Kwa hisani ya Mdau G. SENGO!

KAMA UNADHANI MIUJIZA ILIKUWA WAKATI ULE HADI HII LEO IPO, MSUKUMA HUYU KACHIMBIA
KICHWA KWENYE MCHANGA KWA DAKIKA KADHAA, MBWEMBWE ZA MCHEZO TU HAPOA

Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu, waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na mbunge huyo wa ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
MBUNGE wa Jimbo la Kisesa(CCM), Luhaga Mpina ameahidi kuendelea kuenzi utamaduni wa ngoma za kabila la wasukuma kwani zimekuwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano miongoni mwa jamii hiyo.
Mpina alitoa kauli hiyo juzi wakati akifunga mpambano wa ngoma za asili katika Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu uliwakutanisha Malogi Hamsini Mgika na Magise Jilunga Mgalu.

Hata hivyo katika mpambano huo ulihudhuriwa na watazamaji zaidi elfu nane kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Simiyu ambapo Magise Jilunga aliibuka mshindi baada ya kumbwaga Malogi.

Akizungumza mara baada ya mpambano huo, Malogi Hamsini alikubali kushindwa na mpinzani wake na kueleza kuridhika na uamuzi uliofanywa na kuomba kukutanishwa tena siku nyingine na mpinzani wake huyo.

Naye Magisa Jilunga alisema pamoja na kumshinda mpinzani wake lakini alikiri pambano hilo lilikuwa gumu kwake na kuamba nae pia kurudiana ombi ambalo lilikubaliwa na Mbunge wa jimbo hilo.

Pambano hilo lililodhaminiwa na Mbunge Mpina lilivuta hisia za mashabiki wengi na kuomba kufanyika mara kwa mara kwa pambano hilo kwani linaleta umoja na mshikamano miongoni mwa jamii.

Mpina aliwazawadia shilingi milioni moja kila mmoja katika mpambano huo na kuahidi kudhamini tena pambano lingine kama hilo baadae mwakani.ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA YALIYOJIRI
Wachezaji wa ngoma toka kundi la Malogi Hamsini ambaye ni Mgika wakifanya yao.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akipiga ngoma kuashiria ufunguzi wa mpambano wa ngoma asili kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
Kiongozi wa Wagika, Malogi Hamsini (kulia) akiwa amesimama barabara kuuanza mpambano ambapo alizidiwa nguvu ya uchawi na Mpinzani wake Magise Jilunga ambaye Mgalu.
Wachezaji wa kundi la Malogi Hamsini wakionyesha kazi.
Mara baada ya kuona ameshindwa katika nguvu za kichawi Malogi Hamsini alipandwa na hasira ampazo alizielekeza kweye tunguli zake.
Na hapo ndipo alipo amua kuziteketeza kwa kuzifumua kwa mateke..... PwachAaA!!
Wingi wa watu ndiyo pointi za ushindi watu walihama toka kwa Malogi Hamsini na kuelekea kwa Magise Jilunga ambapo kila mmoja alikuwa akipiga ngoma kwa wakati mmoja (yaani kulia na kushoto wapi pananoga?).
Wananchi wakiwa wameizunguka himaya ya Magise Jilunga.
Kiongozi wa Wagalu, Magise Jilunga wa pili kutoka kushoto akiwa tayari kulianzisha kwenye mpambano kati yake na Malogi Hamsini ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina.
Hatari kama anaporomoka vile...
Malogi Hamsini alituma nyoka kuja kuharibu ngoma ya Magise Jilunga lakini hakufua dafu.
Mapanga dizaini....
Akinamama wakiingia kwenye lango kuu kushuhudia mpambano.
Michezo ya hatari balaa ni mwendo kugalagala kwenye moto.
Silaha ya ushindi kwa Magise Jilunga ilikuwa ni kubadilika badilika.
Si kubadilika tu bali alikuwa na vionjo kama kuoga moto mchana kweupe na kunywa mafuta ya dizeli...tobA!
Ni balaa mwanawane!!!
Jamaa aliamua kukizika kichwa kwa dakika kadhaa kiasi cha kusisimua mashabiki!!
Kiongozi wa Wagalu, Magise Jilunga akipiga ngoma kuusaka ushindi.
Viongozi wa kada mbalimbali nao wamo.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu, waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na mbunge huyo wa ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
Maelfu waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na Mhe. Mbunge, ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
Ni wakati wa jaji Mkuu kutangaza matokeo rasmi:- Mpambano wa ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
"Mshindi ni Magise Jilunga...!!"
 Malogi Hamsini (kushoto) akimpongeza kiroho safi Magise Jilunga mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi....
Full m-banano.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akiwaaga wananchi wa Jimbo lake mara baada ya kumalizika mpambano.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akiwaamezungukwa na maelfu ya wananchi waliofika eneo la uwanja wa kusanyiko.
Axact

Post A Comment: