Asema utawafanya wakose nguvu ya pamoja.
MKUU WA MKOA WA MWANZA MHE. EVARIST NDIKILO ( Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa) |
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, amewatahadharisha Wanachama wa chama
kikuu cha Ushirika Mkoani Mwanza kinacho
unganisha Mikoa ya kanda ya ziwa ambayo
ni maarufu kwa kwa kulima pamba, Nyanza
1984 LTD, kuhusiana na fikra zakutaka kuanzishwa kwa Ushirika mwingine wa Mkoa
wa Geita na kusema kufanya hivyo kutafanya Nyanza kukosa nguvu na kusababisha
kuparaganyika vipande vipande.
Ndikilo ameitoa kauli hiyo wakati akifungua Mkutano
wa ishirini na nne katika ukumbi wa chuo cha Uwalimu Butimba kwa niaba ya
Waziri wa Kilimo, Ushirika na Chakula mkoani hapa.
Amesema
wakati wanafikiria kuanzishwa kwa ushirika kwa mkoa wa Geita ni lazima
wafikirie juu ya amali mbali mbali za Ushika huo, sambamba na madeni yaliyopo
pamoja na matatizo mengine mengi yanayo kikabili chama hicho kikuu cha ushirika
Mkoani hapa na kanda ya ziwa kwa ujumla.
“Ndugu
zangu kuna usemi unaosema umoja ni nguvu Utengano ni udhaifu lakini pia
waingereza wana msemo wao usemao (..divide them.., .. and role them easily),
sasa wakati mnapofikiria juu yakuanzisha Ushirika mwingine lazima haya yote
mwende nayo, alisema Ndikilo na kuongeza, “ Unajua mtu anaye taka kukutawala
lazima ahakikishe mmekuwa vipande vipande ndipo aweze kupitisha ajenda zake
kirahisi na kisha kukutawala atakavyo.
Alisema
wakati huko Ulaya wanafikiria jinsi yakuongeza ukubwa kwa kuungana sisi
tunafikiria namna gani tuweze kujitenga vipande pande hii haina tija wala afya
kwa umoja wetu,.. narudia kusema tena ndugu zangu hii ni hatari sana kwa
ushirika wetu huu.
Akaendambali
zaidi na kutahadharisha kuwa kwa hivi sasa chama hicho kina madeni ambayo wadau
mbali mbali wanaidai Nyanza LTD 1984 lakini pia kuna baadhi ya wadau wanadaiwa
na Nyanza 1984 LTD, hivyo kuanza kugawanya gawanya vipande vipande inakuwa
ngumu sana katika kushughulikia migogoro hiyo.
Awali
akisoma risala ya Waziri mwenye dhamana na ushirika, Mkuu huyo wa mkoa, alisema
suala la ulinzi wa mali za chama ulisha tolewa ufafanuzi na aliyekuwa waziri wa
Kilimo chakula na Ushirika Steven Wasira wakati wa Mkutano mkuu wa chama hicho
uliofanyika 2009, ambapo waziri huyo alionya wachache wajanja kutotumia mwanya
wa udhaifu unaojitokeza katika chama katika kukihujumu chama hicho.
Hata
hivyo kwa Mujibu wa habari ambazo mtandao huu wa www.kuninewsblogspot.com
umezipata na kuthibitishwa na
Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya ushirika mkoani hapa bwana Emmanuel Omuyanja zimesema wajumbe wote
wa kamati hawakuwa tayari kukubaliana na hivyo mada ambayo ilikuwa
imetayarishwa kwa ajili hiyo kuwekwa kando.
Post A Comment: