Ikiwa leoni tarehe 21 Mei 2017, wananchi katika mkoa wa Mwanza wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, wameendele kuwalilia na kuwakumbuka watu waliozama na Meli Mv. Bukoba, huku simanzi na majonzi vikishindwa kufutika katika fikra na mawazo ya watanzania.
Eneo la Makaburi ya Mv. Bukoba Jijini Mwanza katika Wilaya Nyamagana eneo la Igoma |
Akizungumza
katika kumbukumbu hiyo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, amewataka watanzania kila mmoja
kwa imani yake kuendelea kuwaombea marehemu wote waliotangulia mbele ya haki
huku akiwataka wamili wa vyombo vya usafiri wa majini kuwa makini na
kuhakikisha vyombo vyao vinakaguliwa kabla yakuanza safari.
“Napenda
kuchukua fursa hii pia kutoa wito kwa wasafirishaji na wasafiri kuzingatia
usalama ili kukabiliana na ajali zinazoweza kuzuilika”, amesema Mongella na kuongeza kuwa “kusaidia
kutoa taarifa katika vyombo husika pale mnapoona kuna dalili za uzembe wa kutozingatia
usalama ili hatua zichukuliwa mapema kabla ya ajali kutokea”.
Aidha,
amewaomba wananchi wasikubali kupanda
vyombo vya usafiri vilivyojaa kupita kiasi na vile vyombo visivyo imara.
amewataka
wananchi wote kushirikiana na Serikali katika kuhifadhi kumbukumbu hizi muhimu
kwa ajili ya ndugu waliotangulia mbele ya haki.
Kumbukumbu
hiyo ilifanyika katika eneo la Makaburi ya Mv. Bukoba Eneo la Igoma Mwanza na
kuhudhuriwa na wananchi pamoja na Viongozi wa dini na serikali waliokusanyika
kwaajili yakuwaombea marehemu hao, kwa sala na Duwa zilizo ongozwa na viongozi
wa dini.
Mmoja
ya Manusura wa ajali hiyo Charles Limbu, amesema, suala la elimu wakati wa kusafiri ni
muhimu sana kwani mbali yakutokujua kwake kuogelea lakini, alimu aliyoipata
wakati wa kuanza safari katika bandari ya Kemondo mkoani kagera ndiyo ilikuwa
pona pona yake. “Mimi nilipoona chombo kinazidi kupoteza muelekeo niliamua
kukimbilia kuchukua boya na ndilo lililo nisaidia” alisema Limbu.
Mv.
Bukoba ilizama 21 Mei, 1996 na kuuwa watanzania kwa mamia waliokuwa wakisafiri
kwa meli hiyo kutokea mkoani Kagera kuelekea Mwanza na kisha kuzama umbali
mfupi kabla yakutia nanga katika Bandari ya Mwanza.
Post A Comment: