Huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda
mjini Mombasa pwani ya Kenya ambapo magaidi walivamia kanisa siku ya Jumapili
na kuwapiga risasi waumini, mmoja wa waathiriwa wa shambulizi hilo amefikishwa
Nairobi mwa matibabu maalum.
Shirika
la madaktari la AMREF, limemleta Nairobi Mtoto Cyprian Osinya aliye na miezi
kumi kutoka Mombasa kwa matibabu maalum ya upasuaji wa kichwa baada ya
madaktari kugundua kuwa risasi imekwama katika ubongo wake.
Mamake
aliyekuwa anamkinga kutoka kwa magaidi waliovamia kanisa hilo siku ya Jumapili
,alifariki kanisani humo baada ya kupigwa risasi. Inaarifiwa risasi
aliyomuingia kichwani Cyprian ilitoka kifuani kwa mamake na kuishia katika
ubongo wa mtoto huyo.
Mamake
Cyprian, alikuwa miongoni mwa watu sita waliouawa katika shambulizi hilo, baada
ya washukiwa watatu wa ugaidi kulivamia kanisa la Joy in Jesus katika mtaa wa
Likoni na kuanza kuwafyatulia waumini risasi kiholela.
Cyprian
atafanyiwa upasuaji maalum katika hospitali kuu ya Kenyatta mjini Nairobi.
Post A Comment: