Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema kukwama kwa mpango wa Milenia yaani Millennium Development Goals (MDGs), nikutokana na mpango huo kutoshirikisha serikali za Mitaa kikamilifu.


Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akifungua Semina hiyo ya Uaandaaji wa Mpango Mkakati

Mpango mkakati mara baada ya uzinduzi


Baadhi ya washiriki wakiwa wanamsikiliza kwa umakini mtoa mada wakati wasemina hiyo ya uandaji mpango Mkakati
Akizungumza  mkoani hapa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, wakati wa ufunguzi wa semina ya siku mbili juu ya uaandaji wa mipango mikakati ya Mikoa na  Halmashauri kwa Halmashauri zilizopo kwenye mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu.
Akifunua kikao hicho cha siku mbili, Mongella alisema, utafiti uliofanywa kwa miaka 15 ya utekelezaji wa mpango, haukufika katika ngazi za chini za utawala wa nchi hivyo kupelekea kusuasua kwa mipango mikakati. “ tulikuwa na tatizo la Localization”alisema Mongella.
Hata hivyo Mongella, amewashukuru ESRF kwa juhudi wanazo chukua hivi sasa katika kuwajengea uwezo wataalam wa mipango na uratibu kutoka katika mikoa na halmashauri, hususan katika zama mpya za Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs) yaani “Localization of SDGs’’, nakuwataka wawezeshaji hao kuyapeleka mafunzo hayo
kwenye maeneo mengine ya nchi.
 
 
Awali akizutoa maneno ya utangulizi kabla yakumkaribisha Mkuu wa Mkoa kufungua warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya tafiti za kiuchumi na kijamii (ESRF) Dkt. Tausi Mbaga Kida, alisema Matokeo ya washa hizo pamoja na mambo mengine zilionesha pengo kubwa la uelewa na ujumuishaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu,  kwenda sambamba pamoja na mikakati mingine ya kitaifa kama vile Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (5YDPII) katika mipango ya wilaya, lakini pia ilibainisha kwamba, wilaya nyingi hapa nchini hazikuwa mipango mkakati na zile zilizokuwa nayo pia ilibainika mipango hiyo, ama haikutengenezwa kitaalamu au ilikuwa imepitwa na wakati.
Dkt. Tausi  amesema baadhi ya mada ambazo zitawasilishwa  zikifatiliwa na washiriki kwa umakini zitakuwa ni msaada mkubwa kuwa ni pamoja na Maelezo ya jumla kuhusu mpango mkakati, upangaji wa bajeti, ufuatiliaji na namna ya kutoa taarifa, mada zingine ni Mikakati ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa SDGs, FYDP II, Africa Agenda 2063, Vision 2025 kwakutaja baadhi”, alisema Dkt. Tausi lakini pia Mchakato wa kuandaa mpango mkakati Ufuatiliaji, upimaji, na utoaji wa taarifa (reporting, monitoring and evaluation).
Warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika katika Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza imeandaliwa na taasisi ya tafiti za kiuchumi na kijamii na kuwashirikisha Makatibu Tawala wa mikoa, wakurugenzi na maafisa mipango kutoka mikoa ya Mwanza, Simiyu na Mara kwa ngazi ya halmashauri mikoa.
 
 
Axact

Post A Comment: