Jumla ya mizani 3,070 Iliyo Hakikiwa katika mikoa ya kanda ya ziwa kwa ajili ya matayarisho ya ununuzi wa pamba kwa msimu wa 2017/2018 imekutwa salama mara baada ya kuhakikiwa na wakala wa Vipimo nchini.
Ameongeza kuwa, katika maandalizi ya msimu mpya wa ununuzi wa Pamba zaidi ya mizani 1,402 imekaguliwa katika mkoa wa Shinyanga, mkoa wa Simiyu wamekagua zaidi ya mizani 302, mkoa wa Geita jumla ya mizani 40 tayari imekaguliwa, ilihali katika mkoa wa Mwanza wamekagua mizani 448, mkoa wa Mara mizani 690, mkoa wa Tabora wamekagua mizani 164 pamoja na mkoa wa Kagera wamekagua jumla ya mizani 24 ikiwa ni maandalizi ya ununuzi wa zao la Pamba.
Afisa wa Vipimo Mkoani Kagera akitoa elimu na kuwaonesha wakulima mizani iliyo hakikiwa |
Afisa wa Vipimo Mkoani Kagera akitoa elimu na kuwaonesha wakulima mizani iliyo hakikiwa |
Akizungumza nami Jijini Mwanza, kaimu Meneja Sehemu ya Elimu, Habari na Mawasiliano Bi. Irene John, amesema, Wakala wa vipimo Tanzania ( WMA) chini ya usimamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeendelea kutoa elimu kwa wakulima pamoja na kuhakiki mizani itakayotumika kununulia zao la Pamba ikiwa ni maandalizi ya msimu wa ununuzi wa Pamba kwa mwaka huu.
Maafisa wa Vipimo wakitoa elimu mkoani Shinyanga |
Bi. Irene amesema, Dhumuni kuu la utoaji elimu kwa wakulima wa zao la Pamba Kanda ya Ziwa ni kuwawezesha wakulima kutambua mizani iliyosahihi (inayoruhusiwa kwa biashara) na ile iliyochezewa (isiyoruhusiwa kwa biashara) ili waweze kujilinda wenyewe pindi maafisa vipimo wanapokuwa hawapo katika vituo vya kuuzia Pamba yao, lakini pia ni kuwawezesha wakulima kupata faida ya thamani kamili ya jasho lao.
Afisa wa Vipimo Mkoani Kagera akitoa elimu na kuwaonesha wakulima mizani iliyo hakikiwa |
Ameongeza kuwa, katika maandalizi ya msimu mpya wa ununuzi wa Pamba zaidi ya mizani 1,402 imekaguliwa katika mkoa wa Shinyanga, mkoa wa Simiyu wamekagua zaidi ya mizani 302, mkoa wa Geita jumla ya mizani 40 tayari imekaguliwa, ilihali katika mkoa wa Mwanza wamekagua mizani 448, mkoa wa Mara mizani 690, mkoa wa Tabora wamekagua mizani 164 pamoja na mkoa wa Kagera wamekagua jumla ya mizani 24 ikiwa ni maandalizi ya ununuzi wa zao la Pamba.
Katika hatua nyingine Irene amesema, sheria ya Vipimo Sura 340 inawataka Wakala wa
Vipimo kuhakiki na kupiga chapa vipimo
vyote vinavyotumika katika biashara ikiwa ni pamoja na kuweka
sticker kwa kipimo
kitakachokuwa tayari kimehakikiwa na kukutwa kikiwa sahihi ili iwe rahisi kwa wakulima kuona na kutambua
mizani iliyokaguliwa na kuruhusiwa kwa biashara kwa mwaka husika.
Meneja wa wakala wa Vipimo mkoani Mwanza akitoa elimu kwa Wakulima na wafanya Biashara. |
“Wakala wa Vipimo nchini itaendelea kufanya
ukaguzi wa kushtukiza wakati wowote baada ya msimu wa ununuzi wa Pamba kuanza ili
panapokuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu uonevu katika mizani yaweze
kutatuliwa wa haraka” amesema Irene
Aidha
amewataka wakulima wanaolalamikiwa kuweka maji, kokoto pamoja na mchanga kwenye Pamba kwa ajili ya kuongeza
uzito waache tabia hiyo mara moja sababu
Sheria ya vipimo ipo na inafanyakazi kwa pande zote mbili muuzaji na mnunuzi
wote kwa pamoja hawatakiwi kufanya udanganyifu wowote katika biashara.
Bi
Irene hakusita kutaja faini itakayotozwa kwa wote watakao banika kufanya
udanganyifu “faini itaanzia laki moja badala ya elfu kumi kama ilivyo zoeleka hadi
milioni ishirini endapo mkosaji atakubali kosa, endapo kesi itafikishwa
mahakamani na mlalamikiwa akakutwa kweli alikosa kulingana na ushahidi
utakaokuwa umetolewa “ na kusema “mshitakiwa atatozwa faini kuanzia laki tatu
hadi milioni hamsini au kifungo cha miaka mitatu au vyote kwa pamoja”.
Irene
alisema Tanzania ya viwanda itafanikiwa endapo Mkulima, Mfanyabiashara watazingatia
matumizi ya vipimo sahihi kuanzia maandalizi ya shamba, upandaji wa mazao,
utumiaji wa pembejeo, uuzaji, usafarishaji, upokeaji wa mazao, ufungashaji hadi
utumiaji wa mazao yenyewe.
Afisa wa Vipimo Mkoani Kagera akitoa elimu na kuwaonesha wakulima mizani iliyo hakikiwa |
Wakala wa Vipimo itaendelea kutoa elimu
kwa wakulima na wafanyabiashara ili
wajue thamani ya kuuza kwa kutumia mizani iliyohakikiwa na Wakala wa Vipimo
ikiwa ni pamoja na kumsaidia mkulima kupata fedha kulingana na thamani ya mazao
yake, kufanya biashara ya haki na kuepusha migogoro/migongano, kukuza uchumi wa
mkulima mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla
Bi. Irene alisema "elimu kwa pande zote mbili
(Mkulima na Mfanyabiashara) ni muhimu
lakini zaidi kwa mkulima kwani, mbali ya
kutumia muda wake mwingi katika kuandaa shamba, kulima, kupalilia na hata
kuvuna bado ameoneka kuwa mnyonge kwenye mazao yake ndiyo maana kwa sasa tunazunguka Kanda ya Ziwa mikoa
inayolima Pamba kwa wanunuzi na wakulima kwa ajili ya kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mizani kabla ya uuzaji
wa zao la Pamba kuanza.
Afisa huyo amesema
kuanzia hatua ya awali ya kuandaa shamba hadi kuvuna mkulima anahitaji matumizi
sahihi ya vipimo lakini wakati wa kuuza
mazao, umakini wa matumizi sahihi ya
vipimo unahitajika sana, ambapo kipimo kikiwa sahihi na kikatumiwa kwa usahihi,
kitatoa matokeo sahihi kumwezesha muuzaji (mkulima) kupata fedha sawa na
thamani ya bidhaa aliyouza.
Hivyo, nia na lengo la utoaji wa elimu pamoja
na uhakiki mizani ni kuwasaidia wakulima kabla ya
msimu wa Pamba kuanza wapate elimu ya kutosha hatimaye mkulima aweze kupata fedha kulingana na
thamani ya bidhaa atakayoizalisha na kuwasilisha sokoni. “Mwaka huu
tutajitahidi kuongeza elimu zaidi kwa wakulima ikiwa ni pamoja na kuongeza
kaguzi za kushutukiza ili kuwadhibiti
baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kuchezea mizani kwa lengo la kuwaibia
wakulima” alisema Kaimu Meneja Bi Irene.
Post A Comment: