Meneja wa wakala wa Vipimo mkoa wa Mwanza, Hemed Kipengela, wakati wa Utoaji wa Elimu juu ya Matumizi sahihi ya Mizani mkoani humo. |
Akizungumza na Meneja wa Wakala
wa Vipimo Mkoani Mwanza Bwana Hemed
Kipengele alisema jumla ya mizani 448 tayari imekaguliwa
kutokana na makampuni manne ambayo tayari yamekagulisha mizani yake na imekutwa
ikiwa sahihi ambayo ni ICK (T) LTD
ambao walikuwa a mizani 184, SM HOLDING wenye jumla ya mizani 85 pamoja
na NYANZA COTTON ambao walikuwa na mizani 179. Meneje
aliongezea kuwa zoezi hili la utoaji elimu pamoja na uhakiki wa mizani
itakayotumika kununulia Pamba linaendelea kwa Mikoa yote inayolima Pamba ambayo ni Shinyanga, Simiyu, Geita,
Kagera, Tabora pamoja na Mara.
Bwana Kipengele alisema
wanatarajia kutembelea jumla ya vijiji 101 ambavyo vina jumla ya vituo vya
kuuzia Pamba 150 ili waweze kutoa elimu
na kufanya kaguzi za kushutukize kwa wanunuzi wa Pamba ili kuona kama mizani
waliyopima na ikaonekana ni sahihi itaendelea kununua Pamba ya wakulima kwa
vipimo sahihi.
Meneja Kipengele aliwasihi baadhi ya wakulima wanaolalamikiwa
kuweka maji, kokoto pamoja na mchanga kwenye Pamba kwa ajili ya kuongeza uzito
waache tabia hiyo mara moja sababu Sheria
ya vipimo ipo na inafanyakazi kwa pande zote mbili muuzaji na mnunuzi wote kwa
pamoja hawatakiwi kufanya udanganyifu wowote katika biashara.
Kipengele alisema Sheria ya Vipimo Sura 340
inawataka Wakala wa Vipimo kuhakiki na
kupiga chapa vipimo vyote vinavyotumika katika biashara pia Wakala wa Vipimo imeongeza
na uwekaji wa sticker kwa kipimo kitakachokuwa tayari kimehakikiwa ili iwe rahisi
kwa wakulima kuona na kutambua mizani iliyokaguliwa na kuruhusiwa kwa biashara
kwa mwaka husika.
Alisisitiza kuwa kwa wale
watakaobainika kuchezea mizani kwa ajili
ya kuwaibia wakulima adhabu ni kuanzia laki moja hadi milioni ishirini endapo
mkosaji atakubali kosa, endapo kesi itafikishwa mahakamani na mlalamikiwa
akakutwa kweli alikosa kulingana na ushahidi utakaokuwa umetolewa mshitakiwa
atatozwa faini kuanzia laki tatu hadi milioni hamsini au kifungo cha miaka mitatu
au vyote kwa pamoja. Lengo kuu ni
kumlinda mlaji ili apate faida na thamani ya kile alichozalisha na siyo kupunjwa na wafanyabiashara wajanjawajanja.
Afisa wa Wakala wa Vipimo Daniel Mwakilima, akitoa elimu juu ya Matumizi sahihi na kubaini Mizani iliyo sahihi katika Wilaya ya Magu. |
Tunaimani Tanzania ya viwanda
itafanikiwa endapo Mkulima,
Mfanyabiashara watazingatia matumizi ya vipimo sahihi kuanzia maandalizi ya
shamba, upandaji wa mazao, utumiaji wa pembejeo, uuzaji, usafarishaji, upokeaji
wa mazao, ufungashaji hadi utumiaji wa mazao yenyewe , hivyo vyote vikizingatia
matumizi ya vipimo sahihi viwanda vingi vitaweza kupata malighafi za kutosha
sababu mkulima na mfanyabiashara kila
mtu atakuwa na imani na mwenzake kupitia matumizi ya vipimo sahihi. Msema kweli
na mleta haki katika biashara ni kipimo
sahihi kilichohakikiwa na Wakala wa
Vipimo wala siyo vinginevyo.
Meneja wa wakala wa Vipimo mkoni Mwanza akiendelea kutoa Elimi kwa Wakulima katika Wilayani Magu. |
Post A Comment: