Sudan, waasi wapewa siku 10 kuanza mazungumzo.  

Thabo Mbeki.
   
Thabo Mbeki, mkuu wa kamati ya upatanishi ya Umoja wa Afrika katika mgogoro wa Sudan  
ametangaza kuwa, umoja huo umeipa serikali na waasi wa nchi hiyo muda wa siku 10. Sambamba na kuashiria kusimamia mazungumzo kati ya serikali ya Khartoum na waasi yaliyokuwa yakifanyika kwa lengo la kuhitimisha vita katika eneo la Kordofan na Blue Nile, Umoja wa Afrika umezipa pande mbili hizo hasimu muda wa hadi siku 10 ili kuanza tena mazungumzo hayo. Akielezea sababu za kusimama mazungumzo hayo, Mbeki amesema kuwa mazungumzo hayo yamesimama kutokana na Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Sudan, tawi la kaskazini (SPLM-N) kusisitiza kufikiwa makubaliano kuhusu masuala yote, huku upande wa serikali ukisisitiza kufikiwa tu makubaliano juu ya maeneo ya Kordofan na Blue Nile.
Tangu mwaka 2011 maeneo ya Kordofan kusini na Blue Nile ya kusini mwa Sudan yamekuwa yakishuhudia mapigano kati ya waasi wa harakati ya SPLM kaskazini na serikali ya Khartoum.


 



Axact

Post A Comment: