MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKITOA MAELEKEZO KWA WATENDAJI. |
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Mgesa Mulongo, amewaagiza wakurugenzi wote kuhakikisha Ujenzi
wa vyumba vya Maabara unakamilika
ifikapo Novemba 30 na kinyume na hapo basi itabidi kila mmoja awajibike.
Mulongo
ameyasema hayo katika siku yake ya kwanza kikazi mkoani humo alipo wasili kwa
ajili ya kuripoti tangu alipoteuliwa na
Rais kushika wadhifa huo Novemba 5 mwaka huu.
Amesema
kwakuwa wenyeviti wa mabaraza ya madiwani wote walisha onesha nia kwa kusukuma
na kuhimiza ujenzi huo wa maabara na tayari kamati za fedha zilikwisha
idhinisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara lililopo kwa sasa ni kuhakikisha
mamlaka zinazo takiwa kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi zitekeleze majukumu yake huku akiwakazia sauti
wakurugenzi wa halmashauri.
Amesema
amekuja kuwaomba licha ya kwamba ni mgeni katika mkoa huo, huku akimuagiza
Katibu Tawala Mkoa kuhakikisha kuwa kila siku taarifa ya ujenzi wa maabara
zinawasilishwa mezani kwake na hatua zilizo fikiwa “Nimekuja kuwaomba na nazidi
kuwaomba nazidi kuwaomba tena leo natumia nafasi hii na ugeni wangu huu
kamalizeni maabara, alisema na kuongeza
kuwa ataendelea kulifatilia suala hilo kwa kufanya Monitoring yeye mwenyewe.
Aidha
amehimiza kuwa wakurugenzi wahakikishe taarifa hizo zinasainiwa na wakurugenzi wenyewe
na sio watumishi wengine wanao kaimu ofisi za wakurugenzi.
Ameawaambia
wakuu wa Wilaya ikifika tarehe 30 Novemba, kama hakuna maabara hajui ni hatua
zipi zitakazo fuata kwakuwa wakati
maelekezo yanatolewa na Rais wakuu hao wawilaya walikuwepo na kila mmoja
alisaini moyoni mwake kuhusiana na ujenzi wa maabara hizo.Mkuu huyo wa Mkoa alikuwa katika siku yake ya kwanza mkoani humo
Post A Comment: