|
MTAALAM BWA ONUR OZLY KUTOKA WB AKITOA MCHANGO WAKE JUU YA UMUHIMU WA MFUMO GIS. |
|
JEMA NGWALE MWAKILISHI WA DANIDA AKIZIASA HALMASHAURI KUONA UMUHIMU WA KUTENGA FEDHA ZA MAFUNZO KWA KWA AJILI YA MFUMO WA GIS UNAOTUMIKA KATIKA UKUSANYAJI MAPATO. |
Mfumo wa Ukusanyaji mapato ya Serikali katika Ngazi ya Halmashauri na majiji utakuwa wenye tija na wenye manufaa endapo Halmashauri zote nchini zitafanikiwa kuingia katika mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kwa njia ya Kieletroniki na kuachana na mfumo wa Analogi ambao tija yake imekuwa ndogo kadri siki zinavyokwenda,
Haya yamebainika katika kikao kinachoendelea katika jijini Mwanza, ambapo wataalam kutoka katika halmashauri za manispaa na Majiji yaliochini ya mpango wa TSCP wanaendelea na kikao chao kwa siku ya tatu mfulululizo.
Akiwasilisha mada katika kikao hicho mhasibu kutoka katika Jiji la Arusha Prosper Mlacha amesema kabla yakuanza kutumika kwa mfumo mapato yalikuwa kidogo ukilinganisha na kiwango cha sasa mara baada ya kuanza kutumia mfumo wa Ukusanyaji mapato wa halmashauri kwa kutumia komputa (Local government Revenue Collection Information System) (LGRCIS) amesema, kabla ya kuanza kutumika kwa mfumo katika kipindi cha mwaka 2012/2013 makusanyo yalikuwa bilioni 5.8 na mara baada yakuanza kutumika kwa mfumo mapato yalipanda kutoka bilioni tano hadi kufikia bilioni 8.8 ambapo ni ongezeko la karibia asilimia 44.2.
Kwa upande wake Judith Ngulwa kutoka Jiji la Mbeya alisema mapato kwa upande wao yalipungua kutoka mwaka 2012/ 2013 katika robo ya kwanza 844,947940 na kushuka zaidi 7,52,892,452 kabla yakuanza kutumika kwa mfumo wa LGRCIS kwani mara baada yakuanza kutumika kwa mfumo wa LGRCIS, mapato katika robo ya kwanza yameongezeka kutoka kiasi tajwa hapo juu kwani katika kipindi hicho hicho katika robo ya kwanza ya mwaka 2014 wamepanda na kufikia Bil. 1,778,962.
Kwa upande wake mtaalamu mshauri kutoka DANIDA Jema Ngwale, amezitaka Halmashauri kutenga fedha kwa ajili yaku karabati mifumo ya ili iweze kuendelea kufanya kazi, "Tusitegemee kwamba hawa wahisani wataendelea kuwepo siku zote ni lazima sasa tujifunze ili hata pale watakapo maliza muda wao basi tuendelee sisi wenyewe" alisema na kuongeza " Lakini pia tuone namna yakutenga fedha kwa ajili ya mafunzo kwa watumishi wapya lakini pia wale wa zamani kwani mifumo katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia inabadilika sana" aidha katika hatua nyingine ameziasa halmashauri hizo kuwa zina badilishana taarifa mbali mbali kuhusiana masuala mazima ya mfumo" Ni vema mkawa mna share Information kwa ajili yakujua wenzenu katika maeneo mengine wanafanyaje.
Hadi hivi sasa halmashauri ambazo zipi chini ya mpango huo ni pamoja na Mtwara Mikindani, Mwanza, Manispaa ya Ilemela, Jiji la Arusha, Dodoma Manispaa, Dodoma CDA, Tanga pamoja na Kigoma ambayo ndio imeanza hivi karibuni.
Post A Comment: