Chama Cha wandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) kimeendelea na juhudi zake za kuwafunda waandishi wa habari mbinu za kuripoti na kuandika habari za ukatili wa kijinsia ili kumaliza tatizo hilo linaloonekana kuwa sugu katika jamii
Waandishi zaidi ya ishirini toka mikoa ya kanda ya kanda ya ziwa ikijumuisha Mwanza, Shinyanga, Bukoba na Kagera wamenufaika na mafunzo hayo kwa kupata miongozo ya jinsi ya kuandika habari za ukatili wa kijinsia.
Mwezeshaji mkongwe wa mafunzo hayo Bwana Ndimala aliwafunza washiriki wa mafunzo hayo jinsi ya kutumia vipaji vyao kuisaidia jamii iondokane na ukatili wa kijinsia.
Naye mshiriki wa mafunzo Bwana Revocatus Herman amesema kwamba, mafunzo hayo yatamsaidia kwa kiasi kikubwa kufahamu namna bora ya kuandika habari za kijinsia ili kuleta mabadiliko katika jamii juu ya utatili wa kijinsia.
TAMWA wamekuwa na programu endelevu ya kutoa mafunzo kwa waandishi ili kuwajengea uwezo katika kazi zao. Mafunzo hayo ni awamu ya pili kwa mwaka huu kufanyika .
TAMWA inawasaidia waandishi kufahamu mambo mbalimbali kama wajibu wa watunga sera kutika kukabiliana na ukatili wa kijinsia, mkataba wa SADC kuhusu jinsia na maendeleo na aina za ukatili wa kijinsia.
Awali yalifanyika kwa siku nne na awamu ya pili yalifanyika kwa siku mbili katika hotel ya midland Jijini Mwanza.
Imeandaliwa na Na: Neema Joseph, Mwanza
Post A Comment: