JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI
ZA MITAA
MKOA WA MWANZA
Anwani ya Simu:
“REGCOM”
OFISI YA MKUU WA MKOA,
Simu
Na:028-2500686/2500690 S.L.P. 119,
Fax
028- 2501057/2541242 MWANZA
TAARIFA
KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI.
MKUU
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewaagiza Wakurugenzi
Watendaji wa Halmashauri ya Jiji, Manispaa na Wilaya za Mkoa wa Mwanza kuwasilisha
Hati za Malipo ya Mishahara (Pay roll) za watumishi wao wote waliopo kazini kwa
ajili ya kuanza zoezi la uhakiki watumishi hao.
Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake leo, wakati alipokutana nao kwa ajili ya kujitambulisha,
alisema katika agizo hilo amewataka Wakurugenzi kuwasilisha Pay roll hizo
ofisini kwa Katibu Tawala wa Mkoa tarehe 05 Aprili, 2016 kabla ya saa 6:00
mchana.
Amesema mara baada ya
kuwasilishwa kwa hati hizo za malipo, zitakabidhiwa kwa Kamati maalum ambao
ataiunda kwa ajili ya kupita kwenye halmashauri zote kuwahakiki watumishi wote
waliopo kazini hata wale ambao wapo masomoni au nje ya vituo vyao vya kazi.
Zoezi hili la uhakiki wa
watumishi wote ni muendelezo wa ufuatiliaji wa watumishi hewa katika mkoa wa
Mwanza kufuatia zoezi la awali kukamilika na kubainika kuwa na watumishi hewa
wapatao 334.
“Katika zoezi hili,
tutakuwa tukihakiki wafanyakazi wote waliopo kwa kuonana ana kwa ana kamati nitakayoiunda na kabla ya
kuanza wakurugenzi watapaswa kuwataarifu watumishi walio nje ya kazi kama;
likizo, safari, masomoni au nje ya nchi kurejea wakati wa zoezi hilo kwa ajili
ya kuhakikiwa wakiwa na nakala tatu za picha za Passport Size.
“Nimesha muagiza Katibu
Tawala wa Mkoa, kuwafahamisha haya wakurugenzi wote kuwasilisha Pay roll zote
mezani kwake ili kamati nitakayoiunda kwenda kufanya uhakiki, kukutana nao moja
kwa moja (physical),” alisema Mongella.
Alisema zoezi hilo
litachukua muda wa siku saba kwa kila halmashauri na baada ya hapo ripoti
kamili itatolewa. Aidha alisema hatoshangaa kuona idadi ya watumishi hewa
ikiongezeka au kupungua kwani katika uhakiki huu watapitia kwa kina watumishi
wote
Katika hatua nyingine
Mongella, amewataka waandishi wa habari katika mkoa wa Mwanza kutoa ushirikiano
wa kutosha pale wanapokuwa na taarifa za kusaidia kufichua uhalifu ili
kuimarisha ulinzi na usalama wa mkoa.
“Mwandishi wa habari
hatofautiani na kachero wa Polisi, sasa tusaidiane kuongoza huu mkoa kwakupeana
taarifa, maana mkoa huu ni mkubwa, sio rahisi kwa Mkuu wa mkoa kujua yote yanayoendelea
hadi ngazi ya kijiji lakini kwa kuwa ninyi wenzangu mnao wigo huo basi
tusaidiane ili watu katika mkoa huu waweze kufanya kazi zao kwa amani na
salama. Amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza.
Imetolewa;
Atley
J. Kuni
AFISA HABARI NA UHUSIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA WA
MWANZA
Aprili 04, 2016.
Post A Comment: