MWANDISHI NGULI NA MWENYE KUFANYA VIPINDI VYA UCHUNGUZI NA KISIASA NCHINI TANZANIA , KATIKA UKURASA WAKE WA FACE BOOK LEO, NIMEKUTANA NA HABARI HII, SWALI AMBALO HATA MIMI MWENYEWE NIMEKUWA NAJIULIZA SIKU ZOTE SIPATI JIBU HEBU TUSAIDIANE MAJIBU WAUNGWANA MTAKAOPATA FURSA YAKUISOMA STORI HII KATIKA www.kuninews.blogspot.com
HAWA NDIO BOKO HARAM WANAODAIWA KUWA NA VIFAA VYA KISASA VYA KIVITA. |
HUYU NI RAIS BARAK OBAMA, RAIS WA NCHI KUBWA KIUCHUMI DUNIANI: AMERIKA. |
Na Dotto Bulendu.
Binafsi napata utata sana na haya makundi yanayotekeleza mauaji katika nchi mbalimbali hususani barani Afrika,kumekuwa na makundi ya waasi na haya tumepata kuyashuhudia katika nchi za Uganda, DRC Congo, Afrika ya kati, Mali, Misri, Kenya pia makundi yanayotajwa kuwa ni ya kigaidi kama AlQaeda,AlShabaab na Boko Haram Ntarahamwe nk.!..Makundi haya yamekuwa yanafanya mashambulizi ya kushtukiza na kusababisha mauaji ya watu wasio na hatia Duniani ,na hata dunia sasa inahangaika na kundi la Boko Haram,ambalo wakati dunia ikih...angaika kuwanasua mabinti waliotekwa, jana kundi hili limetajwa kutekeleza mauaji kwa kulipua bomu tena huko kaskazini mwa Nigeria na kusababisha vifo vya watu takribani zaidi ya 120, vikundi vya waasi na kigaidi barani Afrika vimekuwa vinatumia silaha za kisasa kupambana na majeshi ya serikali barani Afrika pamoja na kufanya mashambulizi....utata wangu upo katika maeneo haya.
1.Makundi haya ya silaha nzito,nani anawauzia?silaha hizo zinawafikiaje? tunajua silaha zote nzito zinatengenezwa na nchi zilizoendelea na siyo barani Afrika, je makundi haya yanazinunuaje hizi silaha? tunajua biashara za silaha ni biashara yenye faida sana, nahisi nchi za ulaya,marekani na asia zinazotegeneza silaha zinajua fika undani wa makundi haya.
2.Makundi haya yanaajiri vijana wengi, yanakaa mafichoni, yanapata wapi pesa za kununua silaha na malipo pamoja na posho kwa wapiganaji wake? yamehifadhi wapi fedha zao? nani anakwenda benki kuweka na kutoa pesa za makundi haya? naamini zipo taasisi za fedha ambazo zinaujua kwa undani uasili wa makundi haya!!tunajua pesa chafu zinaendesha baadhi ya mataifa.
3.Nani anafadhiri makundi haya? kwa nini makundi haya yanachomoza kwenye nchi zenye utajiri wa mafuta? na wakati makundi haya yakiendelea na uharibifu huu utajiri uliopo katika nchi hizo unaendea kuporwa na wanaopora hawaguswi wala kushambuliwa na makundi haya!
Nani yupo nyuma ya makundi haya? natafakari na karibuni wanajamvi tufanye tafakuri tunduizi(critical thinking),juu ya makundi ya uasi na ugaidi barani Afrika,nani anayafadhiri?ufadhiri wao unapitia wapi? wanatuza wapi fedha zao? wanapitishia wapi silaha zao?..natafakari sana!.
Toa maoni yako hata bila kutaja jina nasi tutayachapisha
Post A Comment: