Wakala wa Vipimo nchini imezuia matumizi ya mizani 94 kati 150 ya vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) katika Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, isitumike hadi pale itakapo fanyiwa marekebisho na kuonekana inafaa kwa matumizi.
Wakala wa Vipimo Mkoani humo imesema, kuzuiliwa huko
kutakwenda hadi msimu ujao wa ununuzi wa ufuta na korosho, na ili iweze
kutumika ni mpaka pale itakapo fanyiwa
marekebisho na Mafundi Mizani na kisha kugongwa mhuri tena kwa ajili ya
matumizi.
Afisa Vipimo akikagua
mawe ya Mizani kabla ya kuanza kuipima
|
Afisa Vipimo akikagua
mawe ya Mizani kabla ya kuanza kuipima
|
Wakala wa vipimo imesema katika zoezi hilo la ukaguzi wa
Mizani Wilayani Ruangwa imehakiki jumla ya vyama vya ushirika vya msingi
(AMCOS) 23 na kukagua jumla ya mizani 150 ambapo kati ya mizani hiyo iliyopimwa
na kuhakikiwa kuwa sahihi ni mizani 56 na iliyozuiliwa kutumika mpaka
itakapofanyiwa marekebisho ni mizani 94.
Kwa mujibu wa wakala wa vipimo Mizani mingi imeonekana
kuwa na mapungufu kama vile kutokuwa na vipimo sahihi, “Ni kwamba mizani hii
tuliyo ipitia tumeabaini ina mapungufu kuanzia 200g hadi 1kg ambayo kwa kawaida
mzani unatakiwa kuwa na Upungufu unaokubalika wa kiasi cha 80g tu” alisema
mmoja ya maafisa wa wakala wa vipimo.
Ameongeza kuwa, Vilevile
baadhi ya mizani imechakaa na kusababisha kupoteza usahihi katika Upimaji wake
kutokana na namna mizani hiyo inavyo hifadhiwa mara baada ya msimu wa ununuzi
kukamilika, “Mizani mingi huifadhiwa katika maeneo machafu yenye vumbi ambayo
husababisha mizani kupata kutu, lakini pia njia inayotumika kusafirishia mizani
hiyo si salama kwani mizani mingi husafirishwa kwa Usafiri wa pikipiki mara
baada ya msimu mauzo kukamilika, ambapo husababisha mizani kuangusha baadhi ya
vifaa vyake muhimu wakati wakusafiri”. Imesema taarifa hiyo ya wakala wa
vipimo.
Afisa Vipimo akibandika stika katika mizani uliopasishwa kwa
ajili ya ununuzi wa mazao wakati wa msimu
|
Kwa upande wake Meneja wa mkoani Lindi Bw. Stephen
Masawe ameeleza kuwa wameamua kuendesha zoezi hilo la ukaguzi wa mizani ili
kubaini mizani iliyo sahihi na isiyo sahihi ili kuipitisha kwa ajili ya msimu
ujao wa ununuzi wa mazao.”tunaelekea katika msimu wa ununuzi wa mazao, hivyo
kama mkoa lazima tujiridhishe na mizani iliyopo, kabla msimu haujaanza”, alisema
Masawe.
Aidha amesema
kwamba, kwa mizani itakayo hitaji
marekebisho mafundi watapita kuifanyia ukarabati kisha tutaihakiki upya na kama
itakuwa sawa basi itapasishwa kwa ajili ya msimu huu wa ununuzi wa ufuta na
korosho.
“Zoezi hili
litapunguza sana gharama za uendeshaji wa vyama vya ushirika vya msingi kwani
awali mafundi mizani walikuwa wanapita na kurekebisha mizani zote, hii ilikuwa
inapelekea nyama vya ushirika vya msingi kutumia gharama kubwa ya matengenezo
hadi Tsh. 400,000= kwa mzani Mmoja lakini kwa sasa mafundi watapita kurekebisha
mizani iliyobainika kuwa na mapungufu ambayo yameainishwa na Wakaguzi wa mizani
tu” alisema Masawe.
Zoezi la uhakiki wa mizani lilianzia katika Wilaya ya
Ruangwa na sasa zoezi hilo limehamishiwa katika Wilaya ya Nachingwea mkoani
humo, zoezi hilo la ukaguzi wa Mizani ni zoezi endelevu ambalo humsaidia
mnunuzi na muuzaji kutopunjana wakati wa mauzo ya mazao.
Wilaya ambazo
hadi hivi sasa hazijafanyiwa ni Liwale, Kilwa, Lindi Mjini na Lindi Vijijini
hata hivyo wakala wa vipimo amesema zoezi hilo litandelea katika wilaya hizo.
Nao wananchi kwa upande wao wameipongeza Wakala wa
Vipimo kwa kuwapa elimu ya matumizi sahihi ya Vipimo
pamoja na kufanya ukaguzi wa Mizani kabla ya mafundi kupewa tenda ya
kuitengeneza,
Akizungumza kwa niaba ya wnanchi wenzake ndugu Laurent Adrian Muya, ambae ni
mwanakijiji wa Michenga A amesema, kuhakikiwa kwa mizani kunawapa faraja na inatoa
picha kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha mkulima hapunjwi
wala mnunuzi hapunjiki, “Uhakiki huu wa mizani ni ishara kwamba, Serikali yetu
imedhamiria kumkomboa mwananchi, tunampongeza sana Rais wetu John Pombe Magufuli,
Mungu ambariki”, alisema Laurent.
Stika maalum ikiwa imebandikwa katika mizani baada ya
kuhakikiwa na kupasishwa
|
Jiwe la Mizani likiwa limegongwa muhuri wenye nembo ya Bibi
na Bwana pamoja na tarakimu mbili za mwaka husika (17)
|
Afisa Vipimo akikagua rula ya Mizani kabla ya kuanza kupima
|
Kila mwaka Wakala wa Vipimo huendesha zoezi la Uhakiki
kwa nchi nzima inapofikia msimu wa ununuzi wa mazao ya Biashara na Chakula na
katika msimu wa 2017/2018, zoezi hilo limeanzia katika mikoa ya kusini ya
Lindi, Mtwara na pamoja.
Post A Comment: