Kuongeza kiwango cha wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 68%-80% ifikapo desemba 2015, kuongeza kiwango cha huduma baada ya kujifungua ndani ya siku 7 kutoka 21% mpaka 62% ifikapo Decemba 2015, kuongeza kiwango cha watoto wanaozaliwa na kina mama wenye maambukizi ya VVU kutumia ARV (prophylaxis) kutoka 45% to 65% ifikapo Decemba 2015 kuongeza namba ya vituo vinavyotoaa huduma ya IMCI kutoka 69%-80% ifikapo Desemba 2015, mbali ya mikakati hiyo vilevile mkoa umedhamiria Kuboresha utoaji wa taarifa kwa wakati kutoka 66%-100% ifikapo Decemba 2015.
Na
Atley Kuni- Mwanza.
BARAKA KONISAGA ALIYEKUWA AMEMWAKILISHA MKUU WA MKOA WA MWANZA AKIFUNGUA KIKAO HICHO HAPA ALIKUWA AKISISITIZA JAMBO. BIBI SECILIA MREMA AKIJIBU BAADHI YA MASWALI MBELE YA WAANDISHI WA HABARI |
WAKUU WA WILAYA ZA MAGU JAQLINE LYANA (KULIA), DC SENGEREMA (KATIKATI) NA DC MISUGWI WAKIMSIKILIZA KAIMU MKUU WA MKOA WA MWANZA BARAKA KONISAGA HAYUPO PICHANI. |
MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA BARAKA KONISAGA ALIYE SIMAMA WAKATI AKIFUNGUA KIKAO HICHO KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA MWANZA. |
SECILIA MREMA AKITOA UELEKEO KUHUSU AFYA UZAZI MKOANI MWANZA WAKATI WA KIKAO HICHO. |
KAIMU MGANGA MKUU WA MKOA WA MWANZA DKT. KENGIA AKIJIBU BAADHI YA MASWALI YALIYO ULIZWA NA WASHIRIKI WA MKUTANO HUO |
Mkoa
wa Mwanza umejiwekea malengo makubwa ili kukabiliana na afya ya uzazi na malezi
bora kwa mtoto ili kuweza kufikia malengo ya milennia ifikiapo Desemba 2015.
Hayo
yamesemwa na bibi Secilia Mrema wakati akiwasilisha mada kwenye kikao cha
pamoja kilichokutana katika ofisi ya mkuu wa mkoa na wadau wa masuala ya afya
mkoani hapa kwa ajili yakupitia mipango waliojiwekea lakini pia kupeana
majukumu ili kuweza kufikia azma yao hiyo.
Mrema
amesena, kutokana na hali ya uzazi salama kuwa chini ukilinganisha na mikoa jirani
kama vile Kagera ndio maana wameamua kukaa pamoja ili waone kwa namna gani
wanaweza kutoka mahali walipo na kufikia malengo waliojiwekea ifikiapo mwishoni mwa 2015.
Amesema
kutokana na Uelewa mdogo juu ya njia za uzazi salama kwa watoa huduma na kwa jamii, Mila
na desturi zinazofanya utumiaji mdogo wa
huduma za afya ya uzazi na uzazi wa mpango, ushiriki mdogo wanaume ni baadhi sababu kubwa iliyo wasukuma kuja na
mikakati hiyo, lakini pia kutokana na mpango wa Tekeleza sasa kwa matokeo
makubwa (BRN) ni njia moja wapo ya visababishi vilivyo wafanya kuja na mikakati
hiyo “ Tunajua suala la afya ya uzazi ni jukumu la jamii nzima ndio maana
tumeona ni vema tuka kaa wadau wote tunao husika ili tuweze kuangalia kiunaga
ubaga mikakati hii tuliojiwekea.
Kutokana na changamoto hizi mkoa kwa kupitia
halmashauri za wilaya umejiwekea malengo yafuatayo
BWA SATANLEY MATOWO MMOJA YA WASHIRIKI KUTOKA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA |
Kupiga vita mila na desturi
zinazofanya utumiaji mdogo wa huduma za
afya ya uzazi kama vile, uzazi wa mpango, ushirikishwaji wa wanaume, Kuongeza kiwango cha wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya kutolea
huduma za afya kutoka 68%-80% ifikapo
desemba 2015, kuongeza kiwango cha
huduma baada ya kujifungua ndani ya siku 7 kutoka 21% mpaka 62% ifikapo Decemba
2015, kuongeza kiwango cha watoto wanaozaliwa na kina mama wenye
maambukizi ya VVU kutumia ARV (prophylaxis)
kutoka 45% to 65% ifikapo Decemba 2015 kuongeza
namba ya vituo vinavyotoaa huduma ya IMCI kutoka 69%-80% ifikapo Desemba 2015,
mbali ya mikakati hiyo vilevile mkoa umedhamiria Kuboresha utoaji wa taarifa
kwa wakati kutoka 66%-100% ifikapo Decemba 2015.
Mrema
amekwenda mbali zaidi nakusema ili waweze kufikia malengo waliojiwekea watatoa
mafunzo kwa watoa huduma kuhusu (njia za kisasa za uzazi wa mpango, huduma za
dharura wakati wa uchungu na kujifungua, huduma ya kumsaidia mtoto mchanga
kupumua baada ya kuzaliwa, IMCI, mtuha). Aidha kupitia vyombo vya habari
watatumia mwanya wakutoa elimu kwa umma ili wajue umuhimu wa afya ya uzazi
lakini pia kufanya mikutano mingi ya uraghabishaji kwa umma ili ufahamu umuhimu
wa masuala ya afya ya uzazi kwa mama na mtoto.
Mkoa
wa Mwanza ni mojawapo ya mikoa 6 inayo
unda kanda ya Ziwa ambao una wilaya ziapatazo saba zenye visiwa 68. Huku mkoa huo kwa mujibu wa sensa
ya watu na makaazi ya mwaka 2012 ikiwa jumla
ya watu wapatao 2,772,509, idadi ya watoto chini ya mwaka mmoja ikiwa ni
104,507, na watoto watoto chini ya miaka
5 ikiwa ni 516,998 huku wanawake wenye
umri wa kuzaa kwa maana ya umri kati ya miaka (14-49yrs) ni 677,100.
Mrema
amesema, wastani wa watoto katika familia ni 5.4 (Fertility rate), na ukuaji wa
wakazi kwa maana ongezeko la watu kimkoa ikiwa ni 3.2% kwa mujibu wa sense ya
2012, aidha mkoa pia una jumla ya vituo
vya kutolea huduma za afya 360 kati ya hivyo vituo 263 (73) % vinatoa huduma za
afya ya uzazi na mtoto.
Awali
akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo katika hotuba yake
iliyosomwa na Mkuu wa Wilya ya Nyamagana alisema ni jukumu la kila mmoja wetu “kujihoji
ni kwa vipi mama apoteze maisha ili hali kila mmoja wetu anajua kuwa mama ndiye
anaye tengeneza maisha”? aidha amesema
kuwa kutokana na lengo la nne la millennia kugusa suala nyeti kama hili ndio
maana kama taifa tayari tathimini
ilifanyika ambapo Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara, Makatibu Tawala na Waganga
Wakuu wa Mikoa Tanzania walikutana na Mheshimiwa Rais tarehe 15 Mei, 2014 na kupewa
taarifa ya tathimini hiyo na kujadili mkakati mpya ulioboreshwa wa kitaifa
katika kufikia lengo la 4 na la 5. Ifikapo mwishini mwa mwaka 2015, “Pamoja na
mengine tuliyokubaliana mbele ya Mheshimiwa Rais, suala la uwajibikaji lilipewa
kipaumbele ambapo kila mmoja wetu aliweza kupata uzoefu wa mikoa mingine, mfano Singida
na Mara jinsi walivyofaulu katika suala la afya ya uzazi.
Kikao
hicho cha siku moja kimewakutanisha Viongozi wa dini, wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi
wa halmashauri, wenyeviti wa halmashauri, waganga wakuu wa wilaya na waratibu
wa afya ya uzazi wa wilaya pamoja na wataalam kutoka sekretarieti ya mkoa wa
Mwanza.
Imeandaliwa
na Afisa habari- Mwanza
Post A Comment: