Aagiza Shughuli za usafi zifanywe na Vikundi vidogo vidogo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo amekerwa na hali ya uchafu iliyopo katika mitaa ya Jiji la Mwanza na kuwaagiza  watendaji wa halmashauri hiyo  kuacha  kukaa ofisini na badala yake watoke na kwenda kuwasikiliza watu katika maeneo yao ya kibiashara. 
Mulongo ametoa kauli hiyo jijini Mwanza, mara baada yakufanya ziara yakutembelea maeneo yaliyotengwa  maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo Jijini humo na kukuta hali ya mazingira kiafya ikiwa hairidhishi.
 
Mkuu huyo wa mkoa akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa alitembelea maeneo ya Makoroboi, Soko kuu, Sahara na Standi ya Nyegezi.




MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKISHANGAA UCHAFU ENEO LA SOKO KUU.
AKIWA KATIKA ENEO LA MAKOROBOI, HAPA VIJANA WA SHULE WAKICHAGUA NGUO ZA MTUMBA




"HAIKUBALIKI KATIKATI YA JIJI PAWE NA HALI YA UCHAFU KIASI HIKI"- MULONGO




UKARABATI WA VIBANDA KATIKA ENEO AMBALO LIMEZUIWA KUFANYA BIASHARA NDOGO NDOGO

ZAWADI NAZO HAZIKUKOSEKANA (PICHA ZOTE NA OFISI YA MKUU WA MKOA)

MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA BARAKA KONISAGA AKITOA MAELEZO MBELE YA MKUU WA MKOA WAKATI WA ZIARA HIYO


ENEO LILILOKUWA NYUMBA YA NHC AMBAPO MKUU HUYO WA MKOA AMETOA SIKU HADI KUFIKIA TAREHE 30 DESEMBA LIWE LIMEENDELEZWA.


KWA MBALI MKUU WA MKOA AKITAZAMA JENGO LA MSIKITI WA JAMII YA WAHINDU AMBAPO WAFANYABIASHARA WAMEKUWA AKIFANYA BAISHARA BILA YA IDHINI YA SERIKALI.


HUU NDIO UCHAFU UNAO NYOOSHEWA KIDOLE NA MKUU WA MKOA WA MWANZA KATIKA ENEO LA STANDI YA TAX JIJINI HUMO.

KAZI NI UHAI KWA KILA BINADAMU, ASIYEFANYA KAZI NA ASILE(PICHA NA OFISI YA RC MWANZA.)

TUPO KAZINI WAJASIRIAMALI KATIKA ENEO LA MTAA WA SOKONI WAKIUZA SAMAKI AINA YA NEMBE.

MKUU WA MKOA ALIYE NYANYUA MWAMVULI KUMSIKILIZA BIBI ASIA RASHIDI ENEO LA SOKO KUU WAKATI WA ZIARA HIYO.(PICHA NA OFISI YA RC MWANZA)

MKUU WA MKOA AKISHUHUDIA WAKINA MAMA WAUZA SAMAKI KATIKA MTAA WA SOKONI.

 Aidha katika hatua nyingine ameuagiza uongozi wa jiji hilo kuhakikisha wana viainisha vikundi vidogo vidogo vinavyo undwa na vijana pamoja na kina mama ili viweze kukabidhiwa jukumu la kutunza mazingira badala ya kazi hiyo kuachiwa mawakala wa usafi ambao kwa namna moja au nyingine wameonekana kulemewa na jukumu hilo .

 
" Tunacho taka kuona ni hawa samaki wadogo wadogo na wao wanakuwa na kuvuka hatua hii waliyo nayo na kukuza mitaji yao, alisema Mulongo na kuongeza kuwa, wenye kutaabika na hali mbaya ya usafi sehemu zote ni hawa wanao kaa katika maeneo hayo.
Alitoa agizo hilo kwa uongozi wa Jiji la Mwanza kufuatia majibu yaliyo tolewa na Afisa afya wa jiji bw. Kamenya kwamba wao kama jiji huwalipa mawakala kiasi cha Tsh. 1000 kwa kila mita miatatu za usafi wanazo zifanyia usafi, suala ambalo lilizua mjadala na kumlazimisha mkuu wa mkoa kuugaiza uongozi wa jiji kuachana na mpango huo na badala yake wawatambue kwanza watu wanao kaa katika maeneo husika ndio wapewe jukumu lakutunza usafi " Pale Moshi, wenzenu walichofanya ni kuwaweka vijana na akina mama katika vikundi na kisha kuwaelekeza nini cha kufanya.

Amesema endapo vikundi hivyo vikiwezeshwa ndivyo vinaweza kufanya suala la usafi kupata suluhisho la kudumu la usafi,  kwakuwa watakuwa na uchungu wakimuona mtu yeyote anathubu kuchafua mazingira wao watakuwa wakwanza kumkemea na kumfikisha kwenye mamlaka husika kwa ajili ya hatua stahiki.
Mkuu huyo wa mkoa tangu aliporipoti na kujitambulisha amefatilia kwa karibu suala la ujenzi Maabara pamoja na hali ya usafi katika Jiji la Mwanza, ambapo siku zote amekuwa akinukuliwa akisema anataka kila mmoja atomize majukumu ya kazi aliyo ajiriwa nayo kwa ufanisi bila kutegea.
 

 

Axact

Post A Comment: