Hatma ya mgogoro wa
watumishi ambao walikuwa na vyeti feki itajulikana mwishoni mwa mwezi wa sita
mara baada ya zoezi la kusikilizwa kwa rufaa kukamilika.
Akizungumza Mkoani
Mwanza juzi na watumishi wa Mkoa wakati wa juma la Utumishi wa Umma, Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Laurian Ndumbaro alisema, hadi kufikia Juni 30, 2017 hatma
ya wale wote waliokuwa na vyeti vya bandia itajulikana mara baada ya kupitia
rufaa zote ambazo ziliwasikishwa ofisini kwake.
“Baada ya uchambuzi
kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa na wahusika, mnamo kesho Juni 30
tutatoa majibu,” alisema.
Ndumbaro alifafanua
kwamba wapo watakaorejeshwa lakini wapo pia ambao uwezekano wa kurejeshwa
hautakuwepo kutokana na ushahidi uliopatikana.
“Lazima tuelewane
katika hili, wapo ambao wao walikuwa na vyeti vya daraja sifuri, wakaenda
wakatengeneza vyeti vyenye dara la pili au la kwanza au latatu, hawa
tulipojaribu kuitisha vyeti vingine kama vya ndoa nk. Ilionekana kutofautina
hawa itabidi watupishe” alisema Ndumbaro.
Aidha aliongeza kamba, “wapo baadhi ambao wao
walipoteza vyeti lakini kwa uvivu hawakutaka kufuatilia Polisi au barazani kwa
ajili yakutapatiwa nakala zingine badala yake wakaenda kutengeneza kwa matokeo
yale yale ya vyeti vyao halisi hawa tutawafikiria kwani dhamira yao ilikuwa sio
kughushi bali walikwepa usumbufu,”
Ndumbaro amesema mara
baada yakukamilika kutolewa kwa taarifa ndipo vibali vya ajira vitatolewa ili
kuweza kuziba nafasi zitakazo kuwa zimebaki wazi, lakini pia kuongezwa kwa
baadhi ya watumishi kulingana na mahitaji kwenye maeneo tofauti tofauti.
”Ni kwamba mara baada
ya zoezi hilo tutakuwa tunahitimisha utumishi hao walikata rufaa na wale
watakaoshindwa wataungana na wale 8000, ili watupishe tufanya taratibu zingine”
alisema Ndumbaro.
Ndumbaro pia aliwaagiza
watumishi wote kuwasilisha taarifa zao sahihi kwa maafisa Utumishi ili waweze
kuzinakilisha kisha kuziweka kwenye mfumo wa kieletroniki.
“Kuna watu Place of Domicile, hazieleweki ni
vema sasa kila mmoja aweke mambo yake sawa nakupeleka taarifa kwa maafisa
utumishi,” alisema.
Sambamba na Maagizo hayo,
Katibu Mkuu huyo amesema kwasasa serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha mfumo
wa (Service Delivery point), ambayo itasaidia kutambua mtumishi mahali alipo, lakini
pia kuyajua majukumu anayoyatekeleza mtumishi husika. Zoezi hili litaanza na
sekta za afya na elimu.
Awali
akisoma taarifa ya Utumishi wa umma katika
mkoa wa Mwanza kwa niaba ya katibu
Tawala wa Mkoa huo Clodwig Mtweve, Katibu Tawala Msaidizi wa uapnde wa Utawala
na rasilimali watu, katika Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Projestus
Rubanzibwa, alisema mkoa huo umeendelea nashughuli za uboreshaji wa shughuli za umma katika Nyanja
mbali mbali ikiwapo Afya na Elimu, ambapo, katika afya Mpango wa malipo kwa
ufanisi (Result Basing Financing), mpango huu ulio anza Mkoani Mwanza Mwezi, Aprili, 2016 ulio na lengo la kuboresha huduma za afya ya
msingi, ambapo kwa upande wa watumishi mazingira ya kazi yameboreshwa kwa
kuwapatia vitendea kazi, ukarabati wa
miundo mbinu ya kutolea huduma na kulipa motisha kwa watumishi wa sekta husika
kwa kuzingatia matokeo ya utendaji kwa vigezo vilivyoanishwa.
Rubanzibwa
amesema “Baada ya tathmini kufanyika
kupitia mpango huu imeonekana
kuwa kumekuwa na ongezeko la ubora wa takwimu kutoka asilimia 43.4 hadi
asilimia 70.7 kwa kipindi cha kuanzia Aprili, 2016 hadi Aprili, 2017”. Aidha amesema
“Kuongezeka kwa morale ya utendaji kazi kwa watumishi kutokana malipo yanaolipwa
kupitia utendaji na ufanisi Ukarabati wa miundo mbinu ya vituo vya kutolea
huduma ambapo ofisi na majengo ya vituo yamekarabatiwa” aliongeza Rubanzibwa.
Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma Laurean Ndumbaro, alipokuwa akiongea na baadhi ya watumishi wa Umma katika mkoa wa Mwanza wakati wa juma la Utumishi wa Umma. |
Akizungumzia
maboresho katika sekta ya elimu, Rubanzibwa amesema Mpango wa Ulipaji kwa
Matokeo umeendelea kutekelezwa kama ulivyokusudiwa, kati ya mwezi Februari na
Aprili, 2017 Wakuu wa Idara za Elimu
Msingi na Sekondari wa Halmashauri
walipatiwa mafunzo juu ya utekelezaji wa mpango huo. Alisema mpango huo
unalenga kuinua utendaji kazi wa walimu wanaofundisha darasani pamoja na
wanafunzi ili kuwezesha kusawazisha ikama (Pupil Teacher’s Ratio) kwa kulipa
gharama za uhamisho kwa walimu wanaohamishwa kwenda kujaza ikama katika shule
zenye upungufu.
Lakini
pia kuboresha miundo mbinu kwa kufanya ukarabati wa madarasa na ujenzi wa
matundu ya vyoo kutoa motisha kwa wanafunzi na walimu wanaofanya vizuri katika
matokeo ya mitihani mbalimbali ya kitaifa.
Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Halmashauri zake nane (8) kwa taarifa za Mwezi
Aprili, 2017 zina jumla ya watumishi 25,734
Kati ya hao watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa ni 632 na watumishi wa Halmashauri ni 24,742.
Post A Comment: