Idadi ya waliofariki kufuatia shambulio la Likoni imeongezeka na
kufikia 6 huku 9 waliokua wakipokea matibabu wameruhusiwa kurudi nyumbani na 6
hao walifariki kufuatia majeraha ya risasi,Polisi nchini Kenya imesema bado
hawajafutilia mbali uwezekano wa kuwa lilikua shambulio la kigaidi.
Mwandishi wa habari kutoka Dw nchini Kenya anaelezea kwa
sasa kinachoendelea Mombasa>>’Hali ilivyo mjini Mombasa ni hali ya
kutatanisha kukosekana kwa usalama kwa sababu kama unavyojua tukio hili
limezua hofu sana hasa kwa wakazi wa mji huu wa Mombasa’
‘Nakumbuka tukio la watu 5 waliuwawa kwenye kanisa moja hapa
Likonyi ni kitendo kilichotokea siku 2 baada ya Waziri wa usalama kutoa taarifa
kwa wakazi wa hapa kuwa usalama utadumishwa’
‘Hali ni tete hapa Mjini Mombasa baada ya tukio hilo ambalo watu
hao waliuwawa msako wa polisi uliendelea kuimarishwa kuanzia saa 8 na msako huo
uliendelea usiku kucha na taarifa tulizopokea kwa sasa ni kwamba watu 59
wametiwa nguvuni’
‘Wasiwasi upo kwa sababu hiki ni kitendo kilichotengenezwa ndani
ya kanisa na unajua si mara ya kwanza kitendo hiko kutokea hapa Mombasa
nakumbuka fujo zilizozuka baada ya kitendo cha ugaidi kutokea hapa Mombasa
kuliokua na taharuki miongoni mwa wakazi wake hasa baina ya wakristo na
waislam’
‘Hiki ni kitendo ambacho watu wanahofia kimetekelezwa kuzua hofu
hasa miongoni mwa waumini wa dini hizo mbili lakini viongozi wa kidini wamekuja
pamoja na kusema kwamba hiki ni kitendo kilichofanywa na magaidi tu ili kuzua
mtafaruku miongoni mwa waumini baina ya wakristo na waislam hilo ni tukio
linaloendelea kuchunguzwa’
‘Hadi kufikia sasa hakujawa na taarifa za kuthibitisha kitendo
hiki kilitekelezwa kwa malengo gani na wakina nani hasa,hali ya wasiwasi mjini
Mombasa bado ipo na kama unakumbuka kuwa tukio hili limetokea siku chache baada
ya watu wawili kukamatwa wakiwa na mabomu Mabomu ambayo yaliharibiwa hivi juzi
tu kwa hivyo ni tukio linalozidi kutia hofu kwa wakazi wa Mombasa’.
Post A Comment: