Sheik Hassan Kabeke, Mwenyekiti mwenza wa Kamati ya Amani ya mkoa wa Mwanza, akifafanua umuhimu wa mazingira kwa Waandishi wa habari |
Dkt. Charles Mlingwa Mkuu wa mkoa wa Mara akifungua warsha hiyo ya Viongozi wa Dini, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa ya kanda ya Ziwa. |
Akifungua
Semina ya siku moja mkoani hapa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, na risala
yake kusomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, Mongella amesema, viongozi
wa dini wanalo jukumu kubwa kwani wao husimamia imani za watu. “Ninyi Viongozi
wa dini dhima mliyonayo ndani ya jamii ni kubwa sana na chochote mtakacho
waelekeza waumini wenu lazima waweze kukitekeleza, hivyo niwaombe sana viongozi
wangu tulilinde ziwa viktoria kwa jitihada zetu zote’’ alisema Mongella.
Aidha
Mongella amesema kuwa, kuwepo kwa
Ziwa Victoria ni fursa ya uendelezaji ya kauli mbiu ya “Tanzania ya Viwanda” ambayo Serikali ya awamu ya Tano
inasisitiza, “Ziwa hili linasaidia upatikanaji wa rasilimali
zinazotumika kwa matumizi ya nyumbani na viwandani, usafiri na usafirishaji na
uzalishaji wa nishati ya umeme Hivyo basi
hatuna budi kuhifadhi mazingira ya Ziwa na Bonde lake”
amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
Kwa
upande wao, viongozi wa dini wakiongea wamesema, wao wanatambua na hata vitabu
vya dini vinaelekeza juu ya mwanadamu anachopaswa kufanya katika kulinda
mazingira ikiwepo ziwa Viktoria.
Mwenyekiti
mwenza wa Kamati ya amani ya madhehebu ya dini katika Mkoa wa Mwanza, Sheik
Hassan Kabeke, amesema katika Uislam na
hususan ni katika mafundisho ya Mtume Muhama S.A.W, inafafanua juu ya mito miwili yaani mto Nile
na Furabu ambayo mtume aliipitia huku akisema kwamba, Mto Nile ambao
unafungamanishwa na Ziwa Viktoria Mtume amesisitiza kuyatunza mazingira, “Katika
kupanda miti kwenye uislamu mtu hupata thawabu, tunaimani kabisa kwamba kila
mmoja wetu akitunza mazingira ni sehemu ya Ibada, amesema Kabeke.
Naye
Baba Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki la Musoma, kwa upande wake
amesema kwa habari ya mazingira, tunaona ni jukumu la jamii nzima bila kujali
itikadi zetu “ Kukutana kwetu hapa tunataka kuangalia nikwa namna gani
tutaziangazia sababu za kiuchumi na kijamii, alisema Msonganzila na kuongeza
kwamba kwa sasa wao katika Mkoa wa Mara wanayo kampeni kwenye eneo la Serengeti
ambayo wanaendelea kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa Utunzaji wa mazingira na
mabadiliko ya hali ya nchi.
Mradi wa Hifadhi ya Mazingira wa Ziwa Victoria
(LVEMP II) utakamilika mwezi Disemba, 2017, aidha warsha hiyo ni kati ya warsha nne zilizoandaliwa na Mradi
kwa madhumuni ya kukusanya maoni ya wadau ambayo yatawezesha kuandaa awamu
ijayo ya Mradi inayotarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2018.
Kikao hicho
kimewakutanisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na Viongozi wa
dini kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera, Simiyu na Mara
Post A Comment: