WACHAZAJI WA MADRID HAPA WAKIPONGEZANA BAADA YA ROLNARDO KUTUPIA GOLI. |
Ni katika Kombe la Ulaya.
Ronaldo na Bale washerekea ushindi dhidi ya Schalke
04
Mchezaji bora duniani mwaka huu Cristiano Ronaldo Gareth Bale
na Karim Benzima walifunga mabao mawili kila mmoja na kuisaidia Real Madrid ya
uhispania kufuzu kwenye robo fainali ya kombe la mabingwa barani ulaya baada ya
kuinyeshea Schalke 04 ya Ujerumani mabao 6-1 katika mkondo wa kwanza uliosakatwa
huko Ujerumani.
Benzima ndiye aliyefungua kivuno hicho cha mabao baada ya nipe nikupe kunako
dakika ya 13.
Mchezaji aliyeigharimu Madrid kitita kikubwa zaidi msimu huu Gareth Bale
akafanya mambo kuwa mawili bila dakika saba baadaye .

Ronaldo alimpangua Joel Matip kwa miondoko ya aina yake na kufunga la tatu
akimwacha kipa wa Schalke Fahrmann asijue azibe wapi azue wapi.
Masaibu ya wenyeji hao yaliongezeka Karim Benzema alipofuma bao la nne .
Bale akaongezea bao la tano kisha nyota wa Ureno Ronaldo akafunga kiziba
mkonga na kudidimiza kabisa mtumaini ya timu ya tatu ya Ujerumani baada ya
mabingwa Bayern Munich na washindi wa pili Borussia Dortmund kusonga mbele
katika hatua ya robo fainali ya mchuano huo msimu huu.
Uchungu uliwazidi mashabiki wa nyumbani na wachache waliosalia uwanjani
walishuhudia bao la kukata na shoka la nyota wao Klaas-Jan Huntelaar .
Hata hivyo bao hilo la kufutia machozi la dakika ya mwisho ya mechi haitakuwa na faida mbali na kunusuru hadhi ya kocha Jens Keller Schalke itakapozuru bernabou baada ya majuma mawili kwa mkondo wa pili.
Fernando Torres asherekea bao lake
Katika mechi nyingine iliyosakatwa usiku wa jana huko Instabul,Uturuki
,matumaini ya pekee ya timu ya Uingereza kusonga mbele katika hatua ya robo
fainali yalitegemea matokeo baina ya wenyeji Galatasaray na Chelsea .
Matokeo ya mkondo wa Kwanza
- Barcelona 2-0 Man City
- Paris St-Germain 4-0 Bayer Leverkusen
- Atletico Madrid 1-0 AC Milan
- Bayern Munich 2-0 Arsenal
- Manchester United 0-2 Olympiakos
- Borussia Dortmund 4-2 Zenit St Petersburg
- Chelsea 1-1 Galatasaray
- Real Madrid 6-1 Schalke
Kwa kila hali na mizani mechi hii ilitarajiwa kuwa ngumu kwa Galatasaray
chini ya kocha wa zamani wa Manchester city Roberto Mancini ikiongozwa na
aliyekuwa mshambulizi wa Chelsea Didier Drogba na Emmanuel Ebue zamani
akiichezea Arsenal ilikuwa inakabiliana na The Blues chini ya Kocha Jose
Mourinho .
Uwanjani mashabiki wa nyumbani walinyamazishwa na bao la dakika ya 9 ya
kipindi cha kwanza iliyofungwa na Fernando Torres.
Roberto Mancini alilazimika kufanya badiliko la mapema ilikuzia kuabishwa na
wimbi la mashabulizi ya vijana wa Mourinho .
Katika kipindi cha pili juhudi za Galatasaray kujinasua zilizaa matunda
Aurelien Chedjou alifunga bao la kusawazisha baada ya kutumia vyema mpira wa
kona uliomchanganya Peter Cech .
Bao hilo ndilo litakaloamua mshindi baina ya timu hizo mbili zitakapokutana
katika mechi ya mkondo wa pili tarehe 18 mwezi Machi huko Stamford Bridge
Post A Comment: