JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA
WATOTO
(TAARIFA KWA UMMA)
WITO WA KUWASILISHA MUHTASARI WA MADA (ABSTRACT) KWA AJILI YA KONGAMANO LA KITAIFA LA SIKU YA WANAWAKE
DUNIANI LITAKALOFANYIKA MOROGORO 6/03/2015
Tarehe 8 Machi, 2015 Tanzania itaadhimisha
Siku ya Wanawake Duniani ambayo itaadhimishwa kitaifa mkoa wa Morogoro. Kauli
Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake mwaka 2015 ni “Usawa kwa Wanawake ni
Maendeleo ya Haraka kwa Wote”.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, itaadhimisha
siku hiyo kwa kuandaa kongamano la kitaifa litakalofanyika tarehe 6/03/2015 mkoani
Morogoro sanjari na wiki ya maonesho ya wadau mbalimbali yatakayozinduliwa
tarehe 03/03/2015 na kufikia kilele chake
tarehe 8/03/2015. Lengo kuu la kongamano ni kujenga jukwaa la majadiliano ya
kina kuhusu masuala ya maendeleo ya wanawake na usawa wa kijinsia.
1. Ukatili wa kijinsia (intimate partner violence- Ukatili
katika mahusiano)
2. Haki za wanawake/binadamu na mchango wa wanaume katika
utetetezi wa haki za wanawake (Kwa mfano, ubakaji, ukatili kwa watoto/
wasichana)
3. Hali ya Mtoto wa Kike (mf. Ndoa za utotoni)
4. Ajira salama na haki katika ajira,
5. Tathimini ya sheria na sera (dawati la jisia na polisi)
na
6.
Majadiliano ( panel discussion) kuhusu uwezeshaji wa wanawake
kiuchumi.
Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto inakaribisha mwanajamii yeyote aliyetayari
kuandaa mada katika maeneo yaliyotajwa hapo juu, awasilishe muhtasari wa mada
yake (ikisiri, abstract) yenye maneno kati ya 300 na 500 kwa ajili ya
maandalizi ya kongamano hili muhimu. Siku ya mwisho ya kuwasilisha maelezo hayo
(abstract) ni tarehe 20/01/2015.
Waandishi
ambao muhtasari wa mada zao utakubaliwa watafahamishwa tarehe 20/01/2015 na watashirikishwa
katika maandalizi ya mada kamili tarehe 31/01/2015.
Maelezo ya
mada (abstract) yatumwe kwa:
(i) Elizabeth Makawa: e_palelamakawa@yahoo.com – Simu No. 0655
975478
(ii) Dinah Enock: edinnah@yahoo.com – Simu No. 0766
070376
(iii) Judy Kizenga: kizengajudy@yahoo.com - Simu No. 0754 564414
Tangazo hili limetolewa na
Anna
T. Maembe
Katibu Mkuu
05/01/2015
Post A Comment: