Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amewataka vijana wanamichezo wa UMITASHUMTA na UMISETA pamoja na walimu wao kujizatiti katika suala zima la taaluma mara baada yakufanya vizuri katika michezo hiyo iliyo malizika mkoani hapa kwa mwaka huu wa 2017 na mkoa huo kuibuka mshinda wa kwanza na wapili.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, akipokea kikombe cha Ushindi wa Jumla kutoka kwa Mwanafunzi Chausiku Bahati aliyekabidhi kikombe hicho kwa niaba ya wenzake walioshinda UMITASHUMTA. |
Mongella ameyasema hayo wakati
alipokuwa akiipokea timu ya mkoa wake ya UMITASHUMTA iliyo ibuka mshindi wa jumla mara baada
yakumalizika kwa michezo hiyo iliyoshikisha mikoa ishirini na sita (26) ya
Tanzania bara.
Ameongeza kuwa, ili Michezo waliyo shinda
iwe na maana, hawana budi kujizatiti katika taaluma “Nichukue fursa hii
kuwaelekeza kwamba nguvu hii na mshikamano huu ambao tumeuonesha katika michezo
uende mbele zaidi, tukajizatiti kwenye masomo, ili tuwe wakwanza katika kila
nyanja” alisema Mongella na kuongeza kuwa, yupo tayari kushirikiana nao bega
kwa bega katika kuhakikisha mkoa huo unakuwa wa mfano wakuigwa katika sekta
zote.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa amemuagiza
Afisa Elimu wa mkoa huo, Michael Ligola, kumpatia orodha ya wanafunzi wote
walishiriki na kutwaa ubingwa huo ili waweze kuingizwa katika mipango ya mkoa.
Awali akitoa maelezo ya utangulizi,
Afisa Elimu wa mkoa wa Mwanza, amesema, kumalizika kwa mashindano hayo ndio
mwanzo wa mashindano yajayo sambamba na taaluma. “Mh. Mkuu wa Mkoa, tuliona
mara baada yakumalizika kwa mashindano haya sio vizuri waondoke bila kupata
maneno ya nasaha kutoka kwako hususan ni katika suala zima la taaluma”
Kwa mujibu wa taarifa ilisomwa
mbele ya mkuu wa mkoa na Afisa Elimu Msingi kutoka Wilaya ya Misungwi, Ephrahim
Majinge, mkoa wa Mwanza umefanikiwa kuwa mshindi wa jumla kwa upande wa
UMITASHUMTA kwa michezo yote, huku ukitwaa vikombe vya Soka wanaume, mshindi wa
kwanza, Mpira wa mikono mshindi wa kwanza na Riadha mshindi wa kwanza kitaifa,
michezo mingine ni Netball mshindi wa kwanza kitaifa, sambamba na mkoa kushika
nafasi ya pili kwa michezo ya Wavu na mpira wa mikono.
Aidha kwa upande wa UMISETA, mkoa
wa Mwanza, umeshika nafasi ya pili kitaifa kwa kutwaa vikombe vipatavyo sita kutoka
michezo tofauti tofauti, iliyoshikisha timu 28 za mikoa Tanzania bara na
Zanzibar.
Mkoa wa mwanza umekuwa mwenyeji wa
michezo hiyo kwa mwaka wa 2017, ambapo katika ufunguzi wa michezo hiyo, ulifanywa
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan
kwa upande wa UMISETA na kwa upande wa UMITASHUMTA yalifunguliwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene (MB) na kufungwa Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.
Post A Comment: