|
WAKUU WAPYA WAWILAYA ZA MKOA WA MWANZA WALIOSIMAMA KWA NYUMA, WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA. |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, amewaapisha Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais kwenye viwanja vilivyopo kwenye Ofisi ya Mkuu wa mkoa.
Walio apishwa na kupewa majukumu ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Zainab Terack, mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mwajuma Nyiruka na mkuu wa wilaya ya Kwimba Pili Moshi.
Akiwaaasa mara baada ya kuapishwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, aliwaambia viongozi hao wapya katika nafasi ya ukuu wa wilaya, waende wakawatumikie wananchi na kwamba huko kwenye wilaya zao kuna viongozi wengine walioko huko waende kujifunza kutoka kwao ili waweze kuwahudumia wananchi. " mimi niowaombe ndugu zangu wakuu wa wilaya wala msiogope huko muendako kuna viongozi wenzenu chukueni muda mjifunze kwao" alisema Mulongo na kuongeza kuwa zipo changamoto kadhaa kwenye wilaya ambazo wamepangiwa ikiwapo ya suala la ulinzi na usalama wameaswa kulipa kipaumbele katika shughuli zao za kila siku lakini wahakikishe pia wanasimamia shughuli za maendeleo .
FATILIA HAPA CHINI MATUKIO KATIKA PICHA.
|
SHEHE HASSAN KABEKE AKITOA MAOMBI WAKATI WA SHUGULI YAKUWAAPISHA WAKUU WA WILAYA. |
|
WAKUU WA WILAYA ZA MKOA WA MWANZA, KUTOKA KUSHOTO NI CAREEM YUNUS (MAGU), MANJU SALUM MSAMBYA(ILEMEL), MWAJUMA NYIRUKA(MISUNGWI), BARAKA KONISAGA (NYAMAGANA), PILI MOSHI(KWIMBA), JOSEPH MKIRIKITI (UKEREWE) NA ZAINAB TERACK (SENGEREMA) |
|
MKUU WA WILAYA YA KWIMBA PILI MOSHI AKIPOKEA ZANA ZA KUFANYIA KAZI MARA BAADA YA KUAPISHWA. |
|
MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA ZAINA TELACK AKILA KIAPO MBELE YA MKUU WA MKOA HAYUPO PICHANI SIKU YA TAREHE 25.2.2015 KWENYE VIWANJA VYA OFISI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA. |
|
BAADHI YA WAGENI WAALIKWA WAKIFATILIA ZOEZI LA KUAPISHA WAKUU WAPYA WA WILAYA. |
|
WATUMISHI WA OFISI YA MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA WAKIMPONGEZA MKUU WA WILAYA HIYO BARAKA KONISAGA, BAADA YAKUBAKIZWA KWENYE KITUO HICHO, HAPA NIKATIKA VIWANJA VYA OFISI YA MKUU MKOA WA MWANZA. |
|
KATIBU WA ALBINO MKOA WA MWANZA NAYE ALIPATA FURSA YAKUTOA NENO KWENYE HAFLA HIYO |
|
BAADHI YA WAGENI WAALIKWA WAKIFATILIA ZOEZI LA KUAPISHA WAKUU WAPYA WA WILAYA. |
Post A Comment: