MKUU WA MKOA WA MWANZA MWENYE SHATI JEUSI, MAGESA MULONGO, AKIONESHWA KITU NA MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA WAKATI WA MOJA YA ZIARA YAKE MKOANI HUMO. |
Wazee
katika Mkoa wa Mwanza, wamemshauri Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kuanza kulima zao la
alizeti ili kuuwezesha mkoa huo kuinuka kuichumi kutokana na hali mbaya ya
mazao kama pamba kupoteza umaarufu kwenye sekta ya uchumi wa mkoa huo.
Wakizungumza
katika kikao kilicho wakutanisha wazee hao na mkuu wa mkoa hivi karibuni katika
hoteli ya Mwanza, wazee hao walisema kutokana na hali isiyoridhisha kwa zao
kama pamba ambalo ndilo lilikuwa zao kuu la uchumi wa mkoa huu kupoteza
umaarufu ni vema sasa jamii ikabadilika na kuhamishia nguvu zake kwenye zao la
alizeti.
Akizungumza
kwa niaba ya wazee wenzake, aliyekuwa Mkuu wa kwanza wa wilaya ya Ilemela, Jared John Gachocha,
alisema, haoni sababu ya mkoa wa Mwanza kushindwa kutilia mkazo zao la alizeti
ambalo gharama zake za uzalishaji ni nafuu zaidi ukilinganisha na pamba.” Mh.
Mkuu wa mkoa mimi nadhani kipindi hiki tushughulike kufa na kupona kwenye
alizeti, sioni kwa nini wenzetu wa Singida watupite katika hili, zao la alizeti
ni rahisi mno kulilima halina usumbufu halihitaji mbolea nyingi, haliitaji maji
mengi na maandalizi yake kwakweli ni rahisi lakini pia faida yake ni kubwa”
alisema na kuongeza kuwa “hali hiyo itasaidia mkoa kujitosheleza kwa mafuta
lakini pia kuweza kuuza kwa watu wengine.
Mbali
ya zao la alizeti wazee hao pia walimuasa mkuu huyo wa mkoa, kuelekeza nguvu
zaidi kwenye masuala ya ufugaji, wakisema kuwa tupo nyuma sana katika masuala
ya mifugo huku wakitolea mfano nchi ya Kenya kwamba Ng’ombe anauwezo wakutoa
maziwa lita hadi 20 tofauti na Tanzania, hali inayo walazimu wazee hao kumuasa
mkuu wa mkoa kuwataka wafugaji kuachana na ufugaji wa kizamani na badala yake
watafute mitamba itakayoweza kuleta tija kwa wafugaji. “Ni ukweli usiopingika
kwamba hapa kwetu kumpata ng’ombe anayeweza kukupatia lita 10 za maziwa ni
nadra sana hivyo tuwashawishi wakulima waweze kutafuta mitamba ambayo itakuwa
niya kisasa ili waweze kukuza uchumi wao lakini uchumi wa mkoa kwa ujumla.
Awali
akizungumza mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kabla yakuanza kupokea maoni ya wazee hao,
alisema mkoa wa Mwanza wenye watu Milioni mbili na laki saba na mia saba sabini
na mbili mia tano na tisa, huku mkoa ukiwa unachangia Trioni 4.9 katika pato la
taifa, Watu wake milioni moja uchumi wao
unategemea zaidi katika Sekta ya Uvuvi, “Wazee wangu nimewaiteni tusaidiane
kuongoza mkoa huu, mkoa huu ni mkubwa na changamoto tulizo nazo ni nyingi”
alisema Mulongo na kuongeza kuwa, “kati ya watu mil. 2.7, watu Milioni moja wanategemea
ziwa kuanzia mvuvi ziwani hadi mparuaji na mchuuzi mdogo mdogo wa mtaani sasa
hali ya ziwa letu kwa upande wa uzalishaji sio salama sana, tuna kwendaje
lazima tujipange kisawasawa alisema Mulongo.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza toka amewasili mkoa wa Mwanza, ameweka utaratibu wakukutana
na watu wa makundi mbali mbali mkoani hapa ili kufahamu changamoto ambazo zipo
ili waweze kuzitatua kwa kushirikiana kwa pamoja, makundi ambayo tayari
yamekutana na mkuu huyo wa mkoa hadi sasa ni pamoja na, Wananchi wa kawaida kwa
kuzungumza nao kwenye mikutano ya hadhara na kusikiliza kero zao na kuzipatia
ufumbuzi, Wafanya biashara wadogo ambao alifanikisha kufanyika kwa uchaguzi
wao, wakuu wa taasisi za umma zilizoko mkoani hapa, viongozi wa dini, viongozi
wa kisiasa na asasi zisizo za kiraiya.
Mkoa
wa Mwanza ni mkoa wa pili kwa uchangiaji wa pato la taifa kwa asilimia 9.15% ukitanguliwa na Mkoa wa Dar Es Salaam, huku
wastani wa pato la mwananchi wa kawaida ikiwa ni
Tshs. 910,824 kwa mwaka.
Post A Comment: