HUYU NDIYE JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA |
________________
UTANGULIZI
Mheshimiwa Mwenyekiti na
Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,
Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,
1. Kwa mujibu wa kifungu 20 (3) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya
83 na Tangazo la Serikali Na. 30 la tarehe 14 Februari, 2014, naomba
kuwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum la Katiba. Rasimu ya Katiba
ninayoiwasilisha imeandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya
kukamilisha kazi ya kuratibu, kukusanya, kuchambua na kutathmini maoni ya
wananchi kuhusu Katiba Mpya.
2. Mwanzo kabisa, nieleze kwamba, Maelezo haya ninayoyatoa, ni sehemu ya
Randama (Memorandum) iliyoandaliwa na Tume kwa lengo la kufafanua kwa kina,
maudhui ya kila Ibara iliyomo katika Rasimu ya Katiba na sababu za mapendekezo
ya Ibara hizo. Hivyo, naomba maelezo yote yaliyomo katika Randama yawe sehemu
ya maelezo yangu na yaingizwe katika kumbukumbu za Bunge hili.
3. Rasimu ya Katiba ni miongoni mwa Nyaraka zilizoambatanishwa katika
Ripoti ya Tume kuhusu Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania tuliyowakabidhi Waheshimiwa Marais tarehe 30 Desemba, 2013. Nyaraka
nyingine ni:
(a) Taarifa ya Maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko ya Katiba. Taarifa hii
ina maoni ya Wananchi kuhusu maeneo mbalimbali ya kikatiba ambayo ndio msingi
wa uandishi wa Rasimu ya Katiba;
(b) Taarifa ya Mabaraza ya Katiba ambayo inaainisha maoni ya Wananchi
kuhusu Ibara zilizokuwemo katika Toleo la Kwanza la Rasimu ya Katiba na jinsi
zilivyofanyiwa kazi;
(c) Taarifa ya maoni ya Wananchi kuhusu Sera, Sheria na Utekelezaji.
Taarifa hii ina maoni ya wananchi kuhusu mambo ambayo yanahitaji kufanyiwa
uamuzi wa kisera, kutunga au kurekebisha sheria zilizopo au utekelezaji wa
kiutendaji;
(d) Taarifa ya Utafiti Kuhusu Masuala Mbalimbali ya Kikatiba, ambayo ina
taarifa nne ambazo ni:
(i) Utafiti Kuhusu Madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(ii) Utafiti Kuhusu Maadili ya Viongozi na Uwajibikaji;
(iii) Utafiti Kuhusu Masuala Yanayohusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar; na
(iv) Ushauri Elekezi Kuhusu Mifumo ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi, Tanzania (Final Report on the Review of Various Aspects of Electoral Systems and the Electoral Commission in Tanzania).
(ii) Utafiti Kuhusu Maadili ya Viongozi na Uwajibikaji;
(iii) Utafiti Kuhusu Masuala Yanayohusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar; na
(iv) Ushauri Elekezi Kuhusu Mifumo ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi, Tanzania (Final Report on the Review of Various Aspects of Electoral Systems and the Electoral Commission in Tanzania).
(e) Taarifa ya Takwimu za Ukusanyaji wa maoni ya Wananchi ambayo inaainisha
maeneo makuu yaliyotolewa maoni, jinsi, elimu na kazi za watoaji maoni; na
(f) Viambatisho vya Ripoti ambavyo vinaainisha hatua mbalimbali za
mchakato, uamuzi, hotuba za viongozi na miongozo mbalimbali iliyotolewa na
Tume.
4. Ripoti ya Tume na baadhi ya Taarifa zimegawiwa kwa kila Mjumbe na
Taarifa nyingine zimewekwa katika Maktaba ya Bunge ili kuwawezesha Wajumbe
kufanya marejeo. Tume inaamini kwamba Ripoti na Taarifa zinazowasilishwa pamoja
na maelezo haya zitawasaidia Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kujadili na
kufanya uamuzi sahihi kwa kila Ibara iliyopendekezwa kwa kuzingatia maslahi ya
wananchi na Taifa kwa jumla.
Shukrani kwa Uteuzi na Kuchaguliwa
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Mheshimiwa Mwenyekiti,
5. Naomba kutumia fursa hii, kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa
kuiwezesha Tume kukamilisha kazi ya kuandaa Rasimu ya Katiba na kuiwasilisha
katika Bunge lako.
6. Mwenyezi Mungu alitulinda katika mchakato mzima wa kuratibu na kukusanya
maoni ya wananchi hadi kukamilisha kazi ya kuandaa Rasimu. Kwa huzuni kubwa
tulimpoteza mmoja wetu, Dkt. Adrian Sengondo Mvungi katika hatua za mwisho za
kazi yetu. Mchango wa Dkt. Mvungi ulikuwa mkubwa sana na ingawa hatuko naye,
Rasimu ya Katiba ninayoiwasilisha imesheheni maoni yake mengi. Kazi ya Mungu
haina makosa na tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema
peponi.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Mheshimiwa Mwenyekiti,
7. Napenda kukupongeza wewe mwenyewe na Makamu wako kwa kuchaguliwa kwenu
ili kuongoza Bunge hili ambalo lina jukumu kubwa la kujadili na kupitisha
masharti ya Rasimu ya Katiba iliyotokana na maoni ya wananchi. Bunge hili
Maalum la Katiba litapendekeza Katiba Mpya itakayopigiwa kura ya maoni na
wananchi. Kuchaguliwa kwenu ni ishara ya imani kubwa waliyonayo wajumbe wa
Bunge Maalum juu yenu. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awawezeshe kuifanya kazi
hiyo kwa weledi, hekima, busara, uzalendo na uadilifu mkubwa ili kukamilisha
jukumu la Bunge Maalum la Katiba. Tunawapongeza pia wajumbe wote wa Bunge
Maalum la Katiba na tunawatakia kila la kheri katika kutimiza jukumu ambalo
taifa limewakabidhi.
Shukrani kwa Marais, Watendaji
Mheshimiwa Mwenyekiti,
8. Kwa niaba ya Wajumbe, na Watumishi wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa niaba yangu mwenyewe, ninawashukuru kwa dhati kabisa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohammed Shein, kwa mambo yafuatayo:
Mheshimiwa Mwenyekiti,
8. Kwa niaba ya Wajumbe, na Watumishi wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa niaba yangu mwenyewe, ninawashukuru kwa dhati kabisa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohammed Shein, kwa mambo yafuatayo:
· Kwanza, kwa uamuzi wao wa busara wa
kusikiliza matakwa ya Wananchi ya kutaka Katiba Mpya.
· Pili, kwa kututeua kuwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kutuwezesha kuifanya na kuikamilisha kazi ya kuandaa Rasimu ya Katiba kwa wakati uliowekwa kisheria.
· Tatu, kwa kuipatia Tume, Watumishi wa Sekretarieti walio makini, wenye ujuzi, utaalamu na uelewa katika fani zao walioiwezesha Tume kukamilisha kazi yake kwa ufanisi.
· Nne kuheshimu, kuisimamia na kuipa Tume nyenzo za kutekeleza majukumu yake kwa uwazi na bila ya kuiingilia.
· Mwisho kwa mujibu wa sheria, kuunda Bunge Maalum la Katiba lililojaa wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali ya jamii za watanzania.
· Pili, kwa kututeua kuwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kutuwezesha kuifanya na kuikamilisha kazi ya kuandaa Rasimu ya Katiba kwa wakati uliowekwa kisheria.
· Tatu, kwa kuipatia Tume, Watumishi wa Sekretarieti walio makini, wenye ujuzi, utaalamu na uelewa katika fani zao walioiwezesha Tume kukamilisha kazi yake kwa ufanisi.
· Nne kuheshimu, kuisimamia na kuipa Tume nyenzo za kutekeleza majukumu yake kwa uwazi na bila ya kuiingilia.
· Mwisho kwa mujibu wa sheria, kuunda Bunge Maalum la Katiba lililojaa wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali ya jamii za watanzania.
9. Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Mawaziri wa Katiba na Sheria wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar; Wanasheria Wakuu wa Serikali; Makatibu Wakuu Viongozi, Watendaji
Wakuu wa Wizara za Katiba na Sheria; Wakuu wa Mikoa; Wakuu wa Wilaya;
Wakurugenzi na Makatibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Watendaji wa Tarafa,
Kata, Shehia,
Vijiji na Mitaa kwa ushirikiano mzuri waliotoa kwa Tume wakati wote wa
mchakato wa kupata maoni ya wananchi.
10. Tume pia inatoa shukrani maalum kwa Jeshi la Polisi la Tanzania na
vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kwa kuhakikisha mchakato mzima unaenda kwa
usalama. Aidha, Tume inatoa shukrani kwa Vyama vya Siasa, Jumuiya za Kidini,
Asasi za Kiraia, Vyombo vya Habari, Taasisi na Makundi mengine kwa mchango wao
mkubwa wakati wote wa mchakato wa kupata maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya.
Shukrani kwa Wananchi
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Mheshimiwa Mwenyekiti,
11. Kwa namna na kwa uzito wa pekee, Tume inawashukuru sana Wananchi wote
kwa ushiriki, na kwa mchango wao mkubwa wa mawazo, maoni na mapendekezo
yaliyowezesha kupatikana kwa Rasimu ya Katiba. Hii ni mara ya kwanza katika
historia ya nchi yetu, kwa wananchi wa kawaida kushiriki katika kutoa maoni kwa
uhuru na uwazi kuhusu aina ya katiba wanayoitaka, na wamefanya hivyo kwa wingi,
uhuru, uwazi, umakini na kwa uzito unaostahili.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
12. Baada ya kutoa shukrani sasa naomba nitoe maelezo marefu kidogo kuhusu
Rasimu ya Katiba. Maeneo yote ya Rasimu ni muhimu lakini kwanza nitayazungumzia
machache kwa ujumla kutokana na umuhimu wake. Baadaye nitaizungumzia Rasimu ya
Katiba kwa kupitia maudhui ya kila Sura. Maelezo kwa kina ya kila Ibara na
sababu za mapendekezo zinaelezwa kwenye Randama
6
ambayo tayari imekabidhiwa kwa Katibu wa Bunge Maalum la Katiba na wabunge wote watapata nakala.
Dhana ya Katiba
6
ambayo tayari imekabidhiwa kwa Katibu wa Bunge Maalum la Katiba na wabunge wote watapata nakala.
Dhana ya Katiba
Mheshimiwa Mwenyekiti,
13. Katika nchi yoyote, msingi wa uendeshaji wa nchi unategemea Katiba.
Katiba ni sheria kuu au sheria mama katika nchi yoyote. Sheria nyingine zote
zinategemea au zinatungwa kwa mujibu wa Katiba. Wakati mwingine Katiba
hutafsiriwa kuwa ni mkataba wa Kijamii kati ya Viongozi na Wananchi. Ni
makubaliano ya wananchi kuhusu utaratibu na kanuni za uendeshaji wa mambo
mbalimbali katika nchi yao. Katiba ni muafaka wa kitaifa juu ya misingi mikuu
ya kuendesha nchi.
14. Katiba ni Sheria ya msingi ambayo inaweka mfumo wa uendeshaji wa nchi.
Katiba inafanya hivyo kwa kuainisha misingi ya taifa, mgawanyo wa madaraka na
majukumu ya mihimili mikuu ya dola, usimamizi wake, mgawanyo na ukomo wa
mamlaka ya vyombo mbalimbali vya dola.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Mheshimiwa Mwenyekiti,
15. Katika nchi ambazo zimefanya mabadiliko ya katiba, njia kuu zifuatazo
huwa zinatumika:
(i) Rais kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya kikatiba;
(ii) Kuundwa Tume ya kuandaa Katiba kwa kupitia sheria zilizopo; na
(iii) Bunge kutunga sheria maalum ya mabadiliko ya Katiba.
(ii) Kuundwa Tume ya kuandaa Katiba kwa kupitia sheria zilizopo; na
(iii) Bunge kutunga sheria maalum ya mabadiliko ya Katiba.
16. Nchi yetu imetumia utaratibu wa Bunge kutunga Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, Sura ya 83, inayoelezea utaratibu wa mchakato mzima wa kupata katiba
mpya ambao unawashirikisha wananchi kisheria katika hatua zote muhimu za
uandikaji wa katiba yao.
17. Sheria imeanzisha Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ikaweka Hadidu za Rejea
na kuipa Tume jukumu la kuratibu, kukusanya maoni ya wananchi, kuchambua na
kutathmini maoni na kuandaa Ripoti na Rasimu ya Katiba. Baadaye wananchi,
kupitia Mabaraza ya Katiba, walipewa fursa tena ya kutoa maoni yao kabla ya
Tume kufanya maboresho na kuiwasilisha katika Bunge Maalum la Katiba; hatua
ambayo ndipo tulipofikia hivi sasa.
18. Baada ya Bunge Maalum kutoa Katiba inayopendekezwa, wananchi watapata
fursa ya kufanya uamuzi wa mwisho kuhusu Katiba Mpya kupitia kura ya maoni. Si
nia yangu kutoa maelezo kuhusu historia ya katiba nchini, kwa kuonyesha
tumetoka wapi, tupo wapi na tunakwenda wapi. Maelezo ya kina kuhusu suala hilo
yamo kwenye Sura ya Tatu ya Ripoti ya Tume kuhusu Mchakato wa Mabadiliko ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Utangulizi wa Rasimu ya Katiba
19. Rasimu ya Katiba inaanza na utangulizi. Utangulizi ni sehemu muhimu ya
Katiba ya nchi. Katika hali ya sasa ya mwelekeo wa taaluma ya sheria duniani,
na kwa mujibu wa Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1 ya Sheria za Tanzania,
Utangulizi ni sehemu ya Katiba. Utangulizi ndio kioo kinachoonyesha dhamira ya
Katiba kwa kutoa tafsiri ya jumla ya Katiba. Sehemu hii inatoa taswira na picha
halisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watu wake, historia yao, matarajio
yao, misingi na masuala muhimu ambayo wanataka kuyaendeleza katika jamii,
kizazi hadi kizazi.
20. Utangulizi wa Rasimu ya Katiba unatamka rasmi kwamba Katiba hii ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetungwa na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na kuthibitishwa na wananchi kupitia kura ya maoni.
Eneo la Jamhuri
Eneo la Jamhuri
21. Tume imependekeza eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lijumuishe
eneo lote la iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika ikijumuisha sehemu yake ya bahari
na eneo lote la iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ikijumuisha sehemu yake
ya bahari, kama ilivyoainishwa katika Katiba za Uhuru za nchi mbili hizi.
22. Madhumuni ya kubainisha eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni
kukubaliana na maoni ya wananchi waliotaka kuwepo kwa ufafanuzi thabiti kuhusu
eneo na mipaka ya nchi. Kufanya hivi, kutatunza historia ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na kuondoa utata na hisia kwamba mipaka ya nchi hizi mbili
inabadilika.
23. Lengo pia la sehemu hii ni kuainisha mipaka ya kimataifa ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inayotambulika na mikataba mbalimbali ya kimataifa na
Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Bahari wa mwaka 1982.
Misingi Mikuu ya Taifa
24. Rasimu ya Katiba, kama ilivyo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977, imeorodhesha misingi mikuu ya Taifa inayojenga Taifa la
Tanzania na kusimamia ustawi wa wananchi wake. Katiba ya sasa ina misingi mikuu
minne, yaani, uhuru, haki, udugu na amani. Wananchi walipendekeza misingi
mingine minne iongezwe, yaani utu, usawa, umoja na mshikamano. Kwa hiyo,
misingi inayopendekezwa ni Utu, Uhuru, Haki, Udugu, Amani, Usawa, Umoja na
Mshikamano.
Tunu za Taifa
Tunu za Taifa
25. Tunu za Taifa ni mambo muhimu ya kujivunia kwa jamii yoyote ile. Tunu
ndio msingi wa maadili na utamaduni wa jamii. Tume inapendekeza tunu zifuatazo
zitajwe ndani ya Katiba: Utu, Uzalendo, Uadilifu, Umoja, Uwazi, Uwajibikaji na
Kiswahili ambayo ni lugha rasmi ya Taifa.
26. Madhumuni ya kupendekeza Tunu hizi kuingizwa katika Katiba ni kuheshimu
na kuzingatia maoni na mapendekezo ya wananchi kuwa Katiba itaje Tunu za Taifa
ili kuifanya jamii kuzitambua, kuzithamini na kuzitekeleza.
Malengo Muhimu
Malengo Muhimu
27. Sura ya Pili ya Rasimu inaelezea Malengo Muhimu na Misingi ya Shughuli
za Serikali na Sera za Kitaifa. Wakati wa kukusanya maoni, wananchi wengi, hasa
wale wanaoishi vijijini, walizungumzia sana dira ya taifa kuhusu maendeleo yao.
0
28. Moja ya mambo ambayo wananchi waliyatolea maoni kwa msisitizo mkubwa ni ardhi. Wananchi wengi walilalamika kwamba wanayo matatizo kutokana na ugumu wa kupata ardhi kwa ajili ya kilimo na shughuli nyingine lakini wawekezaji wakubwa wanapewa upendeleo wa kupata ardhi kwa urahisi. Pia, kuna migongano isiyokwisha ya makundi mbalimbali, wakulima na wafugaji, wananchi na mamlaka za hifadhi za taifa na kadhalika. Kuna malalamiko mengi kuhusu huduma za kilimo kama vile zana za kilimo, pembejeo na mizania ya bei.
0
28. Moja ya mambo ambayo wananchi waliyatolea maoni kwa msisitizo mkubwa ni ardhi. Wananchi wengi walilalamika kwamba wanayo matatizo kutokana na ugumu wa kupata ardhi kwa ajili ya kilimo na shughuli nyingine lakini wawekezaji wakubwa wanapewa upendeleo wa kupata ardhi kwa urahisi. Pia, kuna migongano isiyokwisha ya makundi mbalimbali, wakulima na wafugaji, wananchi na mamlaka za hifadhi za taifa na kadhalika. Kuna malalamiko mengi kuhusu huduma za kilimo kama vile zana za kilimo, pembejeo na mizania ya bei.
29. Mkulima mmoja wa pamba, wilaya ya Kahama, alilalamika kwamba ingawa
wanaambiwa na Serikali kwamba watajiondoa kwenye lindi la umaskini kupitia
kilimo bora, lakini haoni dalili hizo. Alisema wakulima wana matatizo ya mbegu,
dawa za kuuwa wadudu na bei ndogo ya mazao. Alisema mwaka 2012 alikuwa ametumia
shilingi mia nane kupata kilo moja ya pamba, lakini bei aliyopewa ilikuwa
shilingi mia sita. Katika mazingira haya, badala ya kupata maisha bora, anazidi
kuwa maskini.
30. Wakulima wa mazao ya chakula wana matatizo ya aina hiyo, na hivyo hivyo
kwa wakulima wa mazao ya biashara. Wafugaji nao wana matatizo ya ardhi ya
malisho, maji, madawa ya mifugo na bei ya mifugo yao. Wavuvi wana matatizo ya
maeneo ya uvuvi, zana za uvuvi bei na kadhalika.
31. Wananchi pia walizumgumzia hifadhi ya jamii, hasa kwa wazee. Wanasema
wafanyakazi wana mifumo ya hifadhi ya jamii na mishahara yao inaongezwa kila
wakati. Kwa Wakulima, mapato yao ni madogo na wakizeeka hawana hifadhi yoyote.
Hata matibabu ya wazee siyo bure kama utaratibu wa Serikali
unavyoelekeza, kwani sharti wanunue dawa wakati uwezo wao wa kifedha ni mdogo.
unavyoelekeza, kwani sharti wanunue dawa wakati uwezo wao wa kifedha ni mdogo.
32. Wananchi pia walizungumzia elimu na huduma za afya. Kwa maoni yao,
elimu bora na huduma za afya bora zinatolewa kwa watu wa tabaka la juu. Wao
wanabaki na shule zenye huduma hafifu na zahanati zenye kutoa huduma hafifu.
33. Tume imezingatia maoni ya wananchi na imependekeza mambo kadhaa. Kubwa
ni kuweka dira ya taifa. Sura ya Pili yote ya Rasimu ya Katiba inazungumzia
dira ya taifa. Madhumuni ya kuweka Malengo Muhimu na Misingi ya Shughuli za
Serikali ni kuhakikisha kuwa Serikali na mamlaka zake zinapewa mwongozo wa
kisera na mwelekeo wa kiutendaji. Pamoja na mambo mengine malengo yafuatayo
yamewekwa kwa ajili ya wakulima, wafugaji na wavuvi:
(i) Kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima, wafugaji na wavuvi;
(ii) Kuweka mazingira bora kwa ajili ya kukuza kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kuhakikisha kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao;
(iii) Kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa mazao kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, utafutaji na uendelezaji wa masoko ya mazao yao;
(iv) Kuweka utaratibu mzuri wa upangaji na usimamiaji wa mizania ya bei za mazao na pembejeo.
34. Haki ya kumiliki mali imejumuishwa kwenye haki za binadamu, na vivyo hivyo, haki ya elimu bora ya msingi ipatikanayo bila malipo.
(i) Kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima, wafugaji na wavuvi;
(ii) Kuweka mazingira bora kwa ajili ya kukuza kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kuhakikisha kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao;
(iii) Kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa mazao kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, utafutaji na uendelezaji wa masoko ya mazao yao;
(iv) Kuweka utaratibu mzuri wa upangaji na usimamiaji wa mizania ya bei za mazao na pembejeo.
34. Haki ya kumiliki mali imejumuishwa kwenye haki za binadamu, na vivyo hivyo, haki ya elimu bora ya msingi ipatikanayo bila malipo.
Maadili
35. Wananchi walio wengi walionyesha kufadhaishwa sana na kuporomoka kwa
maadili ndani ya jamii na ndani ya Uongozi wa Umma kwa kiwango kikubwa. Aidha,
wananchi walitoa maoni yao kuwa Sekretariati ya Maadili ya Viongozi iliyopo
haina mamlaka ya kutosha ya kuchukua hatua zinazostahiki kwa viongozi
wanaovunja na kukiuka maadili ya uongozi.
36. Katika kuchambua na kutathmini maoni ya wananchi kuhusu maadili ya
viongozi wa umma na uwajibikaji, Tume ilifanya utafiti kuhusu dhana ya
uwajibikaji. Aidha, Maoni ya Mabaraza ya Katiba yamesisitiza umuhimu wa kuwepo
kwa Maadili na miiko ya Viongozi wa Umma ndani ya Katiba.
37. Kwa kuzingatia maoni ya wananchi na Taarifa ya utafiti, Tume
inapendekeza Maadili ya Viongozi wa Umma na Miiko ya Uongozi yawekwe katika
Katiba. Aidha, inapendekezwa Sekretariati ya Maadili ya Viongozi ibadilishwe
kuwa Tume kamili ya kikatiba yenye mamlaka na uwezo mkubwa wa kusimamia maadili
ya viongozi.
Haki za Binadamu
38. Kwa kiwango kikubwa Haki za Binadamu zilizoainishwa kwenye Rasimu ya
Katiba zinafanana sana na namna zilivyo kwenye katiba ya sasa. Kwa kuzingatia
maoni ya wananchi ya kutaka kuimarishwa kwa Haki za Binadamu, Tume inapendekeza
kuimarishwa kwa Haki hizo kwa kuondoa vikwazo visivyo vya lazima. Kwa mfano,
kuimarisha ushiriki wa wananchi kwenye uongozi kwa kuruhusu mgombea huru
kikatiba.
39. Tume kwa kuzingatia maoni ya wananchi na mikataba ya kimataifa
inapendekeza kuongezwa kwa haki mpya kwa kuzingatia maadili ya watanzania.
Miongoni mwa haki hizo ni Haki za Wafanyakazi, Haki ya Mtoto, Haki za Watu
wenye Ulemavu, Haki za Wanawake, Haki za Wazee, Haki za Vijana, Haki za Kupata
Habari, Haki na Uhuru wa Habari na Vyombo vya Habari. Baadhi ya haki hizi zimo
kwenye sheria mahususi za nchi. Hata hivyo, Tume imeona ni vyema zikawekwa
kwenye katiba ili kuweka msingi wa wananchi kuweza kuhoji na kudai utekelezaji
wake kikatiba.
40. Pamoja na haki hizo, haki ya kumiliki mali, ilitolewa maoni na wananchi
kwa msisitizo wa kipekee. Maoni ya wananchi wengi yanahusu upungufu katika
utekelezaji na usimamizi wa sheria za ardhi kuhusu umiliki, uchukuaji wa maeneo
ya ardhi yao na ulipaji wa fidia stahiki. Aidha, wananchi walilalamika kuwa
Serikali imekuwa ikichukua mali zao bila fidia stahiki. Hivyo, Tume
inapendekeza kuwa mtu yeyote ana haki ya kumiliki na kupata hifadhi ya mali
ambayo ameipata kwa njia ya halali na kwamba, asinyang’anywe mali hiyo kwa
madhumuni yoyote, bila ya kupata malipo stahiki yanayolingana na thamani halisi
ya mali hiyo kwa wakati.
Uraia
Uraia
41. Rasimu imetamka Uraia kuwa ni mmoja ambao ni wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Moja ya masuala makuu ya kidola (sovereign functions) ni uraia. Suala
la uraia limeorodheshwa kuwa ni miongoni mwa Mambo ya Muungano.
42. Uraia ni msingi wa utambulisho (identity) unaompa raia haki ya kulindwa
na nchi yake, ikiwa ni pamoja na haki zake za binadamu za asili na
zisizoondosheka (inherrent and inalienable rights) kama zilivyotambuliwa au
zitakavyotambuliwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba za
Nchi Washirika na Mikataba ya Kimataifa.
43. Uraia kama ulivyowekwa katika Rasimu ya Katiba, umejengwa katika msingi
wa uzalendo usiotiliwa shaka (patriotism) unaompatia raia wajibu wa kuitetea,
kuilinda na kuifia nchi yake bila ya mashaka. Kwa hiyo, Uraia ndiyo kigezo na
sifa ya kupewa dhamana ya uongozi wa Taifa na kuajiriwa katika mihimili ya
Serikali na vyombo vya Ulinzi na Usalama. Rasimu inapendekeza kutambuliwa kwa
uraia wa kuzaliwa na uraia wa kujiandikisha ambao, katika kujidhihirisha kwake,
ni uraia wa nchi moja usiojenga au kuleta hisia za kuwabagua au kuwatenga raia
katika matabaka na madaraja yanayotokana na tofauti ya hali au fursa zao.
44. Rasimu ya Katiba pia inapendekeza kuwapatia hadhi mahsusi watu wenye
asili au nasaba ya Utanzania ambao wameacha kuwa raia wa Tanzania kwa kuchukua
Uraia wa nchi nyingine.
45. Lengo ni kuwarahisishia watu wenye asili ya Tanzania waliochukua uraia
wa nchi nyingine wakija hapa nyumbani wasipate usumbufu usio wa lazima na pia
ili warahisishiwe ushiriki wao katika ujenzi wa taifa kwa kuwawezesha kuchangia
ipasavyo katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania. Utaratibu kama huu unafuatwa
katika nchi kadhaa, kwa mfano Ethiopia, India na Ujerumani ambako umeonyesha
mafanikio.
Mihimili ya Serikali
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Mheshimiwa Mwenyekiti;
46. Sura ya Saba hadi Sura ya Kumi zinahusu Mihimili ya Serikali. Katika
sehemu hii kuna mapendekezo ambayo yataleta mabadiliko makubwa.
47. Tukianza na taasisi ya Urais, kuna mapendekezo manne makubwa. Pendekezo
la kwanza ni kumuondoa Rais kutoka kwenye Bunge.
Hali ilivyo sasa, Rais ni sehemu ya Bunge na Mawaziri wake ni Wabunge. Nia ya pendekezo hili ni kutenganisha mamlaka na madaraka ya mihimili (separation of powers). Kazi kubwa ya Bunge ni kuisimamia Serikali. Bunge haliwezi kuisimamia Serikali kwa uhuru kama Serikali nayo ni sehemu ya Bunge. Kwa kifupi, lengo la pendekezo hili ni kuongeza mamlaka na madaraka ya Bunge.
Hali ilivyo sasa, Rais ni sehemu ya Bunge na Mawaziri wake ni Wabunge. Nia ya pendekezo hili ni kutenganisha mamlaka na madaraka ya mihimili (separation of powers). Kazi kubwa ya Bunge ni kuisimamia Serikali. Bunge haliwezi kuisimamia Serikali kwa uhuru kama Serikali nayo ni sehemu ya Bunge. Kwa kifupi, lengo la pendekezo hili ni kuongeza mamlaka na madaraka ya Bunge.
48. Katika pendekezo la pili, mtu atakuwa amechaguliwa kuwa Rais kama
atapata kura za wapiga kura zaidi ya nusu (absolute majority), badala ya
utaratibu wa sasa wa kupata wingi wa kura (simple majority). Msingi wa
pendekezo hili ni kwamba, Rais si kiongozi wa Serikali tu bali pia ni Mkuu wa
Nchi na Amri Jeshi Mkuu. Kwa sababu hiyo, Rais ndiye alama na taswira ya nchi
na watu wake, na Rais ndiye alama ya umoja na uhuru wa nchi na mamlaka ya nchi.
Kwa maana hiyo, ni muhimu Rais kuonekana anakubalika kwa wananchi walio wengi.
49. Pendekezo la tatu ni kuruhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais kuhojiwa
Mahakamani. Kwa hali ya sasa, matokeo ya uchaguzi wa Rais yakishatangazwa na
Tume ya Uchaguzi, hakuna ruhusa ya kuyahoji matokeo hayo.
50. Katika uchaguzi wa Rais, inawezekana kutakuwa na sababu za msingi
kuamini kwamba uchaguzi huo haukuwa halali. Ni jambo la msingi kuhakikisha
kwamba Rais amechaguliwa kihalali. Hata hivyo, tahadhari imewekwa ili
kuhakikisha kwamba ruhusa hii isitumiwe vibaya. Kwanza, mtu anayeweza kuhoji ni
yule tu aliyekuwa mgombea nafasi ya Urais. Sharti hili litazuia watu kutumia
vibaya ruhusa ya kuhoji matokeo ya uchaguzi wa Rais. Pili, ni Mahakama ya Juu
tu ndiyo yenye madaraka ya kusikiliza shauri la aina hii na ni lazima uamuzi
juu ya shauri hilo utolewe ndani ya muda wa mwezi mmoja. Wenzetu wa Kenya na
mataifa mengine duniani wanao utaratibu kama huu.
51. Pendekezo la nne linahusu madaraka ya Rais. Suala la madaraka ya Rais
limezungumziwa kwa uzito sana katika kipindi hiki. Wakati wa kutunga Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba, suala la madaraka ya Rais lilijitokeza sana. Wakati wa
kukusanya maoni wananchi nao walilitolea maoni mengi.
52. Baada ya uchambuzi na tathmini ya maoni yote na Taarifa ya Utafiti,
Tume imependekeza kwamba Rais abaki na madaraka ya msingi kama Mkuu wa Nchi,
Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa Serikali. Madaraka hayo yameainishwa katika Ibara
ya 72 ya Rasimu. Hata hivyo, madaraka ya Rais akiwa Mkuu wa Serikali na hasa
kwa upande wa uteuzi wa viongozi, ama yamepunguzwa au yamewekewa utaratibu. Rais
amepunguziwa madaraka ya kuteua watumishi wa umma wa ngazi za kati na ngazi za
chini. Watumishi hao uteuzi wao utakuwa kwenye madaraka ya Tume za Utumishi.
53. Rais, atabaki na madaraka ya kuwateua viongozi wa kitaifa, kama vile
Mawaziri, Majaji, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu Wakuu wa
Wizara na Wenyeviti na Wajumbe wa Tume za kitaifa. Pamoja na kubaki na madaraka
hayo, Rais amewekewa utaratibu wa uteuzi. Baadhi ya viongozi watateuliwa moja
kwa moja na Rais na baadaye watathibitishwa na Bunge, kwa mfano, Mawaziri.
Wengine watapendekezwa na Kamati ya Uteuzi na baada ya kuteuliwa,
watathibitishwa na Bunge, kwa mfano, Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya
Uchaguzi. Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama watateuliwa na Rais kwa
kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa. Wengine watateuliwa
kutokana na ushauri wa Tume za Utumishi, kama vile Majaji na Makatibu Wakuu.
Bunge
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Mheshimiwa Mwenyekiti;
54. Kwa Bunge la Muungano, madaraka yake na mamlaka yatabaki kusimamia
mambo ya Muungano. Kinachobadilika sasa ni Bunge kutokuwa na mamlaka juu ya
mambo yasiyo ya Muungano ya Tanganyika kama ambavyo imekuwa kwa upande wa
Zanzibar. Hata hivyo, Bunge la Muungano litapata taarifa ya uratibu na
utekelezaji wa mambo yasiyo ya Muungano ya Tanganyika na ya Zanzibar kupitia
Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali.
55. Imependekezwa pia kwamba Spika na Naibu Spika wasitokane na Mawaziri,
Naibu Mawaziri au Wabunge. Lengo la pendekezo hili ni kupata viongozi ambao
wataonekana hawaegemei upande wowote. Imependekezwa pia kwamba Wabunge wasiwe
Mawaziri. Pendekezo hili limetokana na maoni ya wananchi
kwamba wanahitaji Wabunge kuwa karibu na wapiga kura wao. Wengine wanaamini
kwamba wabunge ambao ni Mawaziri wanapendelea majimbo yao ya uchaguzi badala ya
kutumikia taifa kwa ujumla kwa usawa.
56. Lakini lengo jingine la pendekezo hili, ni kutenganisha madaraka ya
mihimili. Kama Bunge likiwa na madaraka ya kuthibitisha Mawaziri itakuwa vigumu
kwa Wabunge kuwakataa Wabunge wenzao watakaoteuliwa kuwa Mawaziri, kisha kuendelea
kukaa pamoja kwa utulivu ndani ya Bunge.
57. Tume imependekeza ukomo wa ubunge kuwa vipindi vitatu vya miaka mitano
mitano. Hata hivyo, wananchi wanaweza kumwondoa Mbunge wao kabla ya kumaliza
muda wa kipindi chake cha miaka mitano. Pendekezo hili linatokana na maoni ya
wananchi waliotaka kuwepo ukomo wa ubunge ili kuondoa dhana ya umiliki wa jimbo
la uchaguzi, kutoa fursa kwa wananchi wengine wenye uwezo kugombea nafasi ya
ubunge, kuongeza uwajibikaji wa wabunge katika majimbo ya uchaguzi na kuongeza
mamlaka ya wananchi kuwawajibisha viongozi wao.
58. Pia, ni maoni ya wananchi kuwa kusiwepo uchaguzi mdogo ili kupunguza
gharama. Endapo nafasi ya ubunge itaachwa wazi kutokana na mbunge wa chama cha
siasa kupoteza Ubunge, basi Tume Huru ya Uchaguzi itajaza nafasi hiyo kutokana
na orodha ya majina yaliyowasilishwa na chama cha siasa husika na kwa
kushirikiana na chama hicho. Uchaguzi mdogo utafanyika tu pale ambapo nafasi ya
ubunge iliyo wazi imetokana na mbunge huru.
Mahakama
59. Kuhusu Mahakama, pendekezo kubwa ni kuundwa kwa Mahakama ya Juu na
kwamba Mahakama hiyo na Mahakama ya Rufani ndizo ziwe Mahakama za Muungano.
Mahakama Kuu ziendelee kutokuwa za Muungano kama ilivyo sasa. Hata hivyo,
inapendekezwa kuwa Mahakama Kuu ya Tanganyika na Mahakama Kuu ya Zanzibar ziwe
na mamlaka sawa katika kusikiliza na kuamua mashauri yanayohusu masuala ya
Muungano na yasiyo ya Muungano (concurrent jurisdiction). Hivi ndivyo ilivyo
hivi sasa kwa upande mmoja, ambapo Mahakama Kuu ya Zanzibar, japokuwa si sehemu
ya Mahakama za Jamhuri ya Muungano, lakini imepewa mamlaka na Katiba ya Jamhuri
ya Muungano kusikiliza na kuamua kuhusu mashauri ya kesi za madai na jinai
yanayohusu sheria za muungano. Pendekezo jingine ni kuuweka Mfuko wa Mahakama
ndani ya Katiba.
Vyombo vya Kikatiba
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Mheshimiwa Mwenyekiti,
60. Masuala mengine ambayo yameainishwa na kuwekewa masharti ya Kikatiba ni
Utumishi wa Umma katika Jamhuri ya Muungano, Tume Huru ya Uchaguzi, Tume ya
Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji na Tume ya Haki za Binadamu.
Tume ya Utumishi wa Umma
Tume ya Utumishi wa Umma
61. Rasimu ya Katiba inaweka utumishi wa umma wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ndani ya Katiba. Sura ya Kumi na Moja inaainisha misingi na kanuni
kwamba utumishi wa umma ni dhamana kutoka kwa wananchi na hivyo, mtumishi
anatakiwa kutumikia wananchi kwa uadilifu na uaminifu. Misingi mingine ni
kudumisha na kukuza viwango vya juu vya maadili ya kitaaluma, na kuhakikisha
kwamba uteuzi na uajiri katika nafasi mbalimbali unazingatia uwezo wa
kitaaluma, uweledi, maarifa, ujuzi, umakini na uzoefu katika eneo husika.
Msingi mwingine ni kutoa huduma kwa umma kwa njia ya haki, usawa na bila
upendeleo. Misingi hii itatumika katika mihimili yote ya dola, taasisi na idara
zote za Serikali, mashirika, makampuni na wakala wa Serikali.
62. Ili kuweka mfumo madhubuti wa usimamizi wa utumishi wa umma, Rasimu ya
Katiba inaanzisha Tume ya Utumishi ya Umma wa Jamhuri ya Muungano ambayo
itaongozwa na Mwenyekiti na wajumbe wengine sita watakaoteuliwa na Rais na
kuidhinishwa na Bunge. Tume ya Utumishi wa Umma itakuwa ni chombo cha juu
katika Utumishi wa Umma chenye mamlaka ya kusimamia na kuratibu mambo yote ya
utumishi wa umma.
63. Ibara ya 188 inaainisha majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma ambayo ni
pamoja na kumshauri Rais juu ya uteuzi wa viongozi katika nafasi mbalimbali za
utumishi wa umma, kutoa miongozo mbalimbali ya kusimamia mchakato wa ajira
katika utumishi wa umma na kuhamasisha utekelezaji wa misingi na kanuni za
utumishi katika Sekta zote za Utumishi wa Umma. Tume pia itakuwa na mamlaka ya
kuunda na kupanga mishahara na marupurupu ya watumishi wote, wakiwemo viongozi
wa kisiasa.
Tume Huru ya Uchaguzi
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Mheshimiwa Mwenyekiti,
64. Rasimu ya Katiba, kama ilivyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka
1977, imetambua haki ya kupiga kura kuwa ni haki ya msingi ya raia ambayo ni
lazima
itambuliwe na kulindwa na Katiba. Kwa umuhimu huo, inapendekezwa kuwepo kwa
mfumo wa wazi wa utaratibu wa ushiriki wa wananchi katika uchaguzi na kura ya
maoni.
65. Ili kusimamia taratibu za uchaguzi, Rasimu ya Katiba inapendekeza Tume
Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano. Tume ndiyo itakayosimamia masuala ya
uchaguzi na kura za maoni. Yapo masharti kuhusu upatikanaji wa wajumbe kwa
uwazi kupitia utaratibu wa kuomba nafasi na kuchujwa na Kamati ya Uteuzi kabla
ya kuteuliwa rasmi na Rais.
66. Rasimu ya Katiba inaanzisha Kamati ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi. Wajumbe hao ni Jaji Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Mwenyekiti, Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano, Spika wa Bunge la Tanganyika, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Jaji
Mkuu wa Tanganyika, Jaji Mkuu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya
Viongozi na Uwajibikaji.
67. Inapendekezwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume
wathibitishwe na Bunge. Rasimu pia inaweka sifa za watu wanaoweza kuchaguliwa
kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume. Tume Huru ya Uchaguzi ni
chombo muhimu katika mfumo wa utawala wa kidemokrasia kupitia uchaguzi huru na
wa haki. Mapendekezo haya yamezingatia misingi inayokubalika duniani kuhusu
umuhimu wa kuwepo vyombo huru vya usimamizi wa uchaguzi. Misingi hiyo ni uhuru,
uadilifu, uwajibikaji na uwazi.
Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Mheshimiwa Mwenyekiti,
68. Kwa kuzingatia masharti yaliyomo katika Sura ya Tatu kuhusu Maadili na
Miiko ya Uongozi na Utumishi wa Umma, Rasimu ya Katiba inapendekeza kuanzishwa
kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji na kutaja sifa za mtu kuteuliwa
kuwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume na kuthibitishwa na Bunge. Tume ya
Maadili itakuwa ni chombo cha kikatiba kitakachokuwa na nguvu ya kusimamia
maadili ya Viongozi wa Umma.
69. Majukumu ya Tume ya Maadili ni kusimamia maadili na uwajibikaji katika
utumishi wa umma, kuchunguza tabia na mwenendo wa mtumishi au kiongozi na
kuchukua hatua pale inapostahili. Uhuru wa Tume katika utekelezaji wa majukumu
yake ni muhimu ili kuhakikisha kuwa haitaingiliwa na mtu au mamlaka yoyote
katika utekelezaji wa majukumu hayo.
Tume ya Haki za Binadamu
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Mheshimiwa Mwenyekiti,
70. Tume ya Haki za Binadamu ni taasisi ambayo inapendekezwa iendelee
kuwepo ndani ya Katiba. Rasimu ya Katiba imeainisha muundo wake na utaratibu wa
kuwateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna.
71. Majukumu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyopo hivi sasa
kuhusu masuala ya utawala bora, yamewekwa katika Tume ya Maadili ya Uongozi na
Uwajibikaji, hasa yanayohusu matumizi mabaya ya madaraka. Vile vile,mapendekezo
haya yanakubaliana na maoni ya wananchi waliotaka kuwepo kwa utaratibu
utakaokuza, kuhifadhi na kulinda haki za binadamu.
72. Rasimu ya Katiba inapendekeza kuendelea kuwepo kwa uhuru wa Tume katika
utekelezaji wa majukumu yake ili kuhakikisha kuwa haiingiliwi na mtu au mamlaka
yoyote. Masharti haya ya kikatiba yataiwezesha Tume kufanya kazi kwa uhuru na
kuwawezesha Makamishna kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu, uadilifu na bila
ya woga au upendeleo. Hali hii itaendeleza imani ya wananchi kuwa; maamuzi
yatakayofanywa na Tume hayatokani na maelekezo, shinikizo au matakwa ya mtu,
kikundi cha watu au chombo kingine chochote.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
73. Baada ya maelezo hayo ya jumla kuhusu Rasimu ya Katiba, sasa naomba
nizungumzie Rasimu ya Katiba kwa kupitia maudhui ya kila Sura. Kama
nilivyoeleza hapo awali, maelezo ya kina kuhusu kila Ibara na sababu za
mapendekezo zimeelezwa kwenye Randama ambayo waheshimiwa wajumbe watapatiwa
pamoja na nakala ya Hotuba hii.
74. Rasimu ya Katiba inayopendekezwa ni ndefu kidogo, ina Ibara 271,
ikilinganishwa na Katiba ya sasa yenye Ibara 152. Rasimu hii imeganywa katika
Sura Kumi na Saba. Ongezeko la Ibara, kwa kiwango kikubwa, limetokana na Tume
kuzingatia maoni ya wananchi ambao walitaka mambo mengi zaidi yaingizwe kwenye
Katiba.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
75. Sura ya Kwanza ya Rasimu ya Katiba imegawika katika Sehemu mbili.
Sehemu ya Kwanza inaanzia Ibara ya 1 hadi 5 na zinahusu Jina, Eneo la Jamhuri
ya Muungano, Alama, Lugha na Tunu za Taifa. Sehemu ya Pili inaanzia Ibara ya 6
hadi 9 zinazopendekeza masharti kuhusu Mamlaka ya Wananchi, Watu na Serikali,
Ukuu na Utii wa Katiba na Hifadhi ya Utawala na Katiba.
76. Sura ya Pili ya Rasimu ina Ibara ya 10 hadi 12. Sehemu hii inapendekeza
masharti yanayohusu Malengo Makuu, Utekelezaji wa Malengo ya Taifa na Sera ya
Mambo ya Nje.
77. Sura ya Tatu ya Rasimu imegawika katika Sehemu mbili. Sehemu ya Kwanza
inaanzia Ibara ya 13 hadi 20 zinazopendekeza masharti kuhusu Dhamana ya Uongozi
wa Umma, Kanuni za Uongozi wa Umma, Zawadi katika Utumishi wa Umma, Akaunti Nje
ya Nchi na Mikopo, Wajibu wa Kutangaza Mali na Madeni, Mgongano wa Maslahi,
Matumizi ya Mali ya Umma na Utekelezaji wa Masharti ya Maadili.
78. Sehemu ya Pili ya Sura ya Tatu inaanzia Ibara ya 21 hadi 22
zinazopendekeza masharti kuhusu Utii wa Miiko ya Uongozi wa Umma na Marufuku ya
Baadhi ya Vitendo kwa Watumishi wa Umma.
79. Sura ya Nne ya Rasimu ina sehemu mbili. Sehemu ya Kwanza inayoanzia
Ibara ya 23 hadi 48 inahusu Haki za Binadamu. Haki hizo kwa sasa zimeainishwa
vizuri zaidi na kuongeza haki za makundi mbalimbali katika jamii.
80. Sehemu ya Pili ya Sura ya Nne inayoanzia Ibara ya 49 hadi 55 inahusu
mipaka ya matumizi ya haki za binadamu na wajibu wa raia na Serikali ambazo
zimewekwa kwa upana na uwazi zaidi ikiwemo Wajibu wa Raia kwa Ujumla, Wajibu wa
Kushiriki Kazi, Wajibu wa Kulinda Mali ya Umma, Haki na Wajibu Muhimu kwa Raia,
Hifadhi ya Haki za Binadamu, Usimamizi wa Haki za Binadamu na Mipaka ya Hifadhi
ya Haki za Binadamu.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
81. Sura ya Tano ya Rasimu ya Katiba inaanzia Ibara ya 56 hadi 59 na
inapendekeza masharti kuhusu Uraia wa Jamhuri ya Muungano. Rasimu inapendekeza
aina mbili za uraia; wa kuzaliwa na kujiandikisha. Ibara 59 inapendekeza kuwapa
hadhi maalum watu walioacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano tofauti na raia wa
nchi nyingine ambao hawana asili au nasaba ya Tanzania.
82. Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba inaanzia Ibara ya 60 hadi 69 na
inahusu Muundo wa Jamhuri ya Muungano. Rasimu inapendekeza masharti kuhusu
Muundo wa Muungano, Vyombo vya Utendaji vya Jamhuri ya Muungano, Mamlaka ya
Serikali ya Muungano, Mambo ya Muungano, Nchi Washirika, Mamlaka ya Nchi
Washirika, Mahusiano kati ya Nchi Washirika, Mawaziri Wakaazi, Mamlaka ya
Wananchi na wajibu wa Kuhifadhi Muungano.
83. Sehemu hii inapendekeza muundo wa Muungano wa Shirikisho la Serikali
tatu, ambazo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya
Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Pia inaainisha mihimili mikuu
ya dola ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama ya Jamhuri ya Muungano. Sehemu
hii pia inatambua kwamba mambo mengine ya kiutendaji yasio ya Muungano
yataainishwa katika Katiba za Nchi Washirika
84. Sura ya Saba inahusu Serikali ya Jamhuri ya Muungano na imegawanyika
katika sehemu mbili. Sehemu ya Kwanza inaanzia Ibara ya 70 hadi 96
zinazopendekeza masharti kuhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano, Uchaguzi wa Rais,
Masharti Mahsusi kuhusu Mamlaka ya Rais na nafasi ya Makamu wa Rais.
85. Sehemu ya Pili ya Rasimu ya Katiba inanzia Ibara ya 97 hadi 108
zinazohusu Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Sehemu hii
inapendekeza Masharti kuhusu Kuundwa kwa Baraza la Mawaziri, uteuzi wa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu Wakuu pamoja na
sifa za uteuzi. Aidha, masharti ya Utekelezaji wa shughuli za Baraza la
Mawaziri yanapendekezwa.
86. Sura ya Nane inaanzia Ibara ya 109 hadi 112 na inahusu Uhusiano na
Uratibu wa Serikali. Ili kuzuia uwezekano wa mgongano, na kwa lengo la
kuwianisha sera, sheria, mipango na mikakati, Rasimu inapendekeza kuundwa Tume
ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali. Tume hii ni muhimu katika Muungano wowote
kwa kuwa mambo yasiyo ya Muungano mara nyingi ndio husababisha tofauti na mgawanyiko
mkubwa katika nchi. Kwa lengo hilo hilo, Rasimu ya Katiba inapendekeza
kuanzishwa kikatiba, Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa. Baraza hilo litakuwa
chini ya Uwenyekiti wa Rais na Wajumbe wake watakuwa ni pamoja na Rais wa
Tanganyika na Rais wa Zanzibar.
87. Sura ya Tisa ya Rasimu inahusu Bunge la Jamhuri ya Muungano. Sura hii
inaanzia Ibara ya 113 hadi 149 na imegawika katika sehemu Sita. Katika Sura
hii, Rasimu inapendekeza masharti kuhusu Muundo na Madaraka ya Bunge, Uchaguzi
wa Wabunge, Uongozi wa Bunge, Utaratibu wa Shughuli za Bunge, Madaraka na Haki
za Bunge. Aidha, Rasimu inapendekeza masharti kuhusu Tume ya Utumishi na Mfuko
wa Bunge.
88. Sura ya Kumi inahusu Mahakama ya Jamhuri ya Muungano. Sura hii inaanzia
Ibara ya 150 hadi 183 na imegawanyika katika Sehemu Tatu. Sura hii inapendekeza
masharti kuhusu Kuanzishwa kwa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano, Muundo wa
Mahakama, Uanzishwaji wa Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani na Uteuzi wa
Majaji. Aidha, masharti ya Usimamizi wa Shughuli za Mahakama, Uanzishwaji wa
Tume ya Utumishi na Mfuko wa Mahakama yanaainishwa.
89. Sura ya Kumi na Moja inahusu Utumishi wa Umma katika Jamhuri ya
Muungano. Sura hii inaanzia Ibara ya 184 hadi 188 ambazo zinapendekeza masharti
kuhusu Misingi Mikuu ya Utumishi wa Umma na Ajira na Uteuzi wa Viongozi wa
Taasisi za Serikali. Aidha, Rasimu inapendekeza masharti ya uanzishwaji wa Tume
ya Utumishi wa Umma pamoja na Mamlaka na Majukumu yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
90. Sura ya Kumi na Mbili inayohusu masuala ya uchaguzi, inaanzia Ibara ya
189 hadi 199. Sura hii inapendekeza masharti kuhusu Kuundwa na Majukumu ya Tume
Huru ya Uchaguzi, Uteuzi wa Wajumbe wa Tume, Uteuzi na Majukumu ya Mkurugenzi
wa Tume ya Uchaguzi na Uteuzi na Majukumu ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
91. Sura ya Kumi na Tatu inahusu taasisi za uwajibikaji. Sura hii inaanzia
Ibara ya 200 hadi 220. Sehemu hii inapendekeza masharti kuhusu uanzishwaji na
majukumu ya Tume ya Maadili ya Viongozi na Uwajibikaji, Tume ya Haki za
Binaadamu na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Seikali.
92. Sura ya Kumi na Nne inahusu fedha za Jamhuri ya Muungano. Sura hii
inaanzia Ibara ya 221 hadi 234 na inapendekeza masharti kuhusu Mfuko Mkuu wa
Hazina na Fedha za Jamhuri ya Muungano, Deni la Taifa na Mikopo, Vyanzo vya
Mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na uanzishwaji wa Benki Kuu ya
Jamhuri ya Muungano.
93. Sura ya Kumi na Tano inaanzia Ibara ya 235 hadi 250 na inahusu ulinzi
na usalama wa Jamhuri ya Muungano. Sura hii inapendekeza masharti ya Vyombo vya
Ulinzi na Usalama wa Taifa, pamoja na kulitambua kikatiba Baraza la Ulinzi na
Usalama wa Taifa.
94. Sura ya Kumi na Sita inaanzia Ibara ya 251 hadi 256. Rasimu katika Sura
hii inapendekeza masharti ya Kujiuzulu katika Utumishi wa Umma, Kukabidhi
Madaraka, Ufafanuzi wa Maneno yaliyotumika katika Rasimu ya Katiba, Jina la
Katiba na Kuanza Kutumika kwa Katiba Mpya.
95. Sura ya Kumi na Saba ndio Sura ya Mwisho na imegawanyika katika Sehemu
Sita na ina Ibara kuanzia 257 hadi 271. Sura hii inahusu Masharti ya Yatokanayo
na Masharti ya Mpito. Rasimu inapendekeza masharti kuhusu matumizi ya masharti
ya kipindi cha mpito na ukomo wa Katiba ya mwaka 1977 ili kuhakikisha kuwa
mabadiliko ya Katiba hayafuti uhalali wa sheria za nchi zilizopo na maamuzi
yaliyofanywa chini ya Katiba iliyofutwa au Katiba za awali zilizopita na ambazo
masharti yake yanatumika hadi sasa.
96. Aidha, Rasimu inapendekeza masharti kuhusu kuendelea kuwepo madarakani
kwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri na Manaibu waziri. Pia masharti
kuhusu kuendelea kuwepo Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mahakama ya Rufani ya
Jamhuri ya Muungano.
97. Inapendekeza kuanzishwa kwa Kamati ya kusimamia utekelezaji wa mambo
yote yanayopaswa kutekelezwa katika kipindi cha mpito, muundo wake, majukumu
yake na masharti ya uteuzi wa Mwenyekiti na wajumbe, Katibu na Watumishi wa
Sekretarieti ya Kamati.
Muundo wa Muungano
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Mheshimiwa Mwenyekiti;
98. Suala la Muundo wa Serikali Tatu limechukua nafasi kubwa sana katika
mjadala tangu Tume ilipozindua Rasimu ya Kwanza ya Katiba. Mjadala wa Muundo wa
Muungano umekuwa mkubwa kwa kiasi cha kufunika mapendekezo mengine yaliyomo
katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
99. Kwa kuwa jambo hili lina umuhimu wa pekee katika mstakabali wa nchi
yetu, naomba nitumie nafasi hii kutoa maelezo ya kutosha ili Waheshimiwa
Wabunge na wananchi kwa jumla wafahamu msingi ulioifanya Tume kutoa pendekezo
hili.
100. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba katika kifungu cha 9(2) imetoa mwongozo
kwa Tume kuzingatia mambo kadhaa ya msingi. Kati ya mambo hayo ni kuendelea
kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano, uwepo wa Serikali, Bunge na Mahakama na
kuendelea kuwepo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tafsiri ya Tume ilikuwa
kwamba mwongozo huu ulikuwa kwa Tume tu, siyo kwa wananchi. Tume iliamini
sheria haikukusudia kuwazuia wananchi kutoa mawazo yao kwa uhuru bila ya
kizuizi wala mipaka. Hivyo, Tume ilipokea mawazo ya kila aina.
101. Pia, Tume ilijadili njia bora ya kupata maoni. Tume ilifikiria kuandaa
dodoso ili wananchi wajibu maswali kuhusu mambo mbalimbali kuhusu Katiba. Hata
hivyo, Tume iliamua wananchi wasipewe mwongozo ili wawe na uhuru kusema
chochote wanachoamini. Msingi huu ndio uliofuatwa na Tume ili kupata maoni ya
wananchi kuhusu maeneo yote, ikiwa ni pamoja na suala la Muungano.
102. Tume ilianza kazi kwa madhumuni ya kupata maoni ya wananchi ili
kuboresha Muungano. Wananchi wengi waliotoa maoni kuhusu Muungano, walijikita
kwenye Muundo wake kama njia ya kuondoa kero. Kwa Tanzania Bara, wananchi zaidi
ya 39,000 walitoa maoni kuhusu Muungano na kati ya hao, karibu 27,000
walizungumzia muundo. Kwa Zanzibar, wananchi karibu wote waliotoa maoni
walijikita kwenye suala la Muungano. Kati ya wananchi karibu 38,000 waliotoa
maoni kuhusu Muungano, wananchi 19,000 walitoa maoni kuhusu muundo wa Muungano.
Mchanganuo wa takwimu hizi unaonyesha kuwa wananchi waliotoa maoni kuhusu
muundo wa Muungano kwa upande wa Tanzania Bara, 13% walipendelea Serikali Moja,
24% walipendekeza Serikali Mbili na 61% walipendekeza Serikali Tatu. Kwa upande
wa Zanzibar, 34% walipendekeza Serikali mbili na 60% walipendekeza Muungano wa
Mkataba, na 0.1% (watu 25) walipendekeza Serikali Moja. Aidha, taasisi nyingi
kama vile vyama vya siasa, asasi za kiraia na jumuia za kidini zilipendekeza
Muundo wa Serikali Tatu.
103. Baadhi ya taasisi za kiserikali, ama moja kwa moja au kwa tafsiri ya
mapendekezo yao, pia zilipendekeza au kukubali muundo wa Serikali Tatu. Kwa
mfano, Baraza la Wawakilishi Zanzibar lilipendekeza kuwepo kwa mamlaka huru ya
Zanzibar, mamlaka huru ya Tanganyika na mamlaka ya Muungano na iwekwe wazi
maeneo, uwezo, nguvu, utendaji na mipaka ya kila mamlaka. Baraza la Ofisi ya
Makamu wa Rais lilipendekeza, kuhusu Muundo wa Serikali kwamba, nanukuu “kuwe
na Rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wakuu wa Serikali za
Washirika wa Muungano wapewe vyeo vingine
vinavyoendana na hadhi na mamlaka zao. Pia katika kutaja hizo serikali tatu inabidi zitenganishwe ili Serikali ya Muungano ionekane ndio ya juu”
vinavyoendana na hadhi na mamlaka zao. Pia katika kutaja hizo serikali tatu inabidi zitenganishwe ili Serikali ya Muungano ionekane ndio ya juu”
104. Baraza la Ofisi ya Waziri Mkuu lilipendekeza, kuhusu uongozi wa taifa
kwamba kuwe, na “Rais wa Jamhuri ya Muungano, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano, Waziri Mkuu wa Serikali ya Tanganyika na Waziri Mkuu wa Serikali ya
Zanzibar. Mapendekezo hayo ni kwa sababu hakuna umuhimu wa kuwa na marais
watatu (3) katika nchi moja na wala neno Rais halimuongezei hadhi kiongozi
yeyote. Pia kutoa nafasi kwa Mawaziri Wakuu kuwa watendaji zaidi na hivyo
kusimamia Serikali za Washirika.” Aidha, Bunge la Jamhuri ya Muungano katika
maoni yake lilipendekeza kuwepo kwa Tume ya Utumishi wa Bunge ambayo inajumuisha,
katika Wajumbe, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano (Mwenyekiti), Spika wa
Bunge la Tanzania Bara na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Mheshimiwa Mwenyekiti;
105. Baada ya kuona takwimu hizi na kuchanganua sababu zilizotolewa na
makundi mbali mbali, Tume iliamua kufanya utafiti wa kina kuhusu Muundo wa
Muungano na matatizo yake tangu Muungano ulipoundwa. Katika utafiti huo mambo
kadhaa yamejitokeza.
106. Kwanza, kulikuwa na changamoto nyingi baada ya Tanganyika na Zanzibar
kuungana mwaka 1964. Ujenzi wa taasisi ili kuendesha mambo ya muungano ulikuwa
ni changamoto kubwa. Serikali ya Muungano haikuwa na taasisi zake, kwa hiyo
ilianza kwa kutumia taasisi zilizokuwapo katika sehemu zote mbili za muungano.
Kwa upande wa sheria, hali ilikuwa hivyo hivyo. Hata uamuzi wa kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya demokrasia ya chama kimoja ulichukuliwa wakati nchi ikiwa
na vyama viwili; TANU na ASP. Kwa hiyo, kila upande uliendesha mambo yake
kutumia itikadi na sera zake.
107. Changamoto hizi hazikuzuia kuimarika kwa muungano kwa sababu utashi wa
kisiasa wa Waasisi wa Muungano ulikuwa mkubwa. Mwaka 1977, vyama vya siasa vya
TANU na ASP viliunganishwa na Chama Cha Mapinduzi kilizaliwa na Katiba ya
kudumu ilitungwa. Baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunjika, baadhi ya
mambo yaliyokuwa chini ya Jumuiya hiyo yaliwekwa kwenye Orodha ya Mambo ya
Muungano. Matokeo yake, nchi ilionekana ni moja, yenye mshikamano, utulivu na
amani.
108. Wakati huo, viongozi na watumishi wa umma na kwenye Chama cha siasa
walipangiwa kazi sehemu yoyote ya nchi bila kujali sehemu wanayotoka. Kwa muda
mfupi nchi ilionekana kuwa kweli ni taifa moja. Lakini hali hiyo haikudumu kwa
muda mrefu. Utaifa wa nchi mbili ukaanza kujitokeza. Viongozi na watumishi wa
umma kutoka upande mmoja wa Muungano wakaonekana hawapendi kwenda kufanya kazi
upande wa pili wa Muungano.
109. Pia majina ya sehemu mbili za Muungano yakabadilishwa. Badala ya
Tanzania Bara na Tanzania Visiwani tukaanza kutumia Tanzania Bara na Tanzania
Zanzibar, ili kulinda Zanzibar isionekane imemezwa. Ni wakati huo, lugha ya
Tanganyika kuvaa Koti la Muungano ilianza kusikika.
110. Mwaka 1984, kulitokea kile kilichoitwa “kuchafuka kwa hali ya hewa ya
kisiasa Zanzibar”. Msingi wake ilikuwa ni mpango wa baadhi ya viongozi wa
Zanzibar kutaka Serikali Tatu. Ingawa jaribio hili halikufanikiwa, Zanzibar
ilitunga Katiba Mpya mwaka huo huo.
111. Katika Katiba hiyo, Zanzibar iliondoa madaraka ya sheria zinazotungwa
na Bunge kutumika moja kwa moja Zanzibar. Katiba ya Zanzibar iliweka masharti kwamba
sheria za muungano zipelekwe kwenye Baraza la Wawakilishi kabla ya kutumika
Zanzibar.
112. Mwaka 1991, Tume ya Jaji Nyalali ilipendekeza muundo wa Serikali Tatu.
Ingawa pendekezo hili halikukubalika, Zanzibar iliamua kuwa na bendera na nembo
yake na baadaye sharti likawekwa kwamba meli zinazoingia kwenye bandari za
Zanzibar ni lazima zitumie bendera ya taifa yenye nembo ya Zanzibar. Kwa maana
nyingine, Zanzibar ikaanza kutumia Bendera ya Taifa iliyo tofauti.
113. Mwaka 1992, Zanzibar ilijiunga na Organisation of Islamic Conferece
(OIC) na Bunge lilipitisha Azimio la kuzitaka Serikali zote mbili kushirikiana
katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo na matatizo mengine ya Muungano na
kutoa taarifa Bungeni katika kipindi cha mwaka mmoja.
114. Mwaka 1993, wakati wa Mkutano wa Bajeti, Wabunge kutoka Tanzania Bara
(G 55) walipeleka Bungeni hoja ya kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika. Hoja hiyo
ilipitishwa.
115. Mwezi Novemba mwaka 1993, Kikao Maalum cha CCM na Serikali zote mbili
kilifanyika Dodoma ili kutafuta maelewano kuhusu Azimio la Bunge. Muafaka
ulifikiwa kwamba Azimio hili lisitekelezwe, yaani Serikali ya Tanganyika
isiundwe.
116. Mwaka 1994, Halmashauri Kuu ya CCM ilipitisha azimio kuhusu haja ya
kuendelea na muundo wa Serikali Mbili kwa lengo la kufikia Muundo wa Serikali
Moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Mheshimiwa Mwenyekiti,
117. Baada ya Tume ya Jaji Nyalali, Serikali iliunda Kamati ya Shellukindo
ikijumuisha wajumbe kutoka Serikali zote mbili. Serikali ya Zanzibar nayo
iliunda Kamati ya Amina Salum Ali. Kamati ya Shellukindo ilichambua Mambo yote
ya Muungano na kutoa mapendekezo ya kuboresha utekelezaji. Lakini pia ilitoa
mapendekezo ya baadhi ya mambo kuondolewa kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano,
kwa mfano bandari. Kwa upande mwingine Kamati ya Amina, pamoja na mambo
mengine, ilipendekeza mambo kumi na mbili yaondolewe kwenye Orodha ya Mambo ya
Muungano. Mambo hayo yalihusu uchumi.
118. Mwaka 1994, Serikali zote mbili zilikutana kutafakari mapendekezo ya
Kamati ya Shellukindo. Pamoja na mambo mengine muafaka ulifikiwa kuondoa au
kubadili baadhi ya mambo kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano.
119. Kwa kuwa mjadala juu ya Muundo wa Muungano ulikuwa unaendelea wakati
wote, Serikali ikaona ni busara kuunda Kamati ya Jaji Kisanga ambayo, pamoja na
mambo mengine, ilitakiwa kupendekeza aina ya Muundo wa Muungano. Kamati ya
Kisanga ilipendekeza muundo wa Serikali tatu. Pendekezo hili halikukubalika
lakini Muafaka wa 1994, kati ya Serikali zote mbili, uliendelea kutekelezwa
bila ya kufanya mabadiliko kwenye Katiba.
120. Katika kipindi chote hiki, kulikuwa na malalamiko kutoka kila upande.
Kwa upande wa Zanzibar baadhi ya malalamiko yalikuwa yafuatayo:
(i) Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Serikali ya Muungano ambalo
linaisaidia Tanganyika zaidi kuliko Zanzibar. Taswira hiyo imeifanya Tanganyika
kuwa ndiyo Tanzania na Watanganyika ndiyo waamekuwa Watanzania; na Wazanzibari
wamebaki kuwa Wazanzibari.
(ii) Mambo ya Muungano yamekuwa yakizidi kuongezeka na hivyo kuathiri uhuru
wa Zanzibar (Autonomy) na kufifisha hadhi ya Zanzibar (Identity);
(iii) Kuvunjwa kwa makubaliano ya Hati ya Muungano kwa kuificha sura ya
Tanganyika katika Muundo wa Serikali ya Muungano;
(iv) Kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano;
(v) Kutokuwepo kwa uwazi wa mapato na matumizi ya fedha za Serikali ya
Muungano;
(vi) Kutokuanzishwa kwa Akaunti ya Fedha ya Pamoja;
(vii) Kuwepo kwa mkanganyiko wa ugawaji wa mapato na jinsi ya kuchangia
gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano baina ya Serikali ya Muungano na
Serikali ya Zanzibar;
(viii) Kuwepo kwa chumi mbili tofauti zinazoshindana katika nchi moja;
(ix) Zanzibar kutoshirikishwa kikamilifu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
katika masuala ya kupata misaada na mikopo kutoka nje ya nchi;
(x) Malalamiko kuwa viongozi wakuu wa Zanzibar wanachaguliwa Dodoma na sio
Zanzibar kwenyewe;
(xi) Zanzibar kulalamika kuwa kuna baadhi ya mambo yamefanywa kuwa ya
Muungano kupitia kutungwa kwa sheria na Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mambo
yasio ya Muungano na baada ya hapo mambo hayo kupata hadhi ya Muungano;
121. Kwa upande wa Tanzania Bara, baadhi ya malalamiko yalikuwa yafuatayo:
(i) Zanzibar imekuwa nchi huru, ina bendera yake, ina wimbo wake wa Taifa,
ina Serikali yake na imebadili Katiba yake ili kujitambua kuwa ni nchi;
(ii) Zanzibar imebadili masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo
inasema sheria za Muungano zinazotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano
zitumike sehemu zote za Muungano, badala yake Katiba ya Zanzibar inaelekeza
kuwa ili Sheria itumike Zanzibar ni sharti ipelekwe mbele ya Baraza la
Wawakilishi. Maana yake ni kuwa, Katiba ya Zanzibar ipo juu ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano;
(iii) Zanzibar imetunga sheria kuhusu fedha ambalo ni suala lililo kwenye
madaraka ya Muungano;
(iv) Zanzibar imetunga Katiba ambayo imechukua madaraka ya Rais yaliyomo
katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano yanayoeleza kwamba Rais wa Jamhuri ya
Muungano ana madaraka ya kugawa nchi katika maeneo ya kiutawala. Mabadiliko ya
Kumi ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yameitambua Zanzibar kuwa ni nchi na
yanampatia mamlaka Rais wa Zanzibar kuigawa nchi katika maeneo ya kiutawala;
(v) Katiba ya Zanzibar inaeleza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi
mbili lakini Katiba ya Jamhuri ya Muungano inaeleza kwamba, Tanzania ni nchi
moja;
(vi) Masharti ya kikatiba yaliyowekwa na Katiba ya Zanzibar kuhusu mchango
wa Zanzibar katika uendeshaji wa Mambo ya Muungano yanapingana na masharti ya
Katiba ya Muungano.
(vii) Muundo wa Muungano uliopo umepoteza utambulisho wa kihistoria wa
Tanganyika na fursa ya watu wa Tanganyika kutetea maslahi yao ndani ya
Muungano;
(viii) Wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi
Zanzibar wakati wenzao wa upande wa Zanzibar wana haki ya kumiliki ardhi
Tanzania Bara;
(ix) Wabunge wa Zanzibar huchangia mijadala kwa mambo yasiyo ya Muungano na
ambayo kwa uhakika wake ni mambo ya Tanganyika na kwamba Wabunge wa Tanganyika
hawana nafasi ya kuchangia katika Baraza la Wawakilishi kwa mambo yasio ya
Muungano yanayohusu Zanzibar; na
(x) Kwa mujibu wa Sheria ya Mzanzibari, 1985, Watanzania ambao ni
Watanzania wa Bara hutakiwa kutimiza sifa maalum ili kuweza kupata haki za
kiraia huko Zanzibar ilhali Mzanzibari huweza kupata haki ya kiraia wakati
wowote na popote katika ardhi ya Tanganyika. Haki hizo za kiraia ni pamoja na
kugombea uongozi na kupiga kura.
Tanganyika kuvaa Koti la Muungano
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Mheshimiwa Mwenyekiti;
122. Tume iliamua kufanya uchambuzi wa kina kuhusu baadhi ya malalamiko,
hasa malalamiko ya Zanzibar. Malalamiko ya Tanzania Bara yanatokana, kwa
kiwango kikubwa, na hatua zilizochukuliwa kwa upande wa Zanzibar. Kama
malalamiko ya Zanzibar yakipatiwa ufumbuzi, malalamiko ya Tanzania Bara nayo
yatakuwa yamepatiwa ufumbuzi.
123. Katika kuchambua malalamiko ya Zanzibar kwamba Tanganyika imevaa koti
la Muungano, Tume imebaini kwamba muundo wa Muungano wa Serikali mbili
umeifanya Serikali ya Muungano, kwa kiwango kikubwa, kushughulikia zaidi mambo
ya Tanzania Bara, hasa mambo ya maendeleo. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano ya mwaka 1977, Serikali ya Muungano ina mamlaka ya kusimamia mambo ya
muungano na mambo yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanzania Bara. Kwa msingi
huo, Serikali ya Muungano inashughulikia sana mambo ya kilimo, elimu, afya,
maji, nishati na madini, ujenzi, uchukuzi, maliasili na utalii na mengine ya
Tanzania Bara ambayo siyo mambo ya Muungano.
124. Wakati wa kikao cha Bajeti, Bunge la Muungano hutenga siku mbili au
tatu za majadiliano kwa Wizara zinazosimamia mambo haya ya Tanzania Bara wakati
mambo ya Muungano kama vile ulinzi, mambo ya nje na mambo ya ndani hutengewa
siku moja au nusu siku. Sheria nyingi zinazotungwa na Bunge zinahusu mambo ya
Tanzania Bara. Maswali ya Wabunge kuhusu mambo ya maendeleo pia yanahusu
Tanzania Bara na ziara za Wabunge kukagua miradi ya maendeleo zinahusu Tanzania
Bara katika mambo yasiyo ya Muungano. Ndani ya Bunge, Mambo haya yanasimamiwa
na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye, kiuhalisia hana mamlaka wala
madaraka yoyote kuhusu Zanzibar na huwa hafanyi ziara Zanzibar kukagua shughuli
za maendeleo. Hali hii ndiyo imeifanya Tanganyika kuonekana imevaa koti la
muungano.
125. Hata Rais wa Jamhuri hafanyi ziara za kukagua miradi ya maendeleo na
kutoa ahadi kwa upande wa Zanzibar. Sura ya Serikali ya Muungano inaonyesha kuegemea
zaidi upande wa Tanzania Bara. Kati ya Wizara 24 ni wizara mbili tu ndizo
zinashughulikia mambo ya Muungano pekee. Wizara kumi zinashughulikia mambo ya
Tanzania Bara na Wizara kumi na mbili zinashughulikia mambo mchanganyiko ambayo
mengi ya mambo hayo yanahusu Tanzania Bara. Kwenye utawala, viongozi wakuu
wengi wa Wizara wanatoka Tanzania Bara. Hivi sasa ni Katibu Mkuu mmoja tu ndiye
anayetoka Zanzibar. Hali hii inatokana na ukweli kwamba Serikali ya Muungano
inashughulikia zaidi mambo yasiyo ya Muungano na ndiyo imeifanya Tanganyika
kuonekana imevaa koti la Muungano.
126. Tume imeona hakuna njia ya kubadili hali hii kwa sababu Serikali ya
Muungano haina mamlaka ya kutosha juu ya mambo ya maendeleo kwa upande wa
Zanzibar. Mawaziri na Serikali kwa ujumla, wanalazimika kupanga maendeleo na
kutafuta rasilimali kwa ajili ya Tanzania Bara kuliko kwa Zanzibar. Zanzibar
hufanya mipango yake ya maendeleo, lakini, ili kupata rasilimali kama mikopo na
misaada, ni lazima Serikali ya Zanzibar ipitie Serikali ya Muungano, jambo
ambalo utekelezaji wake umesababisha matatizo mengi.
127. Njia pekee ambayo ingefanya maendeleo ya Zanzibar yapewe uzito sawa na
mambo ya Tanzania Bara ni kuyaweka mambo yote ya Zanzibar chini ya Serikali ya
Muungano, yaani kuwa na Serikali Moja. Lakini kama nilivyosema, wakati wa
kukabidhi Rasimu kwa Marais wetu, Muundo wa Serikali Moja una changamoto nzito.
Waasisi waliona matokeo ya Muundo huo ni Zanzibar kumezwa na Tanganyika. Tume
ilipokuwa inakusanya maoni, wananchi wengi, hasa Zanzibar, walionyesha hofu
hiyo ni kubwa sana hivi sasa kuliko ilivyokuwa mwanzoni. Kwa hiyo, tathmini ya
Tume ni kwamba Muundo wa Serikali moja hauna uhalisia.
Kuongezeka kwa Mambo ya Muungano
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Mheshimiwa Mwenyekiti;
128. Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kutoka Zanzibar kwamba
kuongezeka kwa mambo ya Muungano kunapunguza mamlaka ya Zanzibar. Katika
mihadhara mingi iliyofanywa Zanzibar muda mfupi kabla Tume kuanza kazi, baadhi
ya watoa mada walitumia mizani kuonyesha jinsi ongezeko la mambo ya Muungano
linavyoathiri mamlaka na hadhi ya Zanzibar.
129. Tume imefanya uchambuzi wa kina kuhusu malalamiko haya. Tangu mwanzo
wa Muungano, ilikubalika kwamba Zanzibar ibaki na hadhi yake na iwe na madaraka
kuhusu Mambo yasiyo ya Muungano. Tume ilifanya uchambuzi wa Mambo ya Muungano
ili kubaini kama yanaingilia hadhi na mamlaka ya Zanzibar. Kati ya Mambo 22 ya
Muungano, Tume imebaini kuwa siyo mambo yote yanatekelezwa kikamilifu
kimuungano. Mambo mengi yamebadilishwa bila ya kubadili katiba, ama kwa
makubaliano kati ya pande zote mbili za Muungano au kwa hatua zilizochukuliwa
na upande mmoja. Mambo ambayo hayatekelezwi kimuungano ni bandari, leseni za
viwanda, utafiti, takwimu, biashara ya nje na maliasili ya mafuta na gesi.
Lakini kuna mambo mengine mengi ambayo hayatekelezwi kikamilifu. Kwa mfano,
mambo yanayohusu uhusiano wa kimataifa, ulinzi, uchukuzi, Mahakama ya rufani,
usafiri wa anga, kodi, posta, simu na uraia.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
130. Katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita, kamati nyingi zimeundwa
kushughulikia matatizo ya muungano na baadhi yake zilipendekeza kuondoa mambo
mengi zaidi kutoka kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano. Kwa mfano, Kamati ya
Amina ilipendekeza mambo yafuatayo yaondolewe kwenye Orodha ya Mambo ya
Muungano:
(i) Kodi ya mapato;
(ii) Mikopo;
(iii) Misaada;
(iv) Uhusiano wa Kimataifa;
(v) Fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za
kigeni;
(vi) Mabenki (pamoja na mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za
mabenki isipokuwa Benki Kuu ya Tanzania);
(vii) “off-shore Banking” na utanganzaji wa maeneo huru ya uchumi na mambo
yanayohusiana nayo;
(viii) Leseni za viwanda;
(ix) Bandari;
(x) Usafiri wa Anga;
(xi) Tawimu (isipokuwa Sensa); na
(xii) Biasahara ya nje (isipokuwa Bodi ya Biashara ya Nje).
131. Mwaka 2003, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliunda kamati nyingine
Kuchambua Matatizo na Kero za Muungano na Taratibu za Kuziondoa.” Kamati hiyo
ilipendekeza mambo yafuatayo yaondolewe kwenye
Orodha ya Mambo ya Muungano:
(i) Mafuta na gesi asilia;
(ii) Elimu ya Juu;
(iii) Posta;
(iv) Simu (mawasiliano);
(v) Biashara ya nje;
(vi) Kodi ya mapato;
(vii) Ushuru wa bidhaa;
(viii) Usafiri wa anga;
(ix) Takwimu;
(x) Utafiti;
(xi) Ushirikiano wa kimataifa;
(xii) Leseni za viwanda;
(xiii) Polisi; na
(xiv) Usalama.
132. Kama mambo haya yote yataondolewa kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano
basi Serikali ya Muungano itakuwa imebaki na mambo ya Tanzania Bara tu kwa
upande wa maendeleo.
133. Tume ilitafakari kama kuna uwezekano wa kuyarudisha mambo
yaliyoondolewa kwenye orodha kufuatia muafaka wa 1994, lakini tathmini ya Tume
ni kwamba kufanya hivyo ni kuzua mgogoro upya kwani itaonekana mamlaka
(autonomy) ya Zanzibar yanaingiliwa. Wakati Tume ilipokuwa inakusanya maoni,
wananchi wengi wa Zanzibar kutoka makundi yote mawili, yaani wale waliotaka
Muungano wa Serikali Mbili na wale waliotaka Muungano wa Mkataba, wote
walipendekeza mambo mengi yaondolewe kwenye Orodha ya Muungano. Wale waliotaka
Muungano wa Mkataba walitaka mambo yote yaondolewe kwenye Orodha ya Mambo ya
Muungano isipokuwa suala la ulinzi. Wale waliotaka Muundo wa Serikali mbili
walitaka mambo yote ya uchumi yaondolewe kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano.
Katika hali hiyo, kuyarudisha mambo ambayo hivi sasa yako chini ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, hata kama siyo kikatiba, kunaweza kuleta mgogoro wa
kisiasa.
Mgongano wa Katiba
Mheshimiwa Mwenyekiti
Mheshimiwa Mwenyekiti
134. Eneo jingine lenye matatizo ni mgongano kati ya Katiba ya Muungano na
Katiba ya Zanzibar. Ibara ya 132 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 imeweka
masharti kwamba sheria zinazotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano
hazitatumika Zanzibar hadi zipelekwe kwenye Baraza la Wawakilishi.
135. Jambo hili limeleta mgongano wa Katiba. Juhudi zilizofanywa na pande
zote mbili hazikufanikiwa kuondoa mgongano huo. Katika muafaka wa mwaka 1994
Serikali zote zilikubaliana kwamba Zanzibar ifanye mabadiliko kwenye Katiba
yake ili mgongano huu wa Katiba uondolewe. Lakini hadi sasa muafaka
haujatekelezwa. Zaidi ya hapo, mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar katika Ibara ya
kwanza yaliyofanywa mwaka 2010 yametamka wazi kwamba Zanzibar ni nchi kati ya
nchi mbili zinazounda Muungano wakati Katiba ya Jamhuri inaelekeza kwamba
Tanzania ni Nchi moja.
136. Mabadiliko katika Katiba ya Zanzibar pia yamehamisha baadhi ya
madaraka ya Serikali ya Muungano kwenda Zanzibar. Kwa mfano, Katiba ya Jamhuri
inampa Rais wa Jamhuri madaraka ya kuigawa nchi katika maeneo. Lakini Katiba ya
Zanzibar imeyahamisha madaraka hayo kwenda kwa Rais wa Zanzibar.
137. Wakati wa kukusanya maoni ya wananchi, Tume ilibaini kwamba haitakuwa
rahisi kubadili Katiba ya Zanzibar kuifanya Zanzibar kuonekana kuwa sehemu ya
Jamhuri ya Muungano badala ya kuwa na sura ya nchi. Mabadiliko ya aina hiyo
yatahitaji kura ya maoni kama Katiba ya Zanzibar inavyoelekeza. Kwa tathmini ya
Tume, baada ya kuwasikiliza wananchi wa Zanzibar, ni dhahiri kwamba uwezekano
wa kufanya mabadiliko kwenye Katiba ya Zanzibar ili Zanzibar iwe sehemu ya nchi
moja badala ya kuwa nchi, ni mdogo sana.
Michango, Gharama za Muungano na Mgao wa Mapato
Mheshimiwa Mwenyekiti
Mheshimiwa Mwenyekiti
138. Matumizi ya fedha na rasilimali za Muungano, mchango wa pande zote
mbili kwa shughuli za Muungano na mgao wa mapato ya muungano yamekuwa ni
masuala yenye utata kwa muda mrefu. Katika jitihada za kupata ufumbuzi wa
tatizo hili, mwaka 1977 Halmashauri Kuu ya CCM ilitoa uamuzi kwamba mapato ya
kodi za muungano yabaki upande wa muungano yanapokusanywa. Kwa msingi huo,
mapato ya kodi za muungano yanayokusanywa Zanzibar yabaki kwenye Hazina ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na yatumike Zanzibar badala ya kupelekwa
kwenye Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano; na yale mapato ya kodi za
Muungano yanayokusanywa Tanzania Bara yabaki kwenye Hazina ya serikali ya
Jamhuri ya Muungano na yatumike Tanzania Bara. Halmashauri Kuu pia ilibadili
utaratibu wa kuchangia. Hata hivyo uamuzi huu haukumaliza matatizo.
139. Zanzibar kwa upande wake imekuwa ikidai kwamba fedha na rasilimali za
Muungano zinatumika na kuinufaisha Tanzania Bara chini ya kivuli cha muungano.
Aidha, kwa upande wa Serikali ya Muungano inadaiwa kwamba Tanzania Bara ndiyo
inayochangia fedha na rasilimali nyingi katika muungano hivyo inayo haki ya
kutumia fedha na rasilimali hizo kwani Zanzibar kwa muda mrefu imekuwa
haichangii katika fedha na rasilimali hizo za muungano.
140. Kutokana na matatizo hayo, chombo maalum cha kikatiba (Tume ya Pamoja
ya Fedha) kilianzishwa ili kushughulikia masuala ya uhusiano wa kifedha baina
ya Serikali ya Muungao na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
141. Tume ya Pamoja ya Fedha ilianzishwa chini ya Ibara ya 134 ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 kufuatia marekebisho ya Katiba yaliyofanywa
mwaka 1984. Kwa mujibu wa Katiba majukumu makubwa ya Tume ni:
(i) Kuchambua mapato na matumizi yanayotokana na, au yanayohusu utekelezaji
wa Mambo ya Muungano na kutoa mapendekezo kwa Serikali mbili kuhusu mchango na
mgawo wa kila mojawapo ya Serikali hizo;
(ii) Kuchunguza kwa wakati wote mfumo wa shughuli za fedha za Jamhuri ya
Muungano na pia uhusiano katika mambo ya kifedha kati ya Serikali mbili; na
(iii) Kutekeleza majukumu mengine ambayo Rais ataipatia Tume au kama Rais
atakavyoagiza, na kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.
142. Ibara ya 134 inaelekeza pamoja na mambo mengine, kutungwa kwa sheria
itakayoweka utaratibu juu ya uteuzi wa Wajumbe wa Tume na namna Tume itakavyotekeleza
majukumu yake. Baada ya takriban miaka kumi na mbili kupita, yaani mwaka 1996,
ndipo ilipotungwa Sheria ya Tume ya Pamoja ya Fedha.
143. Miaka saba baada ya kupitishwa Sheria ya Tume ya Pamoja ya Fedha au
kwa maana nyingine miaka kumi na tisa baada ya Katiba kuianzisha Tume hiyo,
Wajumbe wa kwanza wa Tume waliteuliwa mwaka 2003.
144. Ripoti ya kwanza ya Tume ya Pamoja ya Fedha ilitolewa mwaka 2006
ambayo ilihusu mchango wa gharama za matumizi na mgao wa mapato ya muungano.
Katika Ripoti hiyo, Tume ilipendekeza kiwango cha uchangiaji, utaratibu wa kila
Serikali kuchangia gharama za muungano na kiwango cha mgao na utaratibu wa
mgawanyo wa mapato ya muungano baina ya Serikali hizo. Aidha, Tume ya Pamoja ya
Fedha ilipendekeza kwamba masharti ya Katiba yatekelezwe kwa kuanzishwa kwa
Akaunti ya Fedha ya Pamoja ambapo fedha yote inayohusu gharama za muungano
zitawekwa.
145. Hadi sasa, huu ni mwaka wa nane tokea mapendekezo hayo kutolewa,
hakuna hata moja kati ya mapendekezo hayo lililotekelezwa au kuchukuliwa hatua.
Kwa taarifa ambazo Tume ilipewa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imeshayajadili mapendekezo hayo na kutoa msimamo wake. Serikali ya Muungano
imekuwa ikieleza kwamba imo katika hatua ya kuyafanyia kazi na kutafuta namna
bora ya kuyatekeleza mapendekezo hayo lakini bado haijatoa maoni yake kuhusu
mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya Fedha.
146. Tatizo hili ni kubwa sana. Serikali ya muungano ndiyo ina uwezo wa
kushughulikia mambo ya fedha kwa nchi. Serikali hiyo ina madaraka ya kutoza
kodi na kutafuta mikopo na misaada kutoka nje. Serikali ya Zanzibar haina
madaraka hayo bali ni lazima ipitie kwenye Serikali ya muungano. Mgao sahihi wa
mapato ya kodi, mikopo na misaada ungeleta nafuu kubwa kwa Zanzibar katika
kuendesha mambo yake na Akaunti ya Fedha ya Pamoja ingeweka wazi mapato na
matumizi kwa mambo ya muungano.
147. Hivi sasa, ni miaka thelathini tangu Katiba ilipoianzisha Tume ya
Pamoja ya Fedha, ni miaka kumi na nane tangu Sheria ya Kuanzisha Tume ya Pamoja
ya Fedha ilipotungwa, na ni miaka kumi na moja tangu Tume hiyo ilipoundwa. Ni
miaka minane tangu Tume ya Pamoja ya Fedha ilipotoa mapendekezo ya kiwango cha
uchangiaji, utaratibu wa kuchangia, kiwango cha mgao na utaratibu wa mgawanyo
wa mapato ya muungano. Zaidi ya hapo hadi sasa Akaunti ya Fedha ya Pamoja
haijaanzishwa.
148. Tathmini ya Tume ni kwamba siyo rahisi mambo haya kutekelezwa chini ya
muundo wa Serikali mbili. Hii ni kwa sababu, Wizara za Serikali ya Muungano ni
mchanganyiko. Zipo wizara ambazo zinashughulikia mambo ya Muungano tu na zipo
wizara zinazoshughulikia mambo ya Tanzania Bara pekee. Aidha, zipo wizara
zinazoshughulikia mambo mchanganyiko, yaani mambo ya Muungano na Mambo yasiyo
ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara. Katika mazingira hayo, haiwezekani
kujua kwa uhakika gharama zipi ni za Mambo ya Muungano na zipi ni za Mambo
yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara.
149. Wizara zinazoshughulikia mambo mchanganyiko ni pamoja na Ofisi ya
Rais, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Katiba na Sheria,
Wizara ya Fedha, Wizara ya Elimu na Vyuo vya Ufundi, Wizara ya Mawasiliano,
Wizara ya Biashara na Viwanda, Wizara ya Nishati na Madini Wizara ya Uchukuzi
na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Katika hali hiyo ni vigumu kujua
kwa mfano ni gharama zipi za shughuli za Rais ni za Muungano na zipi ni za
Tanzania Bara.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
150. Mambo manne niliyoyaeleza ndiyo msingi wa kupendekeza muundo wa
Serikali tatu. Kwa muda mrefu Zanzibar imelalamika kwamba Tanganyika imejificha
kwenye koti la Muungano na ndiyo inafaidi. Pamoja na kwamba kuna mawaziri na
wabunge wanaotoka Zanzibar, Serikali ya Zanzibar imekuwa inalalamika kwamba
haishirikishwi kwenye maamuzi ya Muungano. Hata wakati ambapo Rais ametoka
Zanzibar haitoshi kuona kama Zanzibar ni sehemu ya Serikali ya Muungano.
151. Wakati Tume ilipokuwa inakusanya maoni ilikuwa jambo la kawaida
kusikia wananchi wa Zanzibar, na hata viongozi wao, wakizungumzia Serikali ya
Bara badala ya Serikali ya Muungano.
152. Orodha ya mambo ya Muungano ni suala ambalo pia limelalamikiwa kwa
muda mrefu na hatua zilizochukuliwa ni kuyapunguza mambo ya Muungano, ikiwa ni
pamoja na yaliyoorodheshwa kwenye makubaliano ya Muungano (Articles of Union).
Kwa mfano Bandari na Biashara ya Nje. Suala la mahusiano ya kifedha nalo
limekuwa na utata kwa muda wa karibu miaka arobaini. Kiini chake ni malalamiko
ya kutoka kila upande kuhusu nani anafaidi rasilimali za taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
153. Azimio la Halmashauri Kuu ya CCM la 1994, lililenga kubaki na Muundo
wa Serikali mbili kwa lengo la kwenda kwenye Muundo wa Serikali moja. Lengo la
uamuzi huu ilikuwa kuzuia madai ya Serikali tatu ambayo yalikuwa yanatolewa na
pande zote mbili. Lakini hatua zilizochukuliwa, tena kuanzia mwaka huo huo,
zilikuwa zinaelekea kwenye muundo wa Serikali tatu.
154. Mwaka 1994, Serikali zote mbili zilifikia muafaka kuondoa mambo mengi
kutoka kwenye orodha ya Muungano. Katiba ya Zanzibar imebadilishwa kwa msingi
wa kutambua nchi mbili zinazounda Muungano. Mwelekeo wa hatua hizo siyo kwenda
kwenye Muundo wa Serikali moja bali kwenda Serikali tatu.
155. Ripoti ya 2003 iliyotayarishwa na Kamati ya kuchambua “Matatizo na
Kero za Muungano na Taratibu za Kuziondoa,” iliyoundwa na Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar, inaeleza kwamba;
“Matatizo makubwa yaliopo kwa upande wa sheria ni kuwa Zanzibar haina kauli juu ya Sheria zinazohusu mambo ya Muungano. Kwa mujibu wa Katiba ya Muungano, sheria zote hupitishwa kwa wingi wa kura isipokuwa sheria ya marekebisho ya Katiba na sheria kuhusu mambo yaliyoelezwa katika Jedwali la Pili, Orodha ya pili. Mambo hayo ni 8 tu na kati ya hayo 5 tu ndio mambo ya Muungano.
Kutokana na kasoro hii, wananchi wa Zanzibar wamekosa haki ya msingi ya kujitawala nayo ni ya kupitisha sheria kwa ridhaa yao. Hii ni kasoro kubwa sana katika mfumo wowote ule wa utawala. Kwa upande mwingine, wananchi wa Tanzania Bara nao wanalalamika kwamba Wabunge wa Zanzibar wanashiriki katika kuamua mambo ya Bara ambayo si ya Muungano. Ni ukweli ulio wazi kwamba mchango wa Wabunge wa Zanzibar katika mambo ambayo si ya Muungano ni mdogo mno kama upo.
Kwa sababu zilizoelezwa hapo juu Kamati inapendekeza njia mbili muhimu zifuatazo:-
“Matatizo makubwa yaliopo kwa upande wa sheria ni kuwa Zanzibar haina kauli juu ya Sheria zinazohusu mambo ya Muungano. Kwa mujibu wa Katiba ya Muungano, sheria zote hupitishwa kwa wingi wa kura isipokuwa sheria ya marekebisho ya Katiba na sheria kuhusu mambo yaliyoelezwa katika Jedwali la Pili, Orodha ya pili. Mambo hayo ni 8 tu na kati ya hayo 5 tu ndio mambo ya Muungano.
Kutokana na kasoro hii, wananchi wa Zanzibar wamekosa haki ya msingi ya kujitawala nayo ni ya kupitisha sheria kwa ridhaa yao. Hii ni kasoro kubwa sana katika mfumo wowote ule wa utawala. Kwa upande mwingine, wananchi wa Tanzania Bara nao wanalalamika kwamba Wabunge wa Zanzibar wanashiriki katika kuamua mambo ya Bara ambayo si ya Muungano. Ni ukweli ulio wazi kwamba mchango wa Wabunge wa Zanzibar katika mambo ambayo si ya Muungano ni mdogo mno kama upo.
Kwa sababu zilizoelezwa hapo juu Kamati inapendekeza njia mbili muhimu zifuatazo:-
1) Bunge la Jamhuri ya Muungano lipitishe mambo yake kwa utaratibu wa idadi
maalum ya Wabunge kutoka pande zote mbili. Kama ni sheria inayohitaji
kupitishwa kwa “simple majority” iwe ni ya kila upande au sheria inayohitaji
masharti ya theluthi mbili iwe ni kwa kila upande.
2) Bunge la Jamhuri ya Muungano liwe na mabaraza mawili: Baraza la Juu na
Baraza la Chini. Baraza la Juu lipitishe mambo ya Muungano na Baraza la Chini
lipitishe masuala ya Tanzania Bara.”
156. Baraza la Wawakilishi la Zanzibar nalo limetoa mapendekezo ambayo kwa
tafsiri yake yanaelekea kupendekeza muundo wa Serikali Tatu. Katika Waraka
uliowasilishwa kwenye Tume mwezi Februari 2013, pamoja na mambo mengine, Baraza
la Wawakilishi lilitoa maoni yafuatayo:
“Kwa sababu Wazanzibari ni waumini wa Muungano ambao haukuondoa na
hautoondoa uwepo wa Zanzibar kama nchi, ni vyema Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ijayo iweke wazi kuwa Tanzania ni Jamhuri ya Muungano inayotokana
na Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Hali hii itahakikisha
kuwepo na maeneo maalum ya mamlaka ambayo Zanzibar ina uwezo nayo kama nchi
(yaani, Mamlaka ya Dola ya Zanzibar).
Kwa sababu inapendekezwa kuwepo na Mamlaka ya Zanzibar huru na Mamlaka ya
Tanganyika huru ndani ya Jamhuri ya Muungano, Mamlaka ya Muungano iwekwe wazi –
maeneo yake, uwezo au nguvu zake, na utendaji wake. Mambo yote hayo yawekwe
wazi na mipaka yake.
Uwepo wa Muungano uonekane katika hali zote – uundwaji wa Mamlaka za
Muungano, ufanyaji kazi katika Mamlaka za Muungano, ufanyaji wa maamuzi katika
Mamlaka za Muungano, na uingizwaji na upunguzwaji katika orodha wa mambo ya
Muungano.
Kwa mfano, maamrisho kama yaliyopo sasa kwenye Ibara ya 64(4) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, ambayo yanawezesha jambo kufanywa la
Muungano bila ya kuishirikisha katika maamuzi Mamlaka ya Zanzibar, yasiwe na
nafasi tena ya kutokea kwa mujibu wa Katiba ijayo ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Utungaji wa sera na sheria za Muungano isiwe ni jambo la kuzingatiwa na
kutekelezwa na Mamlaka za Muungano pekee. Kama tulivyoelezea hapo awali kuwa
uwepo ushirikishwaji wa sehemu (Dola) mbili huru katika kufanya maamuzi na
uendeshaji wa Mamlaka ya Muungano. Ushirikishwaji huo ni lazima udhihirike
katika maamuzi yatakayopelekea kuundwa kwa sera na sheria zote za mambo ya
Muungano.
Jambo kubwa zaidi ya yote linalohitajika lionekane kwa maneno (maamrisho ya
Katiba) na vitendo ni haja ya kuwa na Muungano wa kweli, hata kama ni kwa
maeneo machache, kwa dhati ya wanasiasa na watanzania kwa jumla. Hali hii
inaweza kupatikana kwa kuzingatia Misingi ya Katiba iliyoainishwa hapo juu
ambayo yanaweka mkazo juu ya haki na maslahi ya pande mbili za Muungano ya
kujiamulia hatma za mambo yao yote, ya kiuchumi, ya kijamii na ya kisiasa.
Kuhusu muundo unaohitajika katika Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano,
Baraza la wawakilishi halikufikia maamuzi maalum. Katika mtazamo wa Baraza kama
taasisi, Muungano wa Tanzania unaweza kuchukua muundo wowote kwa kuzingatia
misingi ya Katiba iliyoelezewa hapo juu”.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
157. Kwa Tahmini ya Tume, Muundo wa Serikali mbili hauwezi kubaki kwa hali
ya sasa. Muungano wa Serikali mbili waliotuachia waasisi siyo uliopo sasa.
Umebadilishwa mara nyingi, wakati mwingine bila ya kufanya mabadiliko kwenye
Katiba. Waasisi walituachia Muungano wa Nchi Moja yenye Serikali Mbili, na siyo
Nchi Mbili zenye Serikali Mbili. Muundo wa Serikali Mbili unaweza kubaki tu
kama orodha ya mambo ya muungano haitapunguzwa bali itaongezwa. La sivyo,
Serikali ya Muungano itabaki na rasilimali na mambo ya Tanzania Bara tu. Katika
hali hiyo, pande zote mbili zitaendelea kulalamika. Kwa upande, mmoja Zanzibar
itaendelea kulalamika kwamba Tanzania Bara imevaa koti la Muungano kwa faida
yake, na kwa upande mwingine, Tanzania Bara itaendelea kulalamika kwamba mambo
yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara na rasilimali zake ndizo zimekuwa Muungano.
158. Kwa kipindi cha miaka thelathini, kumekuwepo hoja za muundo wa
Serikali tatu. Chanzo cha kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar
ilikuwa ni hoja ya muundo wa Serikali tatu. Tume ya Jaji Nyalali ilikuwa na
hoja hiyo. Hoja ya G 55 ilikuwa ni kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika. Kamati
ya Jaji Kisanga nayo ilipendekeza muundo wa Serikali tatu. Tume pia imepata
hoja hiyo kutoka kwa wananchi wakati wa kuratibu na kukusanya maoni.
159. Lakini la muhimu zaidi ni kwamba matendo katika kipindi hicho cha
miaka thelathini. Hatua ambazo zimechukuliwa zimefanya mamlaka na madaraka ya
Serikali ya Muungano yapungue sana na mamlaka na madaraka ya Zanzibar
kuongezeka. Vivyo hivyo, mamlaka ya Zanzibar yameongezeka kiasi kwamba Serikali
ya Muungano imebaki ikishughulikia mambo ya Tanzania Bara tu kwa upande wa
maendeleo.
160. Jambo kubwa zaidi katika kuchukua hatua hizi ni kuvunjwa kwa Katiba.
Hili siyo jambo dogo. Kama Katiba haitaheshimiwa nchi haitakuwa salama.
Mapendekezo ya Tume yanalenga kuondoa matatizo yanayohatarisha kuyumba kwa
muungano, ili kuzuia pande zote mbili kuendelea kuchukua hatua zinazovunja
Katiba.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
161. Muundo wa Serikali tatu haupunguzi uimara wa Muungano. Muungano huu
siyo Muungano wa Serikali ama Viongozi bali ni muungano wa nchi mbili kwa
manufaa ya wananchi. Faida kubwa iliyopatikana katika miaka hamsini iliyopita
ni kuungana kwa wananchi.
162. Njia kuu ya kuimarisha muungano ni kuzingatia haki za raia. Kudumu na
kuimarika kwa muungano kunategemea jinsi wananchi wanavyofaidika katika juhudi
zao za kujiletea maendeleo.
163. Rasimu imependekeza uraia mmoja. Rasimu pia imependekeza orodha ndefu
ya haki za binadamu. Lengo la mapendekezo haya ni kumwezesha mwananchi kupata
haki zake kama raia bila vikwazo. Kisiasa atakuwa na haki ya kwenda mahali
popote katika nchi na kushiriki katika shughuli za utawala bila kujali asili
yake ni upande upi wa nchi. Kama anataka kugombea nafasi yoyote mahali
anapoishi awe na haki hiyo. Awe pia na haki ya kupiga kura ya kumchagua
mwenyekiti wa kijiji, au mtaa, diwani, mbunge na rais.
164. Kiuchumi, bila kujali orodha ya Mambo ya Muungano, raia awe na haki ya
kufanya shughuli zake bila ubaguzi. Kama anahitaji ardhi apewe kama raia bila
kikwazo cha asili yake. Hivyo hivyo, katika kufanya biashara na katika kupata
ajira, mwananchi asizuiwe kufanya kazi mahali popote alipo kwa sababu ya asili
yake.
165. Kijamii, mwananchi ana haki ya kupata huduma popote alipo bila kujali
asili yake. Kwa mfano, ingawa elimu siyo suala la Muungano, mwananchi awe na
haki yake kama raia kupata elimu mahali popote na kwa ngazi yoyote. Huduma ya
afya nayo iwe hivyo hivyo. Kama kuna ulazima wa mwananchi kuhamishiwa hospitali
ya upande mmoja wa muungano kwenda hopitali ya upande mwingine wa muungano,
mwananchi huyo apewe haki yake kama raia. Kama kukitokea ubaguzi wa raia
kinyume na haki za uraia wananchi wataanza kulalamika na kubaguana wenyewe kwa
wenyewe. Likitokea hilo, muungano wa muundo
wowote ule utayumba. Hivyo, ni jambo la lazima Serikali zote kulinda kikamilifu haki za raia.
wowote ule utayumba. Hivyo, ni jambo la lazima Serikali zote kulinda kikamilifu haki za raia.
Muundo wa Serikali Tatu
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Mheshimiwa Mwenyekiti;
166. Muundo wowote wa Serikali utakuwa na changamoto zake. Waasisi waliona
changamoto za Serikali moja, yaani Zanzibar kumezwa na Tanganyika. Hali ni hiyo
hadi sasa. Muundo wa Serikali Mbili umekuwa na changamoto nyingi ambazo
zimekuwa kero na msingi wa malalamiko mengi kuhusu muungano, na hata Katiba
kuvunjwa.
167. Kwa maana hiyo, Muundo wa Serikali tatu utakuwa na changamoto zake.
Moja ni gharama kuongezeka. Ongezeko hilo halitakuwa kubwa sana kama
inavyofikiriwa. Gharama kubwa kwa shughuli za Muungano ni katika eneo la ulinzi
na usalama, yaani jeshi la wananchi, polisi, usalama wa taifa na mambo ya nje.
Gharama hizo hazibadiliki, zinabaki zile zile bila kujali kama ni Muundo wa
Serikali Mbili au Serikali Tatu. Gharama zitaongezeka kwenye utawala. Tume ililiona
hilo na ndiyo maana imependekeza Serikali ndogo.
168. Bunge lililopendekezwa katika Rasimu ya Katiba nalo ni dogo. Hivi
sasa, Bunge la Muungano lina wabunge 357 na Baraza la Wawakilishi Zanzibar lina
Wawakilishi 81, jumla ni 438. Wabunge wanaotoka Zanzibar ni 77 ambao
wasipokuwepo kwenye Bunge la Muungano watabaki wabunge 280 wa Tanganyika.
Wabunge wa mabunge matatu watakuwa ni wachache kuliko wajumbe wa mabunge mawili
ya sasa. Tume inategemea mabunge ya Nchi Washirika yatapunguza wabunge wake ili
kupunguza gharama, hasa wabunge wa kuteuliwa.
Hivi sasa, Wabunge wa kuteuliwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ni 10,
ukiongeza na Wajumbe 5 wa Baraza la Wawakilishi wanakuwa jumla 15. Wajumbe wa
kuteuliwa katika Baraza la Wawakilishi nao ni 10. Hivyo, jumla ya Wajumbe wote
hao ni 25. Kwa kufuata mapendekezo ya Rasimu ya Katiba, upo uwezekano mkubwa
kupunguza idadi wa Wabunge katika Mabunge ya Nchi Washirika na hatimaye
kupunguza gharama za kuendesha Mabunge hayo.
169. Gharama zitakazoongezeka ni za kawaida ambazo haziwezi kuepukika
inapokuwa ni lazima kuleta ufanisi wa mfumo wa utawala katika mazingira ya
muungano wa nchi zilizokuwa huru hapo mwanzoni. Lakini pia, tangu Muungano
uundwe, kila Serikali kati ya Serikali zetu mbili, zimekuwa zikiongeza wizara,
mikoa, wilaya na taasisi mbali mbali za kiutawala ili kuleta ufanisi na hivyo
kuongeza matumizi ya Serikali. Hivyo, suala la kuongezeka kwa matumizi ni suala
la lazima katika kuongeza ufanisi hasa katika enzi hizi za ushiriki zaidi wa
wananchi. Vilevile, ni suala la kawaida kuendana na kukua kwa majukumu, dhamana
na ukubwa wa nchi.
170. Suala la matumizi katika mfumo wa Serikali zetu ni suala la utamaduni
wa matumizi kuliko kuwa suala la muundo wa muungano. Katika Rasimu, Tume
imependekeza mfumo ambao utaweza kudhibiti na kujenga nidhamu ya matumizi ya
fedha na mali za umma. Kwa kuwa Katiba za Nchi Washirika zinapaswa kufuata
misingi iliyomo katika Katiba ya Muungano, basi ni wazi mfumo mpya wa kikatiba
utajenga mazingira yatakayowezesha kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa
Serikali zote tatu pamoja na kuziba mianya ya matumizi yasiyo na tija kwa
taifa, ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha matumizi makubwa katika kuendesha
Serikali zetu.
171. Changamoto ya pili ni uhakika wa mapato kwa Serikali ya muungano. Tume
imependekeza kodi ya bidhaa iwe ya muungano, na pia mapato yasiyo ya kodi,
mikopo na michango ya Nchi Washirika.
172. Ushuru wa bidhaa utakidhi sehemu kubwa ya gharama za muungano. Sehemu
inayobaki itachangiwa na nchi washirika. Utaratibu na viwango vya michango
utawekwa na bila shaka utaratibu huo utazingatia ukubwa wa uchumi, idadi ya
watu na ukubwa wa eneo. Katika muungano wowote ule, mchango unategemea, pamoja
na mambo mengine, uwezo na wakati wote uchumi mkubwa unaubeba uchumi mdogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
173. Changamoto nyingine ni nchi mojawapo kutenda kinyume na Katiba ya
muungano. Lakini hili halitokani na muundo. Chini ya muundo huu wa Serikali
mbili, Katiba imevunjwa. Tume imeona hilo na ndiyo maana imependekeza utaratibu
wa kuzuia hilo, ikiwa ni pamoja na kuanzisha Tume ya Uhusiano na Uratibu pamoja
na kuipa madaraka Mahakama ya Juu kuamua migogoro.
174. Kwa upande wa matatizo ya kiutendaji Tume imependekeza muundo wa
Serikali tatu ujengwe kwenye misingi minne ya utendaji. Misingi hiyo ni muungano
wa hiyari, ushirikiano, mshikamano na kutegemeana.
175. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya
Tanganyika na iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Msingi wa Muungano huu ni
Makubaliano ya Muungano (Articles of Union) ya mwaka 1964 yaliyofikiwa baina ya
mataifa haya mawili. Chini ya makubaliano hayo, mataifa hayo yalikubaliana kwa
hiyari kuachia baadhi ya mamlaka na kuyapeleka mamlaka hayo kwenye Serikali ya
Muungano. Uhiyari huu wa kukubali kuungana kwa mataifa haya mawili ni moja ya
misingi ya utekelezaji wa muundo wa Muungano unaopendekezwa wa Serikali Tatu.
Ibara ya 1 (3) ya Rasimu ya Katiba inapendekeza, pamoja na mambo mengine, Hati
ya Muungano iwe ni msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
176. Msingi mwingine wa utendaji katika muundo wa Serikali Tatu ni
Ushirikiano. Chini ya msingi huu, Serikali ya Muungano na Serikali za Nchi
Washirika zitakuwa na ushirikiano baina yao katika shughuli zote za utendaji na
uendeshaji wa nchi ili mradi ushirikiano huo haukiuki Katiba. Ibara ya 65(1)
inapendekeza kuwa Nchi Mshirika inaweza kuomba ushirikiano kutoka Serikali ya
Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kufanikisha uhusiano wake wa kikanda na
kimataifa. Aidha, Ibara ya 66 inapendekeza masharti kuhusu ushirikiano kati ya
Nchi Washirika zenyewe na baina ya Nchi hizo na Serikali ya Muungano kwa lengo
la kukuza na kulinda maslahi ya Taifa na kukuza maendeleo ya wananchi.
177. Katika mfumo wa Serikali Tatu, uratibu wa uhusiano baina ya Serikali
hizo ni moja ya misingi muhimu. Ibara ya 67 inapendekeza kuwepo kwa Waziri
Mkaazi atakayeteuliwa na kila Nchi Mshirika atakayefanya kazi akiwa Makao Makuu
ya Serikali ya Muungano. Moja ya majukumu ya msingi ya Waziri Mkaazi ni
kuratibu uhusiano baina ya Serikali yake na Serikali ya Muungano. Aidha, Ibara
ya 109 inapendekeza kuanzishwa kwa Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali
chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais. Kuwepo kwa uratibu kutaimarisha uhusiano
wa kiutendaji baina ya Serikali na hivyo kuimarisha Muungano.
178. Mshikamano (Solidarity) ni moja ya misingi muhimu ya utendaji katika
mfumo wa shirikisho. Msingi huu umezingatiwa katika Rasimu inayopendezwa ili
kuhakikisha kuwa Serikali zote tatu zinashikamana na kusaidiana katika kila
hali inayoweza kujitokeza. Mathalani, Ibara ya 62(3) inapendekeza kuipa
Serikali ya Muungano, kwa makubaliano na masharti maalum na Serikali ya Nchi
Mshirika, madaraka ya kutekeleza jambo lolote lililo chini ya mamlaka ya
Serikali ya Nchi Mshirika. Aidha, Ibara ya 65 na 66 zinapendekeza kuwepo kwa
ushirikiano baina ya Serikali za Nchi Washirika na kati ya Serikali hizo na
Serikali ya Muungano. Msingi huu ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wa
pande zote mbili za Muungano wananufaika kwa usawa na mshikamano baina ya Nchi
Washirika.
179. Msingi wa kutegemeana unakusudia kuweka utaratibu wa mamlaka za chini
kutekeleza majukumu yaliyo ndani ya uwezo wake ikiwa mamlaka hizo zina uwezo wa
kutekeleza majukumu hayo kwa ukamilifu. Msingi huu wa kutegemeana unaruhusu
mamlaka ya juu kutekeleza jambo ambalo kwa kawaida hutekelezwa na mamlaka ya
chini iwapo mamlaka ya juu ina uwezo wa kutekeleza jambo husika kwa ufanisi au
vinginevyo. Ibara ya 65 na 66 zimeweka msingi kwamba, ingawa Serikali ya
Muungano itakuwa na mamlaka ya kushughulikia Mambo ya Muungano, Serikali hiyo,
kwa ridhaa ya Serikali ya Nchi Mshirika, itakuwa na mamlaka ya kushughulikia
masuala yasiyo ya Muungano katika Nchi Mshirika. Msingi huu utasaidia
kuimarisha utendaji katika muundo wa Serikali Tatu unaopendekezwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
180. Muungano, pamoja na matatizo yote tuliyonayo, umedumu kwa miaka
hamsini. Kuna hofu kwamba muundo wa Serikali tatu utavunja Muungano. Baada ya
kutafakari kwa kina Tume inaamini hakuna msingi wa hofu hii.
181. Waasisi walikubaliana orodha fupi ya mambo ya Muungano, hasa yale ya
kidola. Hakukuwa na sharti kwamba Muungano utakuwepo tu kama mambo yote ya
Tanganyika yatawekwa chini ya Muungano. Ni Tanganyika kwa hiyari yake ilikubali
mambo yake yote yawe kwenye mamlaka ya Serikali ya Muungano. Sababu za kufanya
hivyo zilikuwa mbili. Sababu ya kwanza ilikuwa kupunguza gharama na sababu ya
pili ilikuwa matumaini kwamba siku ambayo hakutakuwa na hofu ya Zanzibar
kumezwa na Tanganyika, basi tungekuwa na Serikali moja badala ya Serikali
mbili. Hali halisi ilivyo hivi sasa inaonyesha kwamba hatutafikia azma ya kuwa
na Serikali moja.
182. Kuingiza mambo ya Tanganyika kwenye Serikali ya Muungano ndicho chanzo
kikubwa cha matatizo tuliyonayo. Sababu kubwa ya Zanzibar kudai mambo ya
Muungano yapunguzwe ni kutokana na hisia kwamba Serikali ya Muungano inaonekana
ni Serikali ya Tanganyika.
183. Hali hii inapunguza uzalendo na kuchochea utaifa. Kwa miaka hamsini
wananchi wameungana na wameimarisha udugu, umoja na mshikamano wao. Nchi
imejenga taasisi ambazo zimezoea kufanya kazi kwa pamoja na viongozi pia
wamejenga utamaduni wa kufanya kazi kwa pamoja. Mambo yote haya yamejenga
utamaduni wa taifa na kukuza uzalendo. Madhumuni ya kupendekeza muundo wa
Serikali tatu ni kuondoa kero ambazo zinahatarisha umoja, uzalendo na
mshikamano.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
184. Mwisho naomba kutoa shukrani zangu binafsi kwa Watumishi wa
Sekretarieti ya Tume na Wajumbe wenzangu. Tume imekamilisha kazi yake kwa muda
ulipangwa kutokana na kazi nzuri ya Sekretarieti. Wakati Wajumbe wa Tume
walipokuwa wanakusanya maoni mikoani, Watumishi wa Sekretarieti waliofuatana na
Wajumbe, walifanya kazi kwa muda mrefu sana, hata siku za mapumziko. Walikuwa
wa kwanza kuamka na wa mwisho kwenda kulala. Walihakikisha kwamba kila neno
lililosemwa na mtoa maoni limewekwa kwenye kumbukumbu. Madereva nao walifanya
kazi za ziada hata wakati walipokuwa wamechoka.
185. Watumishi waliobaki Ofisini, kila mmoja wao na kwa ujumla wao,
walifanya kazi kwa kujituma sana na waliweza kuziweka pamoja kumbukumbu
zilizotoka mikoani na kufanya maandalizi ya vikao vya wajumbe wa Tume. Kazi hii
waliifanya kwa haraka lakini kwa umakini mkubwa. Nawashukuru sana.
186. Nawashukuru sana Wajumbe wenzangu wa Tume, ikiwa ni pamoja na Makamu
Mwenyekiti, Katibu na Naibu Katibu wa Tume. Baada ya kuteuliwa na kuapishwa na
Mheshimiwa Rais, mimi kama Mwenyekiti, nilikuwa na wasiwasi mkubwa kama
tungeifanya kazi yetu kwa ufanisi na kwa wakati.
187. Tulikuwa katika makundi ya kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
Tulikuwa tumeteuliwa kutokana na mapendekezo ya makundi mbali mbali, Vyama vya
Siasa, Jumuiya za Dini, Asasi za Kiraia, Wanaharakati, Wanauamsho na kadhalika.
Tulikuwa na muono tofauti, itikadi tofauti, misimamo tofauti na imani tofauti.
Ilionekana dhahiri kuwa kazi yetu ingekuwa ngumu.
188. Bahati nzuri wenzangu wote walitambua changamoto hiyo. Mapema kabisa
tulitambua kwamba jukumu letu ni kulitumikia taifa, siyo makundi
yaliyotupendekeza au nafsi zetu. Tulikusanya maoni ya wananchi kwa msingi huo
bila kuchakachua. Mijadala yetu ilikuwa ya uwazi na ukweli.
189. Hata tulipopata matatizo ya kufikia uamuzi kwa suala lolote
hatukukimbilia kupiga kura. Tulijifungia kwenye vikundi vya watu wenye mawazo
kinzani na mwisho tukafikia maridhiano na muafaka. Dira yetu ilikuwa Maslahi ya
Taifa. Hatukupiga kura hata mara moja kwa jambo lolote wala kuwa na mawazo
mbadala. Kila Ibara iliyomo kwenye Rasimu ya Katiba ambayo ninaiwasilisha
katika Bunge Maalum la Katiba, inaungwa mkono na kila mmoja wetu.
190. Hiyo haina maana kwamba kila mmoja wetu ameacha imani yake, itikadi
yake na msimamo wake. Kuna mambo ambayo kila mmoja wetu amebaki na imani yake
na msimamo wake. Kwa mfano, kwenye suala la Muungano tupo tunaoamini muundo
unaofaa ni Serikali Moja, tupo tunaoamini Muundo wa Serikali Mbili, tupo
tunaoamini Serikali Tatu na tupo tunaoamini Muungano wa Mkataba. Tunachoamini
wote kwa pamoja ni umuhimu wa kuendelea kuwepo na kudumu kwa Muungano. Baada ya
kuwasikiliza wananchi, dira yetu imekuwa ni maslahi ya Taifa na siyo maslahi ya
makundi yetu au nafsi zetu. Nawashukuru sana wajumbe wenzangu wa Tume kwa
kusimamia misingi ya kiutendaji ambayo imetuwezesha kukamilisha kazi hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
191. Baada ya kusema hayo nimalizie, kwa niaba ya Tume, kukutakia wewe na
Waheshimiwa Wabunge kheri na fanaka katika kazi yenu muhimu. Jukumu lenu ni
kubwa na lina ugumu wake. Lakini, tunaamini mnao uwezo wa kufanya kazi yenu kwa
ufanisi, na mwisho, mtakubaliana kupendekeza Katiba ambayo itakidhi matakwa ya
wananchi na kuendelea kuliunganisha taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Naomba kuwasilisha Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
Post A Comment: