Serikali imesema ni marufuku kwa shule ambayo itakuwa haina viwanja vya michezo kupatiwa kibali cha kufungua shule ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mashindano ya kwashule za msingi nchini UMITASHUMTA mkoani Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMO) Mh. George Simbachawene, amemuagiza Kamishna wa Elimu nchini, kutozipatia vibali shule zinazo hitaji kufunguliwa endapo zitakuwa hazina viwanja vya michezo.
Simbachawene, amesema kutokana na sheria ya Elimu
namba 25 ya mwaka 1978, ambayo inataka kila shule inapofunguliwa lazima iwe na
viwanja visivyo pungua vitano hivyo nilazima hili lizingatiwe, “nichukue nafasi
hii kumuagiza kamishna wa Elimu kuanzia sasa asisajili shule yeyote ile ambayo
itakuwa haina Viwanja vya michezo, kwani bila kufanya hivyo azma yetu yakuinua
michezo nchini haiwezi kutimia” alisema.
Mbali na kutoa maagizo hayo waziri Simbachawene,
ameziagiza pia halmashauri na wilaya kote nchini kutenga sehemu ya mapato yao
ya ndani kwaajili ya kitengo cha michezo,
huku akizihimiza kuweka katika bajeti ijayo ya serikali fedha kwenye vifungu
vinavyo husiana na michezo na kuonya kuwa endapo Halmashauri itashindwa kufanya
hivyo basi yeye kama waziri mwenye dhamana hatakubali ipite.
Amesema Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015
sehemu ya (61) inatambua suala la Michezo lakini pia Sera ya Elimu ya Mwaka
1995, hivyo kama Serikali lazima waweke kipaumbele katika suala zima la michezo.
Ameongeza kuwa, Msingi wa Michezo nchini ni michezo
ya UMITASHUMTA NA UMISETA ndio Dira ya timu zetu za Taifa, “Tukiwaandaa vijana
wetu vizuri na kutokana kaulimbiu hii ya masula ya viwanda, hatuna wasiwasi
kuwa hawa ndio viwanda vyenyewe, mchezaji mmoja aliyefikia viwango vya
kimataifa huweza kugharamia hata bajeti ya nchi” alisema Simbachawene.
Katika hatua nyingine Simbachawene, amewaagiza
makatibu Tawala kote nchini, kusimamia suala la taaluma na michezo, amesema
hakuna taaluma bila Michezo na Hakuna michezo bila Taaluma kwa mantiki hiyo
lazima nidhamu ya hali ya juu iongezwe miongoni mwa vijana na wanamichezo kwa
ujumla.
Naye Mkurugenzi wa Michezo nchini kutoka Wizara ya
Habari, Michezo Sanaa na Wasanii Dkt. Yusuph Singo amesema Tayari Wadau Mbali
mbali wa Michezo wakiongozwa na Chama cha Mpira wa Miguu na Riadha wapo Mkoani
Mwanza kwaajili ya Kuangalia Vipaji kwa ajili ya Timu mbali mbali za Taifa
lakini pia vilabu vyao.
Aidha amesema kuwa wizara ipo katika Mazungumzo na
Timu Manchester City kupitia wakala wao wa TECHNO kwaajili yakuchukuwa Vijana
wapatao kumi kutoka Tanzania kwaajili yakuwaendeleza kimichezo.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa
Mwanza John Mongella, aliishukuru serikali kwakuichagua Mwanza kuwa mwenyeji wa
mashindano hayo huku akiomba kwa mwaka ujao mashindano hayo kufanyika tena mkoani
humo, kutokana na madhari mazuri lakini pia ubora wa viwanja na hali ya ulinzi
na usalama inayotamalaki katika mkoa huo, “Mh. Waziri mimi niombe tu, haya
mashindando katika mwaka ujao myalete tena Mwanza sisi tupo tayari, huo ndio
mtazamo wangu lakini pia wenzangu wataniunga mkono” alisema Mongella.
Mashindano ya shule za msingi (UMITASHUMTA) ya 2017 ni
mashindano ya 22 ambapo yanashirikisha wanamichezo wapatao 2522 kutoka mikoa 26
ya Tanzania Bara.
Post A Comment: