Kamishna mkuu wa TRA nchini Charles Kichere, akizungumza katika kikao hicho na waandishi wa habari hawapo pichani. |
Mamlaka ya mapato nchini
imetoa muda hadi kufikia Juni 30, mwaka
huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya majengo kuhakikisha wanailipa kodi hiyo
ilikuepuka kufikishwa mahakamani na kutozwa faini.
Kauli
hiyo imetolewa na kamishina mkuu wa TRA nchini ndugu Charles Kichere, alipokuwa
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza hii leo.
“Mwisho
wa kulipa kodi ya majengo bila adhabu ni tarehe 30 Juni, 2017. Hivyo wenye
majengo yaliyopo katika Halmashauri ya
Jiji la Mwanza (Nyamagana), na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo
karibu nao kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa
serikali za mitaa yao au kujisajili na
kulipa kupitia benki yoyote ya biashara” alisema Kichere.
Kichere amefafanuakuwa kwa walioko sehemu ambazo nyumba
zimethaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya thamani ya jengo kama inavyoonesha
kwenye ankara zao na walioko maeneo ambayo hayajapimwa au kuthaminishwa
watalipa viwango maalum vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na kutangazwa na
TRA kwenye vyombo vya habari.
Kichere amevitaja viwango hivyo vilivyopitishwa kuwa, ni shilingi za
kitanzania (20,000) kwa Jiji la Mwanza na kumi na tano elfu (15,000) kwa
Manispaa ya Ilemela.
TRA pia imepongeza ushirikiano
mkubwa inaoupata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na safu yake nzima ya
uongozi ikiwemo Serikali za Mitaa husika. “Mhe mkuu wa Mkoa ushirikiano huo umetuwezesha
kutoa makadirio sahihi ya tozo, kutumia viwango rafiki, kuimarisha usimamizi na
ufuatiliaji, Kutoa elimu kwa jamii, kushughulikia pingamizi za kodi ya majengo
kwa wakati na kuendelea kuimarisha uthamini wa majengo” amesema Kichere.
Mh. John Mongella mkuu wa Mkoa wa Mwanza, akizunguza kabla yakumkaribisha Kamishna Mkuu wa TRA kutoa taarifa kwa vyombo vya habari. |
Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa
wa Mwanza, John Mongella, amesema katika kufikia adhma hiyo ya ukusanyaji mapato,
wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa huo hawataruhusiwa kutoka nje ya vituo
vyao vya kazi hadi kuisha kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. “Ajenda yetu kuu ni
kukusanya Mapato, hivyo Ndugu kamishna mimi nikuthibitishie tu kuwa kwa sasa,
hatuta ruhusu Mkurugenzi atoke katika kituo chake cha kazi labda kama amepata
Msiba” amesema Mongella.
Post A Comment: