Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (wa nne kulia) akiwa na  Jenerali wa Magereza Tanzania John Minja (katikati)  wakimsiliza kwa makini Mnadhimu wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mmeta Manyara akijitambulisha. Kamishna Chato  ametembelea Makao Makuu ya Magereza ikiwa kni ziara ya siku sita nchini Tanzania.Wa tatu kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza John Yumbe, wa pili kulia ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Tebuho Nyambe na wa kwanza ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza James Nkoloma wote kutoka Makao Makuu ya Magereza nchini Zambia.


Kamishna wa Magereza nchini Zambia yuko katika ziara ya siku sita nchini kufuatia mwaliko uliotolewa kwake na Kamishna Jenerali wa Magereza wa Tanzania John Minja mwezi Septemba mwaka, 2013 alipotembelea Magereza nchini Zambia. Ziara ya Kamishna Percy pamoja na maafisa wengine watatu ni kudumisha ushirikiano uliopo kwa muda mrefu baina ya nchi hizi mbili na magereza kwa ujumla. Akiwa nchini Tanzania Kamishna Percy atatembelea baadhi ya Magereza na Vyuo vya Mkoa wa Dare es salaam, Kilimanjaro na Arusha ili kujionea shughuli za urekebishaji wa wafungwa zinavyofanywa kwa vitendo na kuona maeneo ambayo taasisi hizi mbili zinaweza kubadilishana uzoefu.
 
Askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM) cha Ukonga jijini Dar es salaam wakionesha aina mbalimbali za mzoezi ya kujihami na kuanguka bila kuumia katika kukabiliana na hatari yoyote, mblele ya Kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (hayupo pichani)

Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (mwenye suti) akikagua paredi maalum lililoandaliwa kwa heshima yake katika Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Dar es salaam.
 
Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (mwenye suti) akipokea salaam ya heshima kutoka kwa Paredi maalum (halipo pichani) lililoandaliwa maalum kwa jairi yake katika uwanja wa paredi wa Chuo Cha Maafisa wa Magereza Ukonga.Nyuma yake ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Ali Malewa na mwenye nguo za kijani ni Kaimu Mkuu wa Chuo  Kamishna Msaidizi wa Magereza Erasmus Kundi
Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato wa (pili kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa mafundi katika Karakana ya magari ya Magereza iliyoko Ukonga Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Ali Malewa.
: Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (katikati) akifurahia kukaa katika moja ya samani zinazotengenezwa kiwandani Ukonga, kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Tanzania, Dkt Juma Ali Malewa na kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza wa Zambia John Yumbe.
Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato ( wa nne kushoto), akipokea taarifa fupi kutoka kwa mmoja wa maofisa  kiwandani Ukonga. Kamishna Percy alitembelea Kiwanda cha Magereza Ukonga, Dar es salaam kuona shughuliza za urekebishaji wa wafungwa zinavyofanyika.
Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato akisaini kitabu cha wageni Kiwandani Ukonga, wa pili kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Tanzania Dkt Juma Ali Malewa
 Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato ( wa nne kushoto), akipokea taarifa fupi kutoka kwa mmoja wa maofisa  kiwandani Ukonga. Kamishna Percy alitembelea Kiwanda cha Magereza Ukonga, Dar es salaam kuona shughuliza za urekebishaji wa wafungwa zinavyofanyika.

PICHA NA HABARI KNY. YA JESHI LA MAGEREZA KITENGO CHA HABARI.

 

 

 

 

 

 

 

 
Axact

Post A Comment: