Hawa Ndio Munich ambao hata hivyo bado wana kiwewe na Arsenal.

Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola amekiri ni vigumu sana kudhibiti dakika tisini za mechi ya aina yeyote dhidi ya Arsenal ya Uingereza .
Guardiola

"Unaweza cheza vizuri na utawale nyanja zote kwa dakika 30 ama 75 hivi lakini zile zitakazosalia utakabiliwa na upinzani mkali "
Guardiola ambaye hajashinda katika mechi zake mbili uwanjani Emirates ,anatarijia ushindani mkali .
Licha ya hayo , Bayern Munich imeshindwa katika mechi mbili pekee msimu huu.
Bayern ilishindwa na Borussia Dortmund na Manchester City mapema katika mkondo wa kwanza wa ligi ya msimu huu.

Metsu O'zil - Mchezaji wa Arsenal
Mwaka uliopita Bayern,iliilaza The Gunners 3-1 katika hatua hii ya Robo fainali.
Hata hivyo vijana wa Pep walifuzu kutokana na sheria ya bao la ugenini licha ya kushindwa 2-0 katika mkondo wa marudiano huko Ujerumani.

Vijana wa Arsene Wenger hawajahi kushinda taji lolote tangu mwaka wa 2005 lakini Guardiola anasisitiza kuwa sio timu hafifu kamwe.
Kwa hisani ya BBC swahili.
Axact

Post A Comment: