aliyeonja ukatili
wa
kijinsia katika Nyanja ya kielimu.
Baba mzazi wa Juliana aliamua makusudi kuelekeza ukatili wa
kijinsia kielimu kwa binti yake,
fuatilia makala hii yenye simanzi na
masikitiko.
Baba hakutaka nisome kabisa, kwani
kila mara nilipomwambia kuwa nahitaji kusoma
aliniambia kuwa, kusoma kwa mtoto wa
kike hakuna maana yoyote mtoto wa
kike ana jukumu moja tu, ambalo nikuolewa. Alisema
Juliana alipokuwa akinisimulia kisa chake huku
akitokwa na machozi.
Juliana aliniambia kuwa kila mara alijitahidi kumshawishi
Baba yake juu ya yeye kupelekwa shule lakini Baba yake alilirudia kauli yake kuwa,
kusoma ni wajibu wa mtoto wa kiume. Baba yake
Juliana alikuwa na watoto wane, watatu wakiwa
wanaume, kwa upande wa watoto wa kiume wote walipelekwa
shule kasoro
ni Juliana tu ambaye alinyima haki
ya kielemu.
Ni
ukweli usiopingika kuwa kunyimwa kwa
fursa kwa Juliana kulimfanya
Juliana awepo hapo nilipomkuta, nilikutana na
Juliana katika standi kuu ya mabasi ya
Nyegezi Jijini Mwanza akiwa ameketi kwa
hudhuni huku pembeni yake kukiwa na sufulia la uji
wa ulezi aliokuwa akiuuza.
Kutokana na kuwa mapema sana asubuhi
wateja walikuwa hawajafika eneo hilo,
hivyo basi nilipata nafasi ya kumuuliza juu
ya maisha yake yaliyomfanya ajikute kuwa mama
lishe au ntilie , hapo ndipo aliporejea historia yake
ya miaka kumi iliyopita
iliyojaa uchungu na masikitiko ya ukatili wa
kijinsia katika Nyanja ya elimu.
Juliana alisema kuwa kaka yangu namini
leo hii na mimi ningekuwa
kama mama Anne Makinda ambaye ni spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa
Tanznaia, endapokuwa baba yangu hasingenitendea unyama wa
kijinsia kwa kuninyima haki ya kuwa na
elimu basi ningekuwa
mbali kaka yangu,
lakini ndiyo hivyo tena
naishia kwenye kuuza uji.
Juliana aliniambia kuwa, kaka
yangu makubwa
yalinipata kwani nakumbuka mara kwa mara
nilikuwa namkumbusha
baba juu ya kiu yangu ya kusoma,
lakini kuna siku sitaisahau, kwani nilipomkumbusha baba juu
ya suala hilo, aliishia kunipiga huku akiniambia
nishike kichwa changu kwa mikono miwili na
kumzunguka alipokuwa amesimama bila idadi ya mzunguko.
Ikumbukwe kuwa katiba ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania ibara ya 13: 6 inasema
ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu au
kumdhalilisha. Mimi naamini kama mwandishi natumia nafasi hii kupinga
ukatili wa kijinsia hasa kwa kutumia mbinu
za za kuripoti
ukatili wa
kijinsia kama TAMWA walivyoamua kuwajengea
uwezo waandishi wa habari kuripoti matukio hayo.
Chama cha
wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA)
kimekuwa kikipiga kelele huu ya
ukatili wa kijinsia , lakini bado kuna maeneo jamii inaendelea
na vitendo hivyo. Ni
wazi kuna Msichana
Juliana alinyimwa haki yake ya kusoma kwa kuwa
tu yeye ni msichana, huo ni
ukatili mkubwa wa
kijinsia.
Kwa sasa Juliana anaendelea na
biashara yake
ya mamaNtilie na amejiwekea malengo ya
kukusanya fedha kidogo kidogo na mwakani ana mpango wa kuanza
kujiendeleaza kielimu kwa kupitia elimu ya watu wazima.
Post A Comment: