• Robert Mugabe amefikisha miaka 90 hii leo na wikendi hii kutakuwa na sherehe si haba nchini Zimbabwe kusherehekea maisha marefu ya kiongozi huyo.
HONGERA MIAKA 90 UMEFIKA MZEE.
 
Alizaliwa katika kijiji cha Kutama, kusini-magharibi mwa jiji kuu, alisomeshwa na wayesuti, na baadaye akawa mwalimu kabla kujiingiza katika harakati za kupigania uhuru wa Zimbabwe.
Uwanaharakati wake ulimfanya afungwe gerezani kwa miaka 11, na baadaye mwaka 1980 akawa Rais wa kwanza wa Zimbabwe.
Yafuatayo ni mambo tisa ambayo huenda hukuwa unayajua kumhusu kiongozi huyu na ambayo huenda yamemuwezesha kuwa rais kwa muda mrefu mno.

1) Zoezi na vyakula vya kienyeji

Mugabe akionekana kuwa na furaha mno
“Nakuwa mgonjwa wakati sijafanya mazoezi ya viuongo vya mwili,” Bw. Mugabe alisema miaka mitatu iliyopita. Huwa anaamka kati ya saa kumi na kumi na moja alfajiri, na kutoka na jamaa zake wa karibu, huwa anasikiliza BBC idhaa ya dunia mara kwa mara.
Siri nyingine ya kuishi kwake kwa muda mrefu ni kuwa hupenda sana-vyakula vya kienyeji kinacholiwa sana Zimbabwe lakini pia, havuti sigara, ilahunywa pombe kidogo anapokula chakula cha jioni na hasa Wine.

2) 'NI kweli alifufuka?'

Ingawa kumekuwa na uvumi mara nyingi kuwa Mugabe hana afya nzuri, afya yake na kazi yake ya kisiasa inaendelea vema kabisa. “ Nimekufa mara nyingi-hapo ndipo namwelekea Yesu Kristo. Yesu alikufa mara moja, na akafufuka mara moja,” alisema alipotimiza miaka 88.

Ingawa alilielewa kwa familia ya kikatoliki-mamake alikuwa mcha Mungu-alisema alipohojiwa na kituo cha habari cha Afrika Kusini, SABC, miaka michache iliyopita, kuwa si Mkristo anayetumikia dini kwa sana.

3) Je Unajua ni shabiki mkubwa sana wa kriketi?

Kwa muda mrefu amedhihirisha hadharani mapenzi ya mchezo wa kriketi. Ni patroni wa jumuiya ya mchezo wa kriketi wa Zimbabwe, ambapo nyumba yake ipo karibu na uga wa michezo wa Harare, ambapo anaweza kutazama kwa makini kriket wakati wa michezo ya kitaifa.
“Kriketi yafanya watu wawe wangwana, na pia inawafanya watu kuwa wema,” Bw. Mugabe alisema miaka kadhaa baada ya Zimbabwe kujinyakulia uhuru. “Nataka kila mtu acheze kriketi Zimbabwe; nataka nchi ya Zimbabwe iwe nchi ya wangwana.”

4) Hapendi kushindwa

“Alipokuwa kijana, Mugabe alikuwa “mmakinifu na mzuri kabisa” katika mchezo wa tennis,” alisema aliyekuwa mwalimu katika shule ya Wakatoliki aliposomea Mugabe. Ila, aliposhindwa katika mchezo huo, aliitupa raketi yake chini kwa hasira.
Mugabe amekiri kuwa hakuwa mzuri katika mchezo wa kandanda alipokuwa mdogo, ila kwa sasa, anapenda kuutazama mchezo huo. Yeye ni shabiki wa vilabu vya Chelsea na Barcelona vilivyoko Uingereza na Uhispania  “ Ninapotazama kandanda, sitaki usumbufu kutoka kwa mtu yeyote,” alisema mwaka wa 2012. “Hata mke wangu anajua mahala pa kukaa juu wakati wanapofunga bao uwanjani, hata mi pia nafunga bao kwangu kwa kupiga mateke vitu vyovyote vilivyoko mbele yangu.”

5) Kumbe alipata mtoto akiwa miaka 73!

Familia ya Mugabe
Ana watoto watatu na mke wake wa pili, Grace Marufu, aliyekuwa karani wake. Mtoto wao wa tatu alizaliwa 1997, mwaka mmoja baada ya wao kufunga ndoa.
Mwanawe wa kwanza, Nhamodzenyika, alikufa kutokana na Malaria akiwa miaka mitatu bado wakiwa Ghana. Bw. Mugabe hata hivyo hakupata ruhusa ya kwenda Accra kuungana na mkewe kwa mazishi ya mwanawe, kwani alikuwa mfungwa wa serikali ya enzi hiyo ya Rhodesia.

6) Anampenda Cliff Richard kumliko Bob Marley

Mwanasiasa wa Zimbabwe ambaye kwa sasa ni hayati, Edgar Tekere, alimwambia mwandishi wa BBC, Brian Hungwe, kuwa alipokuwa akitayarisha kadhia ya kusherehekea uhuru wa Zimbabwe 1980, Bw. Mugabe hakumtaka muimbaji Bob Marley aalikwe kutumbuiza watu, ila alimtaka muimbaji maarufu wa Uingereza, Cliff Richard. Pia anampenda Muimbaji, Jim Reeves.
Mugabe anawachukia sana wanamitindo wa rasta, na waimbaji wa mitindo ya reggae. Aliwaonya vijana wa Zimbabwe: “ Nchini Jamaica, wana uhuru wa kutumia bhangi, na wanaume huwa wakati wote wamelewa. Hawataki kuenda shule; wanataka tu kuimba, na kuwekea rasata nyweleni. Kama Zimbabwe, tusielekee hapo.”

7) Mvaaji wa nguo maridadi

Anapenda sana suti zinazoutosha mwili wake visawasawa na tai zinazofanana na kitambaa. Jinsi anavyovaa, imewavutia sana wanamitindo nchini Zimbabwe. Ila, mwanamitindo anayemvisha, Khalil Parbhoo anasema: “Bado anavaa kama mabwana wa Uingereza –hivyo ndivyo anavyopenda."

8) Anamtazama Kwame Nkrumah kama kielelezo kwake

Taarifa kuhusu hali ya kiafya ya Mugabe zimekuwa zikigonga vichwa vya habari karibuni
Bw. Mugabe alipata azma ya siasa akiwa Ghana alipokuwa mwalimu; mahali alipokutana na mke wake wa kwanza, Sally Hayfron.
Aliporudi Zimbabwe, aliwaambia wananchi jinsi Ghana ilivyojinyakulia uhuru, na jinsi uhuru ni kitu kizuri. Katika mahojiano mwaka 2003, Mugabe alisema: “Niliwaambia pia kuhusu Kwame Nkrumah jinsi alivyojitolea na kuiiongoza Ghana kupata uhuru;Kwame aliwaambia wa Ghana kuwa Ghana haingekuwa nchi huru bila ya jitihada na kujitolea kwa kila mtu.”

9) Ni mtu mwenye shahada nyingi

 
Kwa jumla, Mugabe ana shahada saba. Digrii yake ya kwanza ni kutoka katika chuo kikuu cha Fort Hare kilichoko Afrika Kusini. Alisomea digrii zake zingine kwa namna ya mtandao-mbili akiwa gerezani-shahada hizo ni za: ualimu, sayansi, sheria na usimamizi au utawala.
Amejikuta akiwa na “shahada katika ujuhula” alipokuwa akivionya vyama vya kutetea haki za wafanyakazi nchini Zimbabwe 1998 kila vilipotishia kugoma.

Habari hii ni kwa msaada wa Idhaa ya Kingereza ya BBC, Imetafsiriwa.
Axact

Post A Comment: